Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 6824

VIJANA NCHINI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KUTATUA TATIZO LA AJIRA

$
0
0
unnamed2
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Riwa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo aliyesimama akitoa mada ya ujasiriamali kwa Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga na jinsi ya kujikomboa kiuchumi.
unnamed1
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa (katikati) akiongea na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga Bw. Oscar Yapesa kuhusu ziara ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa Manispaa ya Mbinga, wa kwanza kushoto ni Afisa Vijana kutoka Wizarani Bi. Amina Sanga.
…………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga wameaswa kushirikiana na Serikali katika kutafuta suluhisho la tatizo la ajira nchini ili waweze kujikomboa kiuchumi.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Riwa wakati wa mafunzo elekezi kwa Vijana wa Halmashauri hiyo ya jinsi ya kujikwamua kiuchumi.
Bi. Riwa alisema vijana wengi wamekuwa wakilalamikia ugumu wa maisha na kuacha kujishughulisha na ujasiriamali hivyo kupelekea kukabiliana na ugumu wa maisha.
Katika mafunzo hayo Bi Riwa alisema vijana wengi nchini wamekuwa wakitaka kupatiwa pesa bila kuzingatia mafunzo ya elimu ya ujasiriamali hivyo kupelekea upotevu na usumbufu katika urejeshaji wa marejesho.
“Nasikitishwa na baadhi ya vikundi vya vijana katika Halmashauri mbalimbali wamekuwa wakigomea mafunzo ya ujasiriamali na kudai posho za mafunzo na kusahau mafunzo wanayapatiwa ni muhimu kuliko hiyo posho mnayoihitaji.
Katika mafunzo hayo Bi. Riwa alisema Serikali haitoi posho za mafunzo ya ujasiriamali bali hutoa elimu na baadae kutoa mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa kisheria.
Katika hatua nyingine Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga alisema ili vijana waweze kupatiwa mikopo wanatakiwa kujiunga katika vikundi na kuunda SACCOS ya Halmashauri ya vijana ambayo itasimamiwa na vijana wenyewe.
Alisema katika utoaji mikopo vigezo mbalimbali huzingatiwa ikiwa ni pamoja na umri wa kuanzia miaka kumi na tano mpaka thelathini na tano.
Akizungumzia kigezo cha umri Bi. Sanga alisema kigezo hicho ni kwa mujibu wa Sera ya maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 ambapo sera hiyo inamtambua kijana ni kuanzia umri wa miaka 15 mpaka 35.
Kuhusu suala la urejeshaji wa mikopo yote Bi Sanga alisema ni wa kipindi kisichozidi miaka miwili na muda wa maandalizi miezi mitatu ambapo kikundi kitalazimika kulipa tozo ya asilimia 15 iwapo kitashindwa kurejesha mkopo katika muda uliopangwa.
Hivyo amewataka vijana kuandika maandiko ya kupatiwa mikopo kwa ushirikiano na Afisa Vijana wa Halmashauri yao na maandiko yao yatawasilishwa Wizarani na kuchambuliwa kwa ajili ya kupatiwa mikopo kwa vikundi vitakavyokidhi vigezo ambapo kikomo cha mkopo kwa kikundi ni kiasi kisichozidi shilingi miloni kumi kulingana na uhalisia wa mradi wa kikundi husika.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 6824

Trending Articles