Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all 6866 articles
Browse latest View live

MWIGULU NCHEMBA NAYE ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

$
0
0

Mwigulu Nchemba akitangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea Urais kupitia CCM jioni hii mkoani Dodoma.
NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ametangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea Urais jioni hii kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika Ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo kwenye Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Kauli mbiu ya Mwigulu ni ‘Mabadiliko ni Vitendo Wakati ni Sasa.’
Katika hotuba yake Mwigulu ameanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, wazee, ndugu zake, wananchi wake wa Iramba na wananchi wote waliohudhuria hafla hiyo ya kutangaza nia.
Mwigulu pia amempongeza Rais Kikwete kwa kumuamini na kumteua katika nyadhifa mbalimbali.
Amesema ameamua kutangaza nia akiwa mkoani Dodoma ili kuondoa dhana ya ‘ukwetukwetu’ iliyozoeleka miongoni kwa viongozi. Aongeza kuwa Dodoma ni makao makuu ya taifa na chama chake ndiyo maana amefanya hivyo.
Aidha Mwigulu ameeleza mambo matatu yaliyomsukuma kutangaza nia kuwa ni pamoja na:
-Kutaka Mabadiliko
-Kujua mbinu za mabadiliko
-Utayari wa kufanya mabadiliko.
Pia kiongozi huyo amekemea viongozi wanaochaguliwa kwa mazoea wakisingizia uzoefu kwa kueleza kuwa kiongozi anayechaguliwa kwa mazoea ataongoza kwa mazoea na atafanya kazi kwa mazoea maana uzoefu ni mazoea.
Kiongozi huyo ameeleza jinsi anavyozijua fika shida za Watanzania na umasikini walionao hajausoma kwenye vitabu bali ameishi maisha ya umasikini.
Mwigulu ameeleza pia alivyobeba zege baada ya kumaliza chuo kikuu na mke wake akiwa mama ntilie akiwapikia yeye na vibarua wengine wa ujenzi.


STEPHEN WASSIRA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

$
0
0

Stephen Wassira akitangaza nia ya kuwania Urais kwenye Ukumbi wa wa BOT jijini Mwanza leo.
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira leo ametangaza nia ya kuwania Urais kwenye Ukumbi wa wa BOT jijini Mwanza.
Wassira anawania nafasi ya kugombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika hotuba yake wakati wa kutangaza nia yake, Wassira amesema amepata kuteuliwa kuongoza sehemu mbalimbali nchini maana marais wote wa awamu nne walikuwa na imani naye.
Pia amewashukuru wageni waalikwa waliofika kwenye ukumbi kutoka sehemu mbalimbali kwa kuweza kufika na kumuunga mkono huku wakiwa na imani naye.
Kauli mbiu yake ni katika mbio hizo ni Uchumi Imara kwa Tanzania mpya.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA MARIAN BAGAMOYO

$
0
0
B2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
ba1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo,  kwa pamoja wakikata utepe kuzindua Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
ba3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, kwa pamoja wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduzi  wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
ba4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu, katika Ibada maalum ya uzinduzi  wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
ba5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian, baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo Mei 31, 2015 mjini Bagamoyo. Picha na OMR
BA7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, baada ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
BA8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, baada ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
BA9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo na baadhi ya viongozi na waumuini  baada ya kuzindua rasmi Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
BA10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkandarasi wa majengo ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian wakati akitembelea kujionea ramani ya Chuo hicho baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo mjini Bagamoyo. Picha na OMR
BA11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na baadhi ya waumini wa Dini ya Kikristu, baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo chuoni hapo mjini Bagamoyo. Picha na OMR

WAZIRI MEMBE AWASIHI WATANZANIA KUTOCHAGUA VIONGOZI WANAOSAKA UONGOZI KWA KUTOA RUSHWA

$
0
0
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimkabidhi Bi. Shamim Khan tuzo ya heshima ya kujishughulisha na kazi za kijamii hapa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Sheikh Ismail Mohamed wakati wa tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe  akizungumza katika tamasha hilo la kwanza Qaswida, lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa,Mh Membe amewataka Watanzania kusubiri kwa hamu siku ya kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,

Alisema siku hiyo ya Juni 6, wananchi wasikilize nini anataka kuifanya nchi iweze kuondoka ilipo ikiwemo kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo. “Mkae tayari siku hiyo, naamini uongozi mzuri wa nchi ni ule wa kudumisha amani na utulivu na ili nchi iweze kusonga mbele, maadili kwa viongozi ni muhimu,” alisema Waziri Membe.

Membe alitumia nafasi hiyo kuwasihi Watanzania kuacha kuchagua viongozi ambao kwa nje, wanajinadi  wana dini, lakini matendo hayaendani na maadili ya  dini zao. Alisema ili mtu aweze kuaminika kuwa ana dini, jamii ifuatilie katika madhehebu yao, hivyo amewasihi wasichague viongozi wanaosaka uongozi kwa kutoa rushwa.

“Msikubali kuwa na viongozi ambao kwa nje, wanaojinadi kuwa na dini kinyume na matendo yao, lazima mchague wenye hofu ya Mungu ambayo husisitizwa na dini zote,” Alisema uongozi wa heshima ni ule unaochukia rushwa ambayo ni adui wa haki, hivyo amewataka wananchi kuwaogopa wapenda rushwa kama ukoma. 
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria tamasha hilo.
Baadhi ya Washiriki waliofika kwenye tamasha hilo la kwanza la Qaswida.
Baadhi ya Washiriki waliofika kwenye tamasha hilo la kwanza la Qaswida.
Mmoja wa washiriki wa tamasha la Qaswida kutoka Madrasa ya Nur-Pugu,Samiu Mussa akighani Qaswida mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kwenye tamasha hilo,lililodhaminiwa na kampuni ya Dira  ya Mtanzania
Kikundhi cha Qaswida kiitwacho Iqhyau wakighani Qaswida ya maadili
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.Bernard Membe akipokelewa na wenyeji wake alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,kwa ajili ya kushiriki tamasha la kwanza la Qaswida
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulamaa Qaswida Promotions ambao ndio waandaji wa tamasha la kwanza la Qaswida,Ustaadh Jumanne Ligopora akimkaribisha mgeni rasmi  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.Bernard Membe 
Sheikh Ismail Mohamed akizungumza jambo na Waziri Membe wakati wa tamasha la kwanza la Qaswida lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.
Waimbaji wa Qaswida kutoka kikundi cha Muumini cha Buguruni jijini Dar es Salaam wakiimba kwenye tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania. 

TAWLA YAANDAA CHAKULA CHA JIONI KUADHIMISHA MIAKA 25 TANGU IANZISHWE

$
0
0
01
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Mh. Anjela Kairuki na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade wakiangalia uzinduzi wa mpango Mkakati wa Chama hicho wa mwaka 2015-2020 uliozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na chama hicho kwenye hoteli ya Hyyat Regency Dar es salaam kutimiza miaka 25 tangu chama hicho kianzishwe hapa nchini, ambapo wanasheria wanawake na waheshimiwa Majaji walialikwa katika hafla hiyo.
02
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Mh. Anjela Kairuki akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regecy Dar es salaam
IMG_3079
Mh. Jaji Winnie Korosso akizungumza na wageni waalikwa Wanasheria wanawake wakati wa hafla ya TAWLA ya kutimiza miaka 25 tangu ianzishwe. 
2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Mh. Anjela Kairuki akimsikiliza  Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade
4
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo.
8
Kamishna wa TRA Bw. Rasheed Bade kushoto akijumuika na wageni waalikwa wanasheria wanawake katika hafla hiyo.
9
Baadhi ya majaji wakiwa katika hafla hiyo.
10
Waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo
11
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Mh. Anjela Kairuki kulia akiwa pamoja na  Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade, kulia ni Mkurugenzi wa TAWLA Tike Mwambipile.
IMG_3043
Bendi ya Skylight ikitumbuiza katika hafla hiyo.
IMG_3045
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Aisha Bade kushoto na  Mkurugenzi wa TAWLA Tike Mwambipile wa tatu kutoka kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanasheria wa TAWLA. 
IMG_3047

Baadhi ya wafanyakazi  wakiwa katika picha ya pamoja

HOTEL YA DOUBLETREE BY HILTON YA JIJINI DAR YAFANYA USAFI WA MAZINGIRA YANAYOIZUNGUKA HOTEL HIYO

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa Hotel ya Double Tree by Hilton nchini Tanzania, Bw.Ian Mclachan (wa pili kutoka kushoto) akifanya usafi katika ufukwe wa Bahari inayoizunguka Hoteli ya Double Tree huku akishirikiana bega kwa bega na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Hoteli ya Double Tree By Hilton, Bw. Yehia Elmansoury (wa kwanza kushoto).
Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Double Tree by Hilton, Bw. Florenso Kirambata(kushoto) akifanya usafi wa mazingira katika fukwe inayoizunguka hoteli hiyo ya jijini Dar es Salaam huku akiwa pamoja na mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo.
Baadhi ya uchafu uliokuwa katoka fukwe ya Bahari inayoizunguka Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar.
Wafanyakazi wa hoteli ya Double Tree ya jijini Dar es Salaam wakifanya usafi maeneo yote yanayoizunguka hoteli hiyo
Viongozi na wafanyakazi wa Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya Hotel hiyo mara baada ya kumaliza kufanya usafi. Picha na Geofrey wa Pamoja Blog

PROF. LIPUMBA ATANGAZA KUGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA UKAWA

$
0
0
 MWENYEKITI wa Chama cha wananchi CUF, Prof Ibrahim Haruna Lipumba huenda akaingia kwa mara ya tano katika mbio za kutaka kuingia Ikulu ya Tanzania endapoUmoja wa Katiba ya WananchiUKAWA utampitisha kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
 
Lipumba ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo ya juu kisiasa nchini, akisema ana sifa zote lakini hatakuwa na kinyongo iwapo UKAWA haitapitisha jinalake kugombea urasi na atampigia kampeni atakaepitishwa.
Profesa Lipumba, anakuwa mwanasiasa wa tatu kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutangaza nia hiyo baada ya mwenyekiti wa NLD, Emmanuel Makaidi na Dk George Kahangwa wa NCCR-Mageuzi kujitokeza kutaka kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano.
Mwanasiasa mwingine aliyejitokeza kuwania urais Tanzania ni Maxmillan Lyimbo wa TLP, wakati Hamad Rashid wa Alliance for Democratic Change (ADC) na Maalim Sharrif Hamad wa CUF wametangaza kuwania urais wa Zanzibar.
Lipumba, ambaye atakuwa akiwania urais kwa mara ya tano, iwapo atapitishwa na Ukawa ambayo imeamua kusimamia mgombea mmoja atakayeungwa mkono na vyama vinne, alitangaza nia yake juzi mjini Tabora wakati wa mikutano yake ya hadhara ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.

DK. SLAA AKIKAGUA UANDISHWA BVR- VWAWA- MBOZI, MBEYA

$
0
0
wil1
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk, Wilbroard Slaa (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mwandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Mailosy Bukuku namna mashine ya BVR zinavyofanya kazi katika kituo cha Igamba Wilayani Mbozi, Mbeya jana.
wil2
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk, Wilbroard Slaa (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mwandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Eldah Chakachaja namna mashine ya BVR zinavyofanya kazi katika kituo cha Igamba Wilayani Mbozi, Mbeya jana wakati Dk Slaa alipfanya ziara ya kutembelea vituo vya kujiandikia wananchi wilayani Mbozi Mbeya.
wil3
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk, Wilbroard Slaa (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mwandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Eldah Chakachaja namna mashine ya BVR zinavyofanya kazi katika kituo cha Igamba Wilayani Mbozi, Mbeya jana wakati Dk Slaa alipfanya ziara ya kutembelea vituo vya kujiandikia wananchi wilayani Mbozi Mbeya.
wil4
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk, Wilbroard Slaa , akizungumza na wananchi waliojikeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga katika kijiji cha Igamba wilayani Mbozi jana. SOURCE: Fullsahangwe.

TAMASHA LA KOMAA CONCERT LILIVYOFANA NDANI YA KIOTA CHA MARAHA CHA DAR LIVE JIJINI DAR.

$
0
0
 Uongozi pamoja na Wafanyakazi wa kituo cha radio ya EFM 93.7 kwa pamoja wakikata keki kusherehekea kutimiza mwaka mmoja wa kituo hicho ambacho kwa sasa kinakuja kwa kasi jijini Dar na kwingineko,hafla hiyo ilikwenda sambamba na kuadhimisha miaka 16 ya msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature,katika tamasha lililoitwa  KOMAA CONCERT,ambalo lilifanyika ndani ya kiota cha maraha cha Dar Live,Mbagala jijini Dar mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki na wapenzi wa muziki . 
 
Lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa Juma Nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM  ilikuwa pia ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo Juma Nature aingie kwenye game ya Muziki nchini Tanzania.
 
Baadhi ya Wasanii walioshiriki kulinogesha tamasha hilo ni pamoja na Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi. Katika tamasha hilo lililowavutia wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake,kiingilio kilipangwa kuwa ni shilingi 7,000 tu. 
 
Meneja Mwasiliano na mambo ya Sheria wa EFM 93.7 Deniss ssebo alisema kuwa wanaamini Msanii Juma nature ni msanii mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya,alisema na kuongeza kuwa lakini kwa Efm huyo ni msanii wa Kwanza tu na itaendelea kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwa kuwa wanaaamini Muziki unaongea. 
Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akiongoza jopo la wafanyakazi wenzake kukata keki 
Pichani kulia ni Meneja Mwasiliano na mambo ya Sheria wa EFM 93.7 Deniss Ssebo akizungumza jambo mbele ya mwashabiki na wapenzi wa muziki na pia wasikilizaji wakubwa wa kituo hicho kuhusiana na utaratibu mzima wa sherehe hiyo,kulia ni Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akigawa keki kwa mashabiki waliofika kushuhudia tukio hilo ndani ya Dar Live. 
 Msanii
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akitumbuiza jukwaani
mbele ya mashabiki wake,pia akiwashukuru kumpa sapoti ya kutosha tangu
ameanza muziki na sasa anatimiza miaka 16 katika tasnia hiyo adhimu.
Wakongwe pamoja  Juma Nature na Prof.Jay wakishoo love kwa mashabiki wao.
Msanii Snura na Madansa wake wakilishambulia jukwaa la KOMAA CONCERT.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Shetta akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la KOMAA CONCERT.
 Mashabiki walikuwa kibao. 
 Burudani ilipangwa sawa bin sawia huku Ma -Mc wakinogesha shughuli
ya Dar Live kwa usiku huo ndani ya jicho la samaki
 Dar Live palinoga usiku huo wa KOMAA CONCERT .
PICHA NA MICHUZI JR.

TAARIFA YA MAKUSANYO UJENZI YA MSIKITI

$
0
0
Kwa Jina la M/Mungu nina anza Andika , Nawashukuru Ndugu zangu WA TANZANIA ,KENYA na wasio kuwa hao kwa Upamoja wao wa Michango yao ya hali na Mali katika Kuimarisha UJENZI WA MSIKITI UNAONA KATIKA PICHA . 

Nakushukuru BLOGS ZOTE ZA TANZANIA shukran za Pekee kwa Brother Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog kwa kuwa Balozi Mzuri wa kulitangaza Jambo hili kwa Jamii pamoja na Blogs nyingi Marafiki wa Father Kidevu Blog. Leo Tarehe 30/5/2015 NAOMBA NIULETE MREJESHO HUU KWENU WA MAKUSANYO TOKA TAREHE 19/5 mpaka Tarehe 29/5/2015. 
Na niwaombe Wadau kurudi tena kuleta mrejesho kama huu M/Mungu akipenda Tarehe 15/6/2015 .
UFUATAO NI MREJESHO WA MICHANGO YA UJENZI WA MSIKITI ULIOPO MKOA WA PWANI , WILAYA YA  MKURANGA , KIJIJI CHA MLAMLENI , KITONGOJI CHA KIMBANGULILE .
Naomba Nianze Ijumaa , Tarehe 29/5/2015 . TUMEPATA KIASI CHA TSHS 238,700/=
  1. CASH :- Tshs 96,700/= Nimezipokea Western Union.
  2. Tigo -Pesa Tshs 142,000/= Jumla ya Pesa zote unapata Tshs 238,700.
  3. TULIZOKUSANYA TSHS 1,373,500/= tukijumlisha na Siku ya Ijumaa Tarehe 29/5 tunapata TSHS 1,612,200/=
  4. Katika hiZo Pesa Taslimu ni Tshs 1,470,200/= na Tigo -Pesa 142,200/=
JUMLA YA MAKUSANYO YOTE Tshs 1,612,200/= 
Balozi wetu wa KENYA Ali Bajiy Nasor update zake zitawajia atakapo kusanya Ahadi alizopewa Mpaka sasa amekusanya KSHS 4300/= ambae anakusanya kupitia M-PESA NAMBA +254725113783. ( Usajili ALI HAMIS ) .
Balozi wetu kwa waliopo Uingereza Tafadhali wawasiliane kwa Namba hii muwasilishe Michango yenu +447460340624.
Tanzania CHANGIA KUPITIA TIGO PESA 0715800772 (Brother ALI )
Mawasiliano zaidi Tuwasiliane Whatsapp : +255689604780 au Tembelea Facebook ID yetu :- Kijana Wa Kiislam Dsm
NAWASHUKURU WOTE MLIO CHANGIA NA MTAKAO ENDELEA KUCHANGIA KWA HALI NA MALI , kwa Pamoja TUIJENGE NYUMBA YA IBADA MALIPO YAKE AKHERA NI MAKUBWA ZAIDI NA DUNIANI PIA UNAPATA .
Daima Jamii ya watu huwa Nzuri zaidi na ikishikamana na IBADA na KUMTAMBUA MUUMBA kama Ni hivyo basi kwa PAMOJA TUUJENGE MSIKITI HUU tupate kuwa na Jamii Njema. 
Wabillahi Taufiqh.
Wako katika Usimamizi wa hili . 
GHALIB NASSOR MONERO.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AWEKA JIWE LA MSINGI NYUMBA 50 ZA GHARAMA NAFUU ZA NHC MJINI KAHAMA

$
0
0

Hizi ni miongoni mwa nyumba 50 za gharama nafuu zilizojengwa na  NHC katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula katika halmashauri ya Mji Kahama mkoani Shinyanga.  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mh.William Vangimembe Lukuvi ameweka jiwe la msingi katika nyumba hizo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mh.William Vangimembe Lukuvi akiwasili kuweka jiwe la msingi zilizojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Mjini Kahama.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi(aliyevaa miwani) akiweka jiwe la msingi katika nyumba  zilizojengwa na NHC Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

 
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akielekea kwenye ya mfano ili kuikagua na kukata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Mjini Kahama.
 Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC  Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa nyumba 50 zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ulioanza kujengwa mwezi Januari mwaka 2015 na kutarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2015.
 Waziri Lukuvi akitizama michoro ya mradi wa nyumba 50 utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.1 unaotekelezwa na NHC Wilayani Kahama. 
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kuzindua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Mjini Kahama. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Felix Maagi. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mh. William Lukuvi  akikagua  majengo ya nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Wilayani Kahama akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi (kushoto).   Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi baada ya kukagua moja ya majengo hayo 50 yaliyojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Wilayani Kahama.
 Mh. William Vangimembe Lukuvi (wa pili  kulia) akirudi jukwaani baada ya kukagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Kahama.
 Waziri Lukuvi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua na kukagua nyumba za gharama nafuu za NHC Mjini Kahama.
 Meza Kuu- Waziri Lukuvi akitazama kikundi cha ngoma wakati alizindua nyumba za gharama nafuu za NHC Mjini Kahama lengo likiwa la kupendezesha mandhari ya miji yetu, kupandisha hadhi ya maeneo lakini pia kuwapatia wananchi wa kipato cha chini nyumba bora na gharama nafuu.

 Kundi la sanaa la Makhirikhiri la Kahama wakitoa burudani
 Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Benson Mpesya akizungumza eneo la Bukondamoyo na kulipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kujenga nyumba za kisasa na imara na kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali katika halmashauri za wilaya nchini.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC,,  Bw. Felix Maagi akizungumza eneo la Bukondamoyo ambapo alisema halmashauri zitakazotoa ushirikiano na kuwa tayari kununua nyumba ndizo zitazojengewa nyumba na NHC. Bw.  Felix Maagi, alisema pia kuwa mradi huo umetengeza ajira za moja kwa moja 290, ajira shirikishi 145 na makazi ya watu 300.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kahama katika eneo la mradi wa nyumba 50 zilizojengwa na  NHC katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Wilayani Kahama. Alizitaka Halmashauri za Wilaya kupima maeneo ya Miji na kuyagawa kwa wananchi kwa utaratibu unaotakiwa ili kuondoa migogoro ya ardhi na kuweka mipango miji vizuri.

 Mbunge wa Jimbo la Kahama Mh. James Lembeli akizungumza katika eneo la mradi ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa ya nyumba hizo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kibiashara katika eneo hilo ili fedha za watu watakaoishi hapo zisitoke nje ya eneo hilo.

 Waziri William Vangimembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wealiohudhuria uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Mjini Kahama.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. William Lukuvi  akiondoka eneo la tukio akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.  Felix Maagi 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe  Lukuvi akiagana na Mbunge wa Jimbo la Kahama Mh. James Daudi Lembeli mara baada ya kuzindua nyumba za gharama nafuu eneo la Bukondamoyo.

CCM MOSHI VIJIJINI WAMPONGEZA MWENYEKITI MPYA WA MJI MDOGO WA HIMO HUSSEIN JAMAL.

$
0
0

Mwenyekiti Mpya wa mji mdogo wa Himo,Hussein
Jamal akiwasili katika ukumbi wa King size katika mji wa Himo kwa
ajili ya sherehe ya kupongezwa baada ya kufanikiwa kushinda kiti
hicho.


Baaadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi
waliofika katika sherehe ya pongezi kwa mwenyekiti wa mji mdogo wa
Himo.
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa
Himo wakiwa katika sherehe hizo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya
Moshi vijijini Miriam Kaaya akizungumza wakatio wa sherehe za
kumpongeza mwenyekiti wa mji mdpgo wa Himo ,Hussein
Jamal.
Kamanda wa Uhamasishaji wilaya ya Moshi
Vijijini Hassan Hussein,akizungumza wakati wa sherehe
hizo.
Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha
Mapinduzi kutoka wilaya ya Kinondoni,
Mzee Shayo maarufu kama King size
akimpongeza naibu kamanda wa jumuiya ya Vijana wilaya ya Moshi
vijijini ,Innocent Melecky  kwa uamuzi wake wa kutangaza nia ya
kutaka kugombea jimbo la Vunjo.

Viongozi wakiimba nyimbo za pongezi
.
Mwenyekiti mpya wa mji mdogo wa Himo
,Hussein Jamal akizungumza na wananchi waliofika katika sherehe za
pongezi zilizofanyika katika ukumbi wa King size uliopo mji mdogo wa
Himo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya
Kaskazini.

PINDA AKUTANA NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA MAREKANI, APOKEA GARI LA WAGONJWA

$
0
0
MIZ1
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gari la kubeba wagonjwa lililotolewa na kampuni ya  Sayed Corporation Limited  kwa ajili ya hospitali ya  Endulen ya Ngorongoro . Gari hilo lilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Juni 1, 2015 na  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Masood  ur Rehman Sayed (kulia kwake) jijini Dar es slaam .  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MIZ2
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Marekani, Ofisi kwake jijini Dar es salaam Juni 1, 2015. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje,Liberata Mulamula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MIZ3
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Marekani baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini Dar es salaam Juni 1, 2015. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa Kimataifa, Liberata Mulamula.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU KATIBU MKUU CHADEMA,ZANZIBAR SALUM MWALIM ATUNUKU VYETI KWA WANACHAMA WA CHASO MKOA WA KILIMANJARO

$
0
0

Naibu Katibu mkuu wa Chadema taifa upande wa
Zanzibar Salum Mwalimu akizungumza wakati wa mahafali ya Chaso mkoa wa
Kilimanjaro yaliyofanyika katika shule ya sekondari
Majengo.

 

Baadhi ya wanachama wa Chaso  kutoka
vyuo mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katimsikiliza Naibu katibu
mkuu wa Chadema taifa,upande wa Zanzibar Salum Mwalimu wakati wa
sherehe za umoja huo.


Wakili wa kujitegemea Elikunda Kipoko
(katikati) akisikiliza kwa makini hotuba ya Naibu katibu mkuu Zanzibar
,Salum aliyoitoa wakati wa mahafali ya kuhitimu kwa wanafunzo wa vyuo
vikuu ,wanachgama wa Chaso. 
Mbunge wa Viti maalum Lucy Owenya (Chadema)
katikati akiwa na Diwani wa kata ya Longuo ,Raymond Mboya (Kushoto) na
kulia kwake ni aliyekuwa katibu wa Chadema wilaya ya Moshi
vijijini.Aquiline Chuwa .
Aliyekuwa katibu wa Chadema wilaya ya Moshi
vijijini,Aquilene Chuwa akizungumza katika mahafali
hayo.
Naibu katibu mkuu Chadema Zanzibar,Salum
Mwalimu akitunuku yeti kwa wanafunzi wana tarajia kumaliza elimu ya
chuo kikuu ambao ni wanachama wa Chaso mkoa wa
Kilimanjaro.
Mratibu wa Chaso aliyemaliza muda wake
,Ibrahim Chotola  akizungumza wakati akiaga nafasi hiyo rasmi na
kukabidhi kwa mratibu mpya wa Chaso mkoa wa
Kilimanjaro.
Chotola akifanya utambulisho wa mratibu mpya
wa Chaso mkoa wa Kilimanjaro Malijoel Mali.
Mratibu mpya wa Chaso mkoa wa Kilimanjaro
,Malijoel Mali akitoa salamu ya chama chake mara baada ya kukabidhiwa
rasmi mikoba ya kufanya shughuli za Umoja huo.
Na

Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDERICK SUMAYE ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

$
0
0

 Waziri Mkuu mstaafu  Sumaye akiwa na mke wake 
Ester Sumaye wakati wa mkutano huo wa kutangaza nia.
 Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (kulia), akizungumza na wanahabari na wadau wengine wakati akitangaza nia hiyo.
 Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (katikati), akiwa meza kuu. Kutoka kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kiluvya, Juma Semendu Nauchiwa. Kada wa CCM, Shabani Uronu, Mama Ester Sumaye na Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Charles Kaenja.
 Mwanahabari Ibrahim Yamola akimuuliza swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia ya nafasi hiyo.
  Mwanahabari Mariam Mziwanda akimuuliza swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia ya nafasi hiyo.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
 Msanii Oscar Nyerere akitoa burudani katika mkutano huo.
 Wananchi wakimpongeza Waziri Mkuu mstaafu Sumaye baada ya kuzungumza nao.
 Msanii Shafii Omari akitoa burudani.
Makada wa CCM na wadau wengine wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mhe. Fredrick Sumaye ametangaza nia ya kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar leo.
Sumaye amesema kuwa ameamua kutangaza nia akiwa Dar es Salaam maana anataka kuwatumikia Watanzania wote siyo wa nyumbani kwake pekee.Kauli mbiu yake ni ‘Uongozi Bora, Komesha Rushwa, Jenga Uchumi’.

Kiongozi huyo amesema ametangaza nia baada ya kujipima, akajitafakari na kujiridhisha kuwa anatosha kuwania nafasi hiyo.Sumaye amesema dira ya taifa katika miaka 10 ijayo ni kwamba Tanzania ifikie uchumi wa kati.

Aidha kiongozi huyo ametumia muda huo kuelezea kiongozi anayetakiwa na Watanzania kuwa:
-Kwanza ajipime, ajitafakari na ajiridhishe kuwa anatosha nafasi hiyo 
-Ajipime kiafya, kiakili, kimaadili na kidhamira

-Mzalendo, anayejua tulipotoka na tunapotaka kufika
-Kiongozi ambaye ni mtumishi atakayewatumikia wananchi na si bosi
-Kiongozi anayefikiri na kushauriwa 
-Kiongozi anayeweka maslahi ya Tanzania mbele na si yake binafsi
-Kiongozi atakayelinda amani ya Tanzania na Muungano wake.
-Mwenye uwezo wa kusimamia uchumi
-Atakayeboresha huduma za jamii zisizobagua watu.

-Atakayesimamia elimu ya Tanzania kurejea ilipokuwa hapo awali na kuiendeleza zaidi
-Atakayepambana na rushwa, ujangili na madawa ya kulevya.

Mhe. Sumaye pia amewatupia swali baadhi ya makada wa CCM waliotangaza nia na kudai kuwa wanauchukia umasikini hivyo kuamua kuutafuta utajiri Ikulu ambapo amewataka kama wanataka utajiri upo mitaani waende wafungue makampuni. (Habari wa Hisani ya Global Publishers).(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

KAMISHNA WA MADINI AZITAKA TAASISI ZA MAZINGIRA NCHINI KUONGEZA USHIRIKIANO KWENYE MIGODI

$
0
0
1
Mijiolojia wa Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe akizungumzia sekta ya madini  nchini kabla ya kumkaribisha  Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje  ili aweze kufungua mafunzo kwa wataalam wa Wizara. Mafunzo hayo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi kutoka Ofisi za Madini Nchini  na kufanyika Bagamoyo mkoani Pwani, yanatolewa na Taasisi ya  Sayansi na Mazingira kutoka  India, lengo likiwa ni kubadilishana  uzoefu na kuwapa uelewa katika usimamizi wa mazingira kwenye migodi.
2
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini akifungua mafunzo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi kutoka Ofisi za Madini Nchini yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
3
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini (wa kwanza kushoto, waliokaa mbele) pamoja na washiriki wengine wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka  Taasisi ya  Sayansi na Mazingira kutoka Nchini India (hawapo pichani) katika mafunzo kuhusu usimamizi wa mazingira migodini yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
4
Sehemu ya wataalam kutoka Idara ya Madini iliyopo chini ya  Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada kuhusu usimamizi wa mazingira kwenye migodi katika nchi  ya India iliyokuwa inawasilishwa na mtaalam mwelekezi kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh (hayupo pichani) kwenye mafunzo  hayo.
5
Mtaalam kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Srestha Banerjee akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.
6
Mtaalam mwelekezi kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh akisisitiza jambo katika mafunzo hayo.
7
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini (wa tatu kutoka kushoto, waliokaa mbele), Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara  ya Nishati na Madini,Mhandisi  Gideon Kasege ( wa pili kutoka kulia, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo  hayo.

PROFESA SOSPETER MUHONGO ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

$
0
0


Leo ni zamu ya Profesa Sospeter Muhongo kutangaza nia ya kuombwa kugombea urais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, kurithi mikoba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Profesa Muhongo anatangaza nia yake leo Mjini Musoma, kwenye Ukumbi wa Open University Hall, kuanzia saa 10 jioni.

MWILI WA MAREHEMU MZEE SAMWELI NTAMBALA LWANGISA WAPOKELEWA BUKOBA, MAJONZI YATANDA KWA WANABUKOBA.

$
0
0

Gari maalum kutoka Nchini Uganda lililobeba Mwili wa Mzee Samwel Ntambala Lwangisa ukiingia Bukoba. 
Na Faustine Ruta, Bukoba
Mwili wa Marehemu Samuel Ntambala Luangisa uliwasili usiku wa kumkia leo katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera. Mauti yalimkuta akiwa Nchini Marekani na maziko yake itakuwa kesho jumatano june 3,2015. Wakati wa Uhai wake Marehe Samwel Luangisa aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa wa Kagera (ukiitwa ziwa magharibi), Aliwahi pia kuwa mbunge wa Bukoba Mjini, Meya wa Bukoba na Diwani wa Kata ya Kitendaguro hadi mauti yalipomkuta.
Mtoto wa Marehemu Bi. Murungi
Kulia ni Mbunge wa Bukoba Mjini Mh. Khamis KagashekiNi majonzi na huzuni.

RAIS KIKWETE ZIARANI FINLAND

$
0
0
1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi Dorah Msechu katika uwanja wa ndege wa Helsinki alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu ya nchi hiyo
2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi wa FinladDorah Msechu katika uwanja wa ndege wa Helsinki alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu ya nchi hiyo
3
Rais Jakaya Kikwete akitembelea maabara ya majaribio ya kampuni ya kutengeza lifti ya KONE jijini Helsinki, Finland.
4
Rais Jakaya Kikwete akitembelea maabara ya majaribio ya kampuni ya kutengeza lifti ya KONE jijini Helsinki, Finland.
5
 Akipokea zawadi ya jezi ya timu ya taifa ya Finland ya basketball
6
JK akitoa zawadi ya mchoro wa Tingatinga kwa viongozi wa kampuni ya KONE
7
JK akitembelea  bandari ya Helsinki
9
Rais Kikwete akipata mapokezi Rasmi kwa mwenyeji wake Rais wa Finland Mhe Sauli Niinisto
10

TIGO YAZINDUA DUKA MOSHI MJINI

$
0
0
LE1Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas T. Gama akiongea na waandishi wa habari na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tawi la Tigo Moshi Mjini jana, wengine kulia Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Novatus Makunga na kushoto Meneja wa Ubora huduma kwa Wateja Tigo, Mwangaza Matotola.
LE2Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas T. Gama aikata utepe kuzindua rasmi Tawi la Tigo Moshi Mjini jana, wanaoshuhudia kulia ni Gwamaka Mwakilembe, Meneja huduma kwa wateja Kanda ya Kaskazini na kushoto ni Meneja wa ubora huduma kwa wateja Tigo, Mwangaza Matotola.
LEO4Meneja huduma kwa wateja Kanda ya Kaskazini, Gwamaka Mwakilembe akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama juu ya bidhaa zilizopo ndani ya Duka la Tigo lililozinduliwa Moshi Mjini jana.
LEO5Meneja wa Ubora huduma kwa Wateja Tigo, Mwangaza Matotola akiongea na waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo Moshi Mjini, wengine kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama na kulia Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Novatus makunga.
LEO7Meneja wa Mawasiliano Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Duka la Tigo moshi Mjini.
LEO8Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Novatus Makunga akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Tawi la Tigo Moshi Mjini, wengine kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama, Katibu wa Mkuu wa Mkoa Daniel Mchomvu na kulia ni Meneja wa ubora hudma kwa Wateja Tigo, Mwangaza Matotola
LEO9
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuini ya Tigo wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Leonnidas Gama wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo moshi Mjini.
Viewing all 6866 articles
Browse latest View live