Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all 6824 articles
Browse latest View live

MKUTANO WA 6 WA WADAU WA GEPF WAANZA LEO JIJINI TANGA

$
0
0

Mgeni Rasmi katika Mkutano wa sita wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Adam Malima akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Mkutano huo, ulioanza leo Mei 28, 2015 kwenye hoteli ya Regal Naivera, Jijini Tanga. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni "Mafao Bora kwa Maisha yako ya Sasa na ya Baadae".PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Daud Msangi akizungumza wakati akitoa utambulisho wa wageni mbali mbali waliohudhulia kwenye Mkutano wa sita wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, ulioanza leo Mei 28, 2015 kwenye hoteli ya Regal Naivera, Jijini Tanga. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Joyce Shaidi akitoa taarifa ya Bodi yake kwa wanachama na wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, wakati wa Mkutano wa sita wa Mwaka wa Mfuko huo, ulioanza leo Mei 28, 2015 kwenye hoteli ya Regal Naivera, Jijini Tanga. 
 Mgeni Rasmi katika Mkutano wa sita wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Adam Malima (kushoto) akizindua rasmi Mafao Mapya yatowewayo na Mfuko huo, mara baada ya kuufungua Mkutano huo.Wengine pichani toka kulia Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Daud Msangi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Juma Muhimbi pamoja na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Joyce Shaidi.
Picha ya pamoja.
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Aloyce Ntukamazina akielezea jambo juu ya muonekano wa logo mpya ya Mfuko huo, iliyozinduliwa rasmi leo Mei 28, 2015 kwenye hoteli ya Regal Naivera, Jijini Tanga. 
 Muwakilishi wa Wakuu wa Mifuko ya Hifadhiza Jamii nchini, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PPF, William Erio akitoa shukrani kwa Mgeni Rasmi pamoja na wadau wote waliohudhuria kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho pia alipata wasaa wa kutoa salamu zake kwa wadau wote waliohudhuria kwenye Mkutano huo.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa sita wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Adam Malima (wa pili kushoto) akikabidhi tuzo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, SACP Zuber Mwombeji kwa niaba ya Jeshi la Polisi lililoongoza kuwa wachangiaji bora wa Mfuko huo.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa sita wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Adam Malima akimkabidhi tuzo Mwanachama wa GEPF anaechangia kwa hiari, Chipegwa Chitojo.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa sita wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Adam Malima akimkabidhi tuzo wakala wa Mfuko wa GEPF, Said Omar Mwagajiko.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Daud Msangi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Juma Muhimbi wakati wa Mkutano wa sita wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, ulioanza leo Mei 28, 2015 kwenye hoteli ya Regal Naivera, Jijini Tanga.

Baadhi ya Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii wakiwa kwenye Mkutano huo.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh. Joshua Nassary akifatilia kwa makini Mkutano huo.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa GEPF, Anselim Peter akifatilia ufunguzi wa Mkutano huo.
Sehemu ya Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF wakiwa kwenye Mkutano huo, ulioanza leo Mei 28, 2015 kwenye hoteli ya Regal Naivera, Jijini Tanga. 
Burudani ya ngoma.
Picha ya pamoja na Viongozi mbali mbali.
Picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya GEPF.
Picha ya pamoja na Washindi wa Tuzo za Uchangiaji bora.
Wadau na Wanachama wa Mfuko wa GEPF.
Picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Mfuko wa GEPF.

WAZIRI MAHENGE:ASILIMIA 61 YA ARDHI NCHINI IMEHARIBIKA, AIRTEL YAPIGA JEKI SIKU YA MAZINGIRA

$
0
0
ASILIMIA 61 ya ardhi nchini imeharibika kutokana uharibifu wa mazingira ya ardhi  katika vyanzo vya mbalimbali na kusababisha kuzama kwa baadhi ya viziwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira,Mhandisi Binith Mahenge wakati akitangaza maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani  yatakayofanyika Juni 5 mwaka  huu mkoani Tanga.  Mahenge amesema Juni 5 ya kila mwaka iliamuliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1972 kuwa Siku ya mazingira duniani kutokana na kuonekana baadhi  ya vyanzo vinapotea kutokana na uchafuzi mazingira.

Amesema mikoa ambayo imekuwa kame kutokana na uharibifu wa mazingira ni Dodoma,Shinyanga,Geita,Singida,Simiyu na Kilimanjaro huku kasi yaukataji miti ikiwa inaongezeka na kufikia hekta 400, 000  kupotea kila mwaka nchini. Waziri huyo ameunga mkono kwa Kampuni ya simu za mikononi Airtel kuungana kuadhimisha siku ya mazingira kwa kuchangia kutoa elimu kwa njia ujumbe mfupi.

Afisa Mawasiliano na Matukio wa Airtel,Dangio Kaniki,amesema watatoa
ujumbe mfupi kwa ajili ya kutoa elimu kwa katika kuhamasisha utuzaji
wa mazingira na kutaka makampuni mengine yajitokeze kuunga juhudu za
utuzaji wa mazingira. Dangio,amesema ujumbe mfupi wataotoa katika utuzaji wa mazingira katika maadhimisho hayo ni zaidi ya Sh.milioni 90 ambazo Airtelingepata kutokana na kutuma ujumbe huo.
 
  Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (katikati) akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (kushoto)akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa RaisDk. Julius Ningu msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel  Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayokitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika haflafupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni AfisaUhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kushoto) na(kulia) ni Meneja Uthibiti wa Airtel, Calvin Simba
  Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (wa pili kulia)   akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhandisi Angelina Madete msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) na (kulia) ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO DAR

$
0
0
 Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidiana na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto), kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa TBL katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi huo, Balozi mstaafu Herman Mkwizu na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
 Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidiana na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto), kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa TBL katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi huo, Balozi mstaafu Herman Mkwizu na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
 Viongozi hao wakipongezana baada ya makabidhiano ya kisima hicho
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Kilindo akielezea mikakati mbalimbali ya kampuni hiyo katika kusaidia jamii hasa katika sekta ya maji kutokana na faida ya mauzo ya vinywaji vyao.
 Herman Mkwizu ambaye Kampuni yake ya Winners inajishughulisha na uboreshaji wa miundombinu ya maji akielezea jinsi watakavyoendelea kuusimamia mradi huo wa maji.
 Ofisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Ilala, Rehema Msologoni akishukuru kwa niaba ya Serikali baada ya kupokea msaada wa kisima hicho kutoka TBL.
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mshana akiishukuru  TBL kwa msaada huo wa kisima ambao ni muhimu mno hasa kwa wanafunzi wenye ulemavu wa shule hiyo waliokuwa wakiteseka kutafuta maji.
 Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu  akizungmza wakati wa hafla hiyo
 Wanafunzi wakifurahia kukabidhiwa mradi huo
 Wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Abisina Rashid (kulia) na Rozalia Polycarp (wa pili kulia), wakishiriki katika uzinduzi wa kisima cha maji kwa kufungua maji baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima hicho kwa shule hiyo Dar es Salaam  juzi. Kisima hicho kitakachohudumia pia Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa ujenzi wake ulisimamiwa na Kampuni ya Winners. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi wa kisima hicho, Balozi mstaafu,Herman Mkwizu, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wa pili kushoto),Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.
 Ofisa Elimu Taaluma Manispaa ya Ilala, Rehema Msogoloni (wa pili kulia) akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Zarina Kigoma baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam  juzi.Anayeshangilia kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana.Kisima hicho kitakuwa kinahudumia pia Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akinywa maji ya bomba baada ya kukabidhi msaada wa kisima kwa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Ofisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Ilala, Rehema Msologoni na Mkurugenzi wa Kampuni ya Winners iliyosimamia ujenzi wa kisima hicho.
Mwanafunzi mwenye ulemavu wa kuona akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo muhimu kwao.

TIGO NA HUAWEI ZATOA MSAADA WA KOMPYUTA 10 NA HUDUMA YA INTANETI KWA SHULE YA MSINGI CHUDA MKOANI TANGA

$
0
0
ta1
Meneja Mahusiano kwa Umma wa kampuni ya Huawei Jin Liguo akiongea na waandishi , Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi Chuda wakati wa sherehe za kukabidhi kompyuta 10 zenye inteneti ya bure ya Tigo kwa shule hiyo iliyopo mkoani Tanga, Msaada huo ulitolewa na Kampuni ya Tigo kushirikiana na Kampuni ya Huawei. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles ,Mwalimu Mkuu wa Shule ya Chuda Omari Masukuzi na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula.
ta2
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles akikabidhi msaada wa  Kompyuta zenye intaneti ya bureya Tigo kwa  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chuda Mkoani Tanga Bw. Omari Masukuzi hiyo ni moja kati ya kompyuta 10 zilitolewa na kampuni ya Tigo pamoja na Huawei kwa shule hiyo. Wanaoshuhudia wa pili toka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula, Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa Huawei  Jin Liguo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Abdallah Suleiman.
ta3
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles akiongea na waandishi , Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi Chuda wakati wa sherehe za kukabidhi kompyuta 10 zenye inteneti ya bure ya Tigo kwa shule hiyo iliyopo mkoani Tanga, Msaada huo ulitolewa na Kampuni ya Tigo kushirikiana na Kampuni ya Huawei. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Magalula Said, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Chuda Omari Masukuzi.
ta4
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chuda Mkoanin tanga wakipokea Kompyuta kwa niaba ya wenzao ambazo zilitolewa na kampuni za Tigo na Huawei.
ta5
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo
ta6
Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula akiongea na waandishi , Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi Chuda wakati wa sherehe za kukabidhi kompyuta 10 zenye inteneti ya bure ya Tigo kwa shule hiyo iliyopo mkoani Tanga
ta7
Mwalimu wa shule ya Chuda Bi.Teddy Simba akipokea simu kwa niaba ya wenzake toka kwa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula. Simu hizo zitawaweza walimu wa shule hiyo kuweza kuwasiliana wao kwa wao na kuperuzi intaneti  bila gharama yeyote kwa kupitia mtandao wa Tigo.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MAGARI YA UKUSANYAJI TAKA YA KAMPUNI YA GREEN WASTE PRO LTD YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.6

$
0
0
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akiwa ameshika mwenge baada ya kufika mtaa wa Kisutu jijini Dar kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kuzoa taka katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na na kampuni ya Green WastePro ltd. Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza jambo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika eneo la Kisutu jijini Dar kwa ajili ya ufunguzi wa Magari ya kisasa ya kuzoa taka.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa magari ya kufanyia usafi yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro ltd.
Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni kiongonzi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2015 , Bw. Juma Khatibu Chum (hayupo pichani).
 Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (kushoto) akikabidhiwa risala na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena iliyosomwa wakati wa uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
9
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiwa kwenye zoezi la kuweka uchafu kwenye moja ya gari la kufanyia usafi lililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Mmoja wa viongozi wa Mbio za Mwenge akizungumza mara baada ya uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro Ltd aliwasisitiza wananchi kuendelea kutumia kampuni hiyo kwani usafi utaendelea kuimarika zaidi na zaidi.
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (wa pili kutoka kushoto), Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy(katikati) Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo( wa pili kutoka kulia) pamoja na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw. Abdallah Mbena wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika eneo la Kisutu jijini Dar.
Mmoja wa viongozi wa mbio za mwenge akiwa ameshikiria Mwenge wa Uhuru tayari kwa kuondoka mara baada ya kumaliza uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi mali ya kampuni ya Green Waste Pro Ltd inayofanya kazi za usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndugu Isaya M. Mngurumi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akiwa na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena wakiwa wanatoa maelezo juu ya uzoaji na usindikaji wa Taka zinazokusanywa katika sehemu mbalimbali za Manispaa ya Ilala na jinsi ya watakavyoyatumia magari hayo yaliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
……………………………………………………………………..
Akizungumza wakati wakati wa tukio la uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi ya Kampuni iliyopewa zabuni kusafisha manispaa ya Ilala, Green Waste Pro Ltd Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi amesema kushirikiana vyema kwa kampuni Green Waste Pro Ltd ndiko kunako pelekea maendeleo na afya bora katika manispaa ya Ilala hivyo tuwaunge mkono wenzetu kwa kuwapa ushirikiano wa kuto tupa taka hovyo bali maeneo husika yaliyo wekwa kwaajili ya kuhifadhi taka hizo ili waweze kuzipitia kwa urahisi na kuzipeleka mahala panapo husika.

ATCL YAONGEZA SAFARI ZAKE VISIWA VYA COMORO.

$
0
0
Na Mwandishi wetu
………………………………………
Dar es Salaam: May 29, 2015: SHIRIKA la ndege la taifa (ATCL) limetangaza  uamuzi wake wa kuongeza idadi ya safari zake kuelekea visiwa vya Comoro hatua inayolenga kuendana  na ongezeko la mahitaji ya huduma za shirika hilo hususani katika kuelekea kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa sasa shirika hilo linatoa huduma zake kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma na Mtwara kila siku. Sambamba na kutoa huduma hizo hapa nchini, shirika hilo lina mpango mpya utakaoanza rasmi tarehe mosi ya mwezi Juni mwaka huu kwa kuongeza safari zake kuelekea visiwa vya Comoro hadi kufikia mara nane kwa wiki ikiwemo mara mbili siku za Alhamisi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Bw. Johnson Mfinanga alisema shirika hilo ndilo pekee linalotoa huduma ya safari za anga kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro huku akibainisha fursa za kibiashara zilizopo kati ya nchi hizi mbili jambo linalosababisha uwepo wa ongezeko la mahitaji ya huduma za ATCL.
Pia amewaasa watanzania hususan wakazi wa mtwara kuchangamkia fursa hizo kwa kuwa shirika hilo kwa sasa linatoa huduma zake kati ya Mtwara na visiwa vya Comoro kwa siku za Jumatano na Ijumaa kila wiki.
“Siku zote tumekuwa tukihakikisha kwamba tunabadilika kuendana na mahitaji ya wateja wetu. Ni dhahiri kwamba katika kipindi hiki kuna hitaji kubwa la usafiri wa anga kuelekea visiwa vya Comoro kwa sababu za  kibiashara, mapumziko na sherehe mbalimbali, hivyo ATCL imejipanga kuchangamkia fursa hiyo,’’ alibainisha.
Akizungumzia ufanisi wa shirika hilo katika safari nyingine ikiwemo zile za Kigoma na Mtwara, Bw. Mfinanga alisema wamekuwa wakihudumia idadi kubwa ya abiria kutokana na ndege za shirika hilo kusafiri kwa mwendo kasi wa kuridhisha sambamba na huduma nzuri zinazotolewa kwa wateja wakati wa safari.
“Zaidi tunaamini kwamba huduma tunazozitoa kati ya Tanzania na Comoro zimekuwa zikichangia kuongeza ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na tunaamini kuwa hata hili ongezeko la safari zetu kwenye mataifa haya mawili zitatoa fursa kwa wateja wetu kufaidi fursa zinazopatikana ndani ya nchi hizi,’’ aliongeza Bw. Mfinanga
Kuhusu mpango wa shirika hilo kujipanua zaidi kihuduma, Bw. Mfinanga alisema:  “Ndege yetu aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 kwa sasa inafanyiwa marekebisho makubwa kwenye karakana yetu iliyopo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa Julius Nyerere (JNIA) na itakapokamilika tutaendelea na huduma zetu katika mikoa ya Mwanza, Tabora, Kilimanjaro na Mbeya,’’
Bw. Mfinanga aliongeza kuwa kwa kufanya safari zake kuelekea visiwa hivyo shirika hilo limekuwa likiwezesha wateja wake kunufaika na fursa zilizopo kwenye visiwa hivyo huku pia akitoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza kushiriki katika kuchangamkia fursa hizo.

SKYLIGHT BAND KUTUMBUIZA LEO KATIKA LUKAS PUB

$
0
0
Waimbaji wa Skylight Band wakiendelea kutoa burudani ya kukata na shoka kwenye stageni na moja ya nyimbo zao
Joniko Flower naye katika muziki wa live hashikiki kwa sauti,viuno mpaka pumzi ni hatareeeee
sakata lumba na sky light band hapana chezea hatareee ukigusa lazima unase
Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao ndani ya kiota cha Lukas pub
baada ya kuonekana kukunwa na burudani inayotolewa na band ya sky light mashabiki wakaanza kulisakata
wajanja wote tunakutana skylight band kila weekend kutupa shida chini na kuweka mikono juu huku viuno tukiwa hatuvisahahu kuvino sasa

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA HEDHI DUNIANI

$
0
0
1
Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi Madina Juma, akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya mnazi mmoja. Kauli Mbiu ya mwaka huu inaeleza “Usisite kuzungumzia hedhi”.
23
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya hedhi duniani yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inaeleza “Usisite kuzungumzia hedhi”
…………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Tanzania imeadhimisha siku ya hedhi duniani, ambapo wizara ya elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekubaliana kuandaa na kusimamia sera inayoondoa vikwazo kwa watoto wa kike katika masomo yao.
Akizungumza katika maadhimisho hayo jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Elimu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Madina Kemilembe, alisema kukosekana kwa miundombinu rafiki mashuleni kunasababisha wanafunzi kutohudhuria masomo.
Alisema ukosefu wa mazingira bora kama vyoo, maji safi na salama pamoja na vyumba mahsusi vya kubadilishia nguo , hasa kwa watoto wa kike wanapokua katika hedhi mashuleni kunachangia utoro.
“Nawashukuru wadau Water Aid, Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV), Kasole Secrets pamoja na wengine kwa kuisaidia serikali kuandaa mazingira rafiki kwa watoto wetu kwa kuwajengea vyumba vya kubadilishia na kuhakikisha upatikanaji wa pedi kwa baadhi ya shule,” alisema Kemilembe.
Alisisitiza juu ya utoaji wa elimu kwa wazazi na wanafunzi wa jinsia zote ili kuondoa unyanyapaa ili kuboresha mazingira ya kusoma kwa mtoto wa kike.
Naye Mkurugenzi wa Water Aid, Ibrahim Kabole, alisema kuna uelewa mdogo pamoja na mila potofu zinazofanya jambo la hedhi kuonekana ni la aibu.

WIZARA ITAPUNGUZA KWA ZAIDI YA NUSU GHARAMA ZA UPIMAJI ARDHI ILI KILA MWANANCHI AWEZE KUPIMA ENEO LAKE NA KUPATA HATI- MHE WILLIAM LUKUVI

$
0
0
1
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali mkoani Tabora leo kuhusiana na masuala yanayohusu sekta ya ardhi mkoani humo katika ukumbni wa mikutano wa Isike. Kulia ni mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua
4
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora, kuhusiana na mgogoro wa Ardhi unaowakabili wananchi hao ambao unaotokana na Manisapaa kutowalipa fidia ya maeneo yao.
5
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya akijadiliana jambo wakati Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvu alipotembelea eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora kusikiliza matatizo ya Ardhi yanayo wakabili wananchi wa eneo hilo leo.
……………………………………………………………
Na Clarence Nanyaro
Kuanzia mwaka ujao wa fedha,serikali itapunguza gharama mbalimbali za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwezesha wananchi wengi kupima maeneo yao na kupata hati miliki ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo imekithiri hapa nchini.
Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora,Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati suala ambalo litapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa inatokea.
Aidha Mh Lukuvi aliongeza kuwa sambamba na kupunguza migogoro ya ardhi, serikali pia itaweza kukusanya bkwa wingi kodi ya pango la ardhi na hivyo kuongeza mapato amabayo yataisiaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo.
Hata hivyo pamoja na kupunguza gharama hizo Wazrizi Lukuvi aliwaonya Maafisa ardhi,kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu,akitolea mfano wa maafisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa linaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.
“Maafisa ardhi lazima wafanye kazi kwa kuzingatia taratibu ili kuepusha migogoro ambayo inatokea miongoni mwa wananchi na kuwasababisha kuichukia serikali yao” alisema Mh Lukuvi na kuongeza kuwa atakayebainika kukiuka taratibu atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu.
Waziri Lukuvi yuko mkoani Tabora kwa shughuli za kikazi,ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa anatafuta suluhu ya migogoro ya ardhi katika manispaa ya Tabora ambapo alikutana na wananchi wa maeneo ya Malabi,Uledi,Malolo na Kizigo ambako kumekuwa na migogoro ya ardhi kutokana na baadhi ya wananchi wa maeneo hayo kutolipwa fidia baada ya Manispaa ya Tabora kupima viwanja katika maeneo hayo.
Akiwa katika eneo la Malabi,Waziri Lukuvi aliiagiza Manispaa ya Tabora kupima upya eneo hilo na kulipatia kanisa la African Inland Church (AIC) ekari kumi na ekari 28 zipimwe kwa ajili ya Wananchi ili kumaliza mgogoro huo na kmujongeza kuwa kila atayepata hati lazima ahakikishe kuwa analipa kodi ya pango la ardhi.
Awali,Katibu tawala wa mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua aliweleza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa kwa sasa Mkoa wa Tabora ndio wenyewe eneo kubwa na hivyo juhudi na nguvu kubwa inatakiwa ili kupima maeneo mengi kuepusha migogor ya ardhi. Tayari Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeidhinisha shilingi milioni 142 kusaidia manispaa ya Tabora kupima maeneo yake.

ASILIMIA 42% YA WATOTO WAMEDUMAA TANZANIA

$
0
0
download (1)
Na Gladness Mushi ,Arusha
Asilimia 42 ya watoto wamedumaa nchini Tanzania hali inayosababishwa
na kukosekana kwa lishe bora yenye virutubisho hivyo hivyo kusababisha
udumavu na kuathiri afya ya akili.
Profesa Joyce Kinabo wa Chuo Kikuu cha Sokoine kilichopo mkoani
Morogoro amesema kuwa kukosekana kwa lishe bora kumekua kukiathiri
maendeleo ya taaluma kwa watoto na kuzorotesha maendeleo ya jamii kwa
ujumla.
Joyce akizungumza katika mkutano wa wa masuala ya Lishe uliondaliwa na
taasisi ya kimataifa ya chakula na lishe (FANUS), uliofanyika jijini
Arusha amesema kuwa kati ya watoto 100 watoto 42 wanakabiliwa na
tatizo la udumavu hivyo ameitaka jamii na serikali kutilia mkazo suala
la lishe bora na virutubisho ili kuondokana na tatizo hilo.
“Serikali na watunga sera wanapaswa kutambua uhusiano ulioko kati ya
lishe bora na maendeleo ya taifa,elimu ya lishe na virutubisho itolewe
kuanzia ngazi ya familia,jamii hadi kitaifa na pia mashuleni somo la
lishe lirudishwe ili kuchochea ustawi bora wa jamii na taifa” Alisema
Joyce
Amesema kuwa jamii ya wafugaji hususani wamasai wanakabiliwa na tatizo
la udumavu ,ukondefu na upungufu wa damu mwilini kwa kukosa kutumia
mboga mboga na matunda na vyakula vingine  kwani jamii hiyo hupendelea
maziwa na nyama.
“Asilimia 16% wana kimo kisicholingana na umri wao yote haya
yanasababishwa na lishe duni kwa baadhi ya watu” Alisema Profesa
Profesa Tola Atinmo wa chuo kikuu cha Ibadan nchini Nigeria kitengo
cha Virutubisho vya binadamu amesema kuwa haki ya kupata lishe na
virutubisho ni haki ya msingi ya kila binadamu kama ilivyoainishwa
kwenye mkataba wa haki za binadamu wa kimataifa wa mwaka 1948.
Ameishauri serikali kuhakikisha kuwa inaboresha masuala ya lishe,afya
na usalama wa chakula kwa raia wake .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa mkutano huo
unatoa fursa kwa wataalamu wa masuala ya lishe nchini na viongozi
kujifunza masuala hayo muhimu katika maendeleo ya jamii.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA KUAPISHWA RAIS WA NIGERIA LEO

$
0
0
bi1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiteremka kwenye Ndege walipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na mtoto Ernest Nkayala alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea shada la maua kutoka kwa Mtoto Elin Mwandobo alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.

PINDA AHUTUBIA SHEREHE ZA MIAKA 25 WA TAWLA

$
0
0
ta5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi Mwanaidi Maajar baada ya kuhutubia katika sherehe za siku ya Wanasheria Wananwakde Tanzania Tawla , kwenye viwanja vya  Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ta4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) baada ya kuhutubia katika sherehe za miaka 25 ya chama hicho kwenye viwanja vya  Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015. Aliyekaa wapili kulia ni balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelaker.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ta2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza wakati alipozindua Uandishi wa Wosia katiak sherehe za miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wananwake (TAWLA) kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015.Kushoto ni balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelaker.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MBUNGE LUCY OWENYA AKABIDHI JEZI KWA TIMU ZILIZOFUZU ROBO FAINALI YA LUCY OWENYA CUP 2015

$
0
0

Dkt Fidelis Owenya akikabidhi jezi kwa vilabu nane vilivyo fuzu kucheza hatua ya robo fainali katika mashindano ya kombe la Mbunge lijulikanalo kama Lucy Owenya Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Moshi vijijini.
Jezi maalumu kwa ajili ya timu zilizo fuzu hatua ya robo fainali katika mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015.

Baadhi ya iongozi wa timu zilizofuzu hatua ya robo fainali wakifunga jezi zao mara baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya hatua ya robo fainali. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


MAFUNZO MAALUM YA SHERIA MPYA YA MANUNUZI YA UMMA YAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Dkt.Joseph .M.Kihanda mwenye suti nyeusi(waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo maalum kuhusu sheria mpya ya manunuzi ya umma yaani PPA 2011 na kanuni zake PPR.2013 ambao ni wadau wa kitengo cha manunuzi kinachosimamiwa na Bi.Juliana Musomi,Pius Seda,Salha Tego,Dickson Biya,Ezra Obilla,Kennedy Ndosi,Zubeda Mohamed,Alton Kumburu  na Stephen Mahinya),wajumbe wa bodi ya zabuni ya Taasisi hiyo ambao ni Bw.Zodo .M.Zodo,Bi.Linah Tumwidike,Bajjet Naresho,Anthony Mzurikwao,Said Mayunga,Lucina Comino na Burkad Haule pamoja  na wawezeshaji toka Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma (PPRA) ambao ni Bw.Gilbert Kamnde akishirikiana na ,Onesmo France,pia washiriki wengine walikuwa ni mkurugenzi wa biashara wa Taasisi hiyo Bw.Mzee Boma na  mameneja wote wa matawi ya Taasisi hiyo ambao ni  Ndugu John Boneka(Kigoma)Bw.Emmanuel Kingu (Singida),Luciana Hembe Mwanza)Bw.Mugisha Kamala (Mbeya na Bw.Matei Mapunda(Mtwara).
Wasiriki wakiwasikiliza wawezeshaji kabla ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki Tanzania T.E.C Kurasini jijini Dar es Salaama kwa siku tano kuanzia tarehe 25/5/2015 hadi tarehe 29/5/2015 ambapo washiriki watatunukiwa vyeti vya mahudhurio toka PPRA.
Mkuu wa kitengo cha Manunuzi wa Taasisi hiyo akiwa anaendelea kufuatilia kwa makini mafunzo hayo ambapo amekiri yatasiadia kuongeza ufanisi katika kitengo chake na Taasisi kwa ujumla hivyo kuomba Afisa mtendaji mkuu kuwawezesha mafunzo mbalimbali yanayohusu manunuzi ili Taasisi iendelee kufanya manunuzi kwa kuzingatia thamani ya pesa yaani '' Value for Money Procurement'' na kuiletea Taasisi Sifa nje na ndani ya Nchi kwani inatoa pia mafunzo katika ngazi ya cheti hadi Postgraduate kwa masomo hyo ya ugavi,ughasibu na mengine mengi katika nynja ya biashara.Hivyo ni wito pia kwa watanzania wote wanaohitaji kusomesha watotot wao katika chuo kinachotambuliwa na serikali kuwaleta watoto wao waje kusoma TIA...kwa maelezo zaidi na form za kujiunga chuo bonyeza hapa chini..




CCM WASHINDA NAFASI YA UENYEKITI MJI MDOGO WA HIMO.

$
0
0

Msimamizi wa Uchaguzi na mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akizungumza wakati wa
kutangaza matokeo katika uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa mji mdogo
wa Himo.


Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika
uchaguzi huo kutoka vyama mbalimbali vya siasa.
Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo Hussein
Jamal akizungumzamara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo
katika uchaguzi huo uliofanyika katika shule ya walemavu wa usikivu
eneo la njia Panda.
Baadhi ya viongozi waliofika kushuhudia
Uchaguzi huo.
Mkurugenzi wa wilaya ya Moshi,Fulgence
Mponji akitoa ufafanuzi katika uchaguzi huo.
Baadhi ya madiwani walioshiriki uchaguzi
huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya
Moshi,Moris Makoi akisalimia mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi
huo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga
akizungumza wakati wa kufunga kikao cha uchaguzi huo.
Dc Makunga akipeana mkono na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Moris Makoi mara baada ya kuzungumza
katika uchaguzi huo.
Na Dixon Busagaga wa Glob ya jamii

MH. LOWASSA KUANZA “SAFARI YA MATUMAINI” MCHANA WA LEO

$
0
0

Gari iliyombeba Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid, jijini Arusha mapema leo asubuhi wakati akielekea kwenye Ofisi za CCM Mkoa. Mh. Lowassa anatarajia kulihutubia taifa mchana wa leo kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid, ikiwa ni sehmu ya kutangaza kwake nia yake ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha.Kulia ni Mkewe Mama Regina Lowassa.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole (hayupo pichani).

MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UDIWANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA SONGEA MKOANI RUVUMA

$
0
0

Mwandishi wa Habari mwandamizi Bi. Celesencia Kapinga akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakata alipotangaza nia ya kugombea udiwani kata ya NDILIMALITEMBO Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa pamoja na Mwandishi wa Habari wa gazeti la Majira ambaye ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilimalitembo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) . Habari na picha na Demasho.com.
……………………………………………………..
WAKATI watu mbalimbali wameanza kujitokeza
kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia vyama vya siasa
mwandishi wa habari  Mwandamizi,  Mkoani
Cresensia Kapinga ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilima
litembo manispaa ya Songea  Ruvuma.
Mwandishi huyo ametangaza nia yeke ya
kuwania nafasi ya udiwani  mbele ya
waandishi wa habari  kwenye ofisi za
chama cha waandishi wa habari  Mkoa wa
Ruvuma  zilizopo mtaa soko kuu
mkoani  humo.
Amesema kuwa  kabla ya kutangaza nia amejipima na kujiona
anaweza kuongoza kata baada ya kuwa
aligombea nafasi hiyo kupitia viti masalumu mwaka 2010 ambapo kura
hazikutosha.
Akijibu masawali mbalimbali ya Waandishi wa
habari amesema kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo baaada ya kuona Changamoto
mbalimbali zinazowakabaili Wananchi Katika Kata hiyo iliyokonje kidogo ya
Manispaa  ya songea hazijafanyiwa kazi. 
‘Ziko Changamoto nyingi zinazowakabili
Wananchi  wa Kata ya Ndilimalitembo bado
hazijafanyiwa kazi,baadhi zikiwa ni Ukosefu wa Zahanati,Shule kukosa Vyoo na
Wananchi kukosa soko la uhakika la kuuza mazao yao ambazo naamini  nikipata
nafasi ya kuwa Mwakilishi wao nitazishughulikia’anasema Bi. Cresensia
Kapinga.
Anasema kuwa kuwa kutokana na  na taaluma yake ya uandishi wa habari ana
uwezo wa kuingia Ofisi yoyote katika Manispaa ya Songea  na kuwasemea Wananchi wa  Kata hiyo hivyo anasema ni fursa  pekee ya Wananchi hao kumpa Fursa ya kuongoza
Kata hiyo.
Kwa upande wa Waandishi wa habari amesema
kuwa  kwa kuwa yeye ni Mwanahabari
atajitahidi kuwasema kwenye Baraza la
Madiwani  akiamini yapo mambo
mengi yanashindwa kushughulikiwa ikiwemo posho zao.
Kwa upande wao Waandishi wa Habari
wamepongeza hatua hiyo  na kutaka
Waandishi wengine wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa
Waandishi wamekuwa  wakinadi watu wengine
wakati wapo baadhi yao wana uwezo wa kuongoza.
Mmmoja wa Waandishi hao Julius Konala
anasema hatua hiyo ni ya kupongeza sana kwa kuwa imefunguia njia kwa Wanahabari
wengine kugombea zaidi  na kuwata
Wananchi  na Wanaccm kumuunga mkono  katika
azma yake ya kutaka kuwa  Diwani
wa Kata ya Ndilimalitembo.

UJUMBE WA MAOFISA WA UMOJA WA BENKI ZA AKIBA DUNIANI KANDA YA AFRIKA WAKITEMBELEA ZANZIBAR

$
0
0

Meneja wa Tawi la Benki ya Posta Zanzibar Ndg Justin S.Nandonde akisalimiana na kumkaribisha wageni wake walipotembelea Tawi hilo Zanzibar kujionea utendaji wa Benki ya Posta Tawi la Zanzibar wakiwa katika ziara yao Zenj.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg. Sabasaba Moshingi, akitoa maelezo ya
Ujumbe wa Maofisa wa Benki wa Umija wa Mabenki Duniani Kanda ya Afrika,
walipotembelea Benki ya Posta tawi la Zanzibar.
Wajumbe wa Mkutano wa Wanachama wa Umoja wa Mabenki Duniani na Kanda ya Afrika wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania wakati walipofika Tawi la Benki ya Posta Zanzibar,
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg. Sabasaba Moshingi, akitowa maelezo ya
Ujumbe wa Maofisa wa Benki wa Umija wa Mabenki Duniani Kanda ya Afrika,
walipotembelea Benki ya Posta tawi la Zanzibar
Mkurugenzi wa Tekohama na Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Jema Msuya akitowa maelezo ya kiufundi kwa ujumbe huo.walipotembelea Benki ya Posta Tawi la Zanzibar Mchangani  
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Zanzibar Ndg. Justin SNdandonde akitowa maelezo kwa ujumbe huo ulipotembelea Tawi hilo na kuagalia ufanisi wa huduma za Benki hiyo kwa wateja wao
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi akiwa na wakeni wake wakitoka katika moja ya sehemu ya historia ya Kanisa la Mkunazi Zanzibar.  
Mtembeza Watalii katika Mji Mkongwe seif Ali akitowa maelezo kwa Ujumbe huwa sehemu za historia za Mji Mkongwe wa Zanzibar. 
Maofisa wa Umoja wa Benki za Akiba Duniani Kanda ya Afrika wakiwa katika ziara yao katika mji mkongwe na kupata kuonja Ubuyu wa Kwaissa sokomuhugo Zenj wakiwa katika ziara ya siku mbili Zanzibar baada ya kumaliza Mkutano wao Dar.
Mtembeza Watalii Zenj akitowa maelezo kwa Ujumbe huo wa Maofisa wa Mabenki ya Akiba wakiwa katika ziara yao kutembelea sehemu za historia za mji Mkongwe Zanzibar wakipata maelezo ya Mlango wa Zanzibar

EDWARD LOWASSA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA TANZANIA, JIJINI ARUSHA

$
0
0

 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SOURCE:http://issamichuzi.blogspot.com/
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana.
 Mh. Lowassa akiwapungia wananchi.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo,  kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya jana.
Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa wakati wa mkutano uliofanyika jioni ya Jana. kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Mh. Edward Lowassa akipongezwa na baadhi ya Wabunge waliohudhulia mkutano huo, baada hotuba yake.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MAALIM SEIF IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad ikulu jijini Dar es Salaam
(picha na Freddy Maro)
1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad ikulu jijini Dar es Salaam.
Viewing all 6824 articles
Browse latest View live