Mgeni Rasmi , Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Benson Mpesya akisisitiza jambo kwa wadau kuhusiana na umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) katika uzinduzi wa sheria ndogo ya Mfuko huo wilaya Ushetu.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Constantine Makala akiwasalimia wadau wa Wilaya ya Ushetu baada ya kukaribishwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Ushetu.
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hawa Duguza, akiwasilisha mada ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa wadau katika uzinduzi wa sheria ndogo ya Mfuko wa Afya Ya Jamii wilayani Ushetu.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Shinyanga, Bwana Imanuel Amani akisisitiza umuhimu wa wana ushetu kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) katika shughuli ya wadau wa Mfuko huo wilayani Usheto.
Wadau wakifuatilia kwa makini mada iliyokua ikiwasilishwa na Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
…………………………………………………………………….
…………………………………………………………………….
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha wananchi wengi wananufaika na bima ya Afya umeshirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga kuanzisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF)
Uzinduzi wa mchakato wa kuanzisha sheria ndogo uliambatana na siku ya wadau wa afya wilayani ushetu ambao umefanyika katika ukumbi wa halmshauri ya wilaya na mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Benson Mpesya.
Katika uzinduzi huo kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mh.Benson Mpesya alisitiza kuhusu umuhimu wa viongozi wa mkoa na wadau wa afya kuhakikisha wananchi wanajiunga kwa wingi kwenye mfuko huu kwani ndio mkombozi wa Afya zao.