Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all 6902 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC

$
0
0
li1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muuangano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Kiondo, wakati alipofika na ujumbe wake Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
li2
li3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Kombe kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani kutoka Kituo cha kuelelea watoto waishio katika mazingira magumu kilichopo Kigamboni, kinachosimamiwa na TBC. Mshana alifika na ujumbe wake Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar esSalaam, leo kwa ajili ya mazungumzo na kumkabidhi zawadi hizo. Picha na OMR
li4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Saa ya ukutani kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
li5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Khanga zenye Nembo ya TBC na zinazotangaza Utalii wa ndani  kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
li6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Tisheti  kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 2, 2015. Picha na OMR
li7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Mshana, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbi na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha kulelea Watoto waishio katika mazingira magumu, kilichopo Kigamboni baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
li8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib BIlal, akiagana na wajumbe walioongozana na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, Clement Kiondo, Omar Rajab (kushoto) na Maico Rugendo, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR

MKE WA WAZIRI MKUU AZINDUA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION

$
0
0

Mgeni Rasmi kwenye halfa ua Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Vipodozi Pendwa Vijulikanavyo kama Luv Touch Manjano Mke wa Waziri Mkuu Mh Tunu Pinda Akitoa Hotuba yake katika Uzinduzi huo .Katika Hotuba yake Mh Mama Pinda Alisema amefurahishwa sana Kwa Mwanamke wa Kitanzania Kuanzisha Bidhaa amabyo imeweza kushindana na Bidhaa kama hizo kutoka mataifa Mengine.Halfa hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifunguliwa na mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania mama Tunu Pinda. 

Alizindua rasmi kwa soko la Tanzania poda ya luvtouch Manjano, rangi ya awali (foundation), na rangi ya mdomo (lipstick) na walio hudhuria hafla hiyo walipata nafashi ya kushuhudia thamani ya bidhaa hizo, aina ya urembo na viwango vya ubora vinvyoshinda hoja zote na kuthibitisha kuwa bidhaa za hapa nchini zinaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Wanawake wengi walipata fursa ya kujaribu moja ya bidhaa hizo na waliweza kununua bidhaa za LuvTouch Manjano ukumbini.

Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar Akisisitiza Jambo kwenye Halfa Hiyo.Mh Balozi Majaar Alisisitiza Umuhimu wa Kumsomesha Mtoto wa Kike Pamoja na Kuwawezesha Kiuchumi.Balozi Majari alisiistiza Jamii ya Kitanzania Kuachana na Kasumba ya Kuwanyanyapaa Watoto wa Kila pia Kutokuwawezesha na Akasema mtoto wa Kike akipewa Fursa ya Kupata Elimu na Kuwezeshwa Wanawake Wanaweza .


Hafla hiyo pia ilihusisha kuzindua Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Shirika hili limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu.

 Shear illusions ilikusanya wanawake takriban 450 wa Kitanzania kusherehekea miaka 10 ya safari ya kumfurahisha kila mwanamke, pamoja na kuzindua kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano iliyobuniwa na Shekha Nasser, mmiliki wa Shear illusions. Pamoja na uzinduzi huo, alizundua pia kitabu cha muongoza kwa kina mama kuonyesha jinsi ya kujipodoa kitaalam kwa kutumia nyenzo na vipodozi sahihi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Katikati akiongea Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda (Kulia) Pamoja na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul Wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Uzinduzi wa Vipodozi Pendwa vya Luv Touch. 
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul (Kulia) Akiwa n Mtoa Mada katika Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda
Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi akitoa Burudani ya aina yake kwenye Halfa hiyo iliambatana na Uzinduzi wa Vipodozi vya Luv Touch 
Wageni waalikwa walioshiriki katika halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation
Mshereheshaji wa Halfa Hiyo Ndugu Angela Bongo akiwa na Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Pili Kushoto akiwa Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda wa Pili Kulia Pamoja na Watoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar na Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda.
Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda Katikati Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser wa Kushoto na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda. 
wageni walikwa


TAASISI YA UTT-PID CHINI YA WIZARA YA FEDHA YAPANUA BARABARA ENEO LA MRADI WA VIWANJA LINDI

$
0
0

 Muonekano wa viwanja vya Mabano vilivyopimwa na Taasisi ya UTT-PID kwa ushirikiano na Halmashauri vilivyopo Manispaa ya Lindi.
Baada ya kupima na kufanikiwa kuuza viwanja zaidi ya 2,500 katika fukwe za Mabano na Mmongo kwa ushirikiano na Manispaa ya Lindi, Mradi huo umeingia katika hatua ya upanuzi wa barabara kuu na za mitaa ndani ya mradi ambapo kwa ushirikiano huo zaidi ya Shilingi Billion 1 zinatarajiwa kutumika mpaka kukamilika kwake.
Mradi huo mkubwa zaidi nchini katika upimaji wa viwanja Manispaa ya Lindi ulifadhiliwa na Taasisi ya UTT-PID utekelezaji wake ulianza mapema mwaka 2013 na sasa uaandaji wa hati kwa wanunuzi upo katika hatua ya mwisho baada ya kila mteja wa kiwanja kufanikiwa kuweka saini kwa hati zao katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi kwenyewe.
 Uchongaji wa hatua za awali wa Barabara ukiendelea katika eneo la Mradi. Ujenzi wa barabara hizi unatarajia kukamilika kabla ya wanunuzi kuuanza ujenzi wa makazi yao katika eneo la mradi.
Uwekezaji huo ukiendelea pia Taasisi hiyo kwa ushirikiano huo na Halmashauri ya Lindi inatarajia kuingia katika awamu ya pili ya Mradi wa upimaji viwanja katika fukwe hizo ambapo zaidi ya viwanja elfu tano vitapimwa na kuuza kwa wananchi wote. Utekelezaji wa awamu ya pili bado upo kwenye hatua za awali na unatarajia kuuanza ndani ya mwaka huu 2015.
 Viwanja vya Mabano na Mmongo vipo katika fukwe nzuri na vikipata upepo mwanana kutoka bahari ya Hindi.
Toka kuanzishwa kwake Taasisi ya UTT-PID imejikita sana katika upimaji wa maeneno katika mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na Halmashauri tofauti nchini. Miradi mikubwa kama ya Bukoba ambapo viwanja zaidi ya 5,000 vilipima kuuzwa, Halmashauri ya Sengerema kwa ushirikiano na Taasisi ilipima zaidi ya viwanja 1,200 na uuzaji pamoja na uwekezaji katika Miundombinu husika unaendelea kwa kasi. Pia Taasisi imewekeza katika miradi binafsi kama vile eneo la Mapinga katika wilaya ya Bagamoyo huku ikatarajia uwekezaji mkubwa zaidi katika mikoa ya Morogoro , Arusha, Dar es Salaam, Maswa, Pwani, Maswa na Ruvuma.
 Upanuzi huu wa barabara utafanyika mpaka kwenye fukwe kuwapa nafasi wakazi wa eneo husika kutembelea maeneo ya fukwe hizo
Zaidi ya viwanja 2,500 vilipimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile Makazi, Biashara, Maeneo ya Umma na sehemu za kupumzika. (Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog).

MBUNGE WA UKONGA EUGEN MWAIPOSA AFARIKI DUNIA

$
0
0


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA
 

TANZIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Mhe. EUGEN ELISHIRINGA  MWAIPOSA  kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 June 2015 nyumbani kwake Dodoma ambako amekuwepo kushiriki Mkutano wa Bunge la Bajeti.

Mwili wa Marehemu utaagwa kesho tarehe 3 Juni 2015 kuanzia saa 4 asubuhi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, na baadaye mwili kupelekwa nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam.
BWANA alitoa, BWANA ametwaa. Jina la BWANA  lihimidiwe. Amina!

Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Dodoma,

2 Juni 2015. 

BUNGE LAAHIRISHWA KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA UKONGA EUGEN MWAIPOSA

$
0
0
7
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga marehemu Bi. Eugen Mwaiposa ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Taarifa za kifo chake zimetangazwa wakati bunge likiendelea na mjadala wa bajeti ya wizara ya afya hivyo kupelekea bunge hilo kuahirishwa hadi tarehe 4 mwezi huu.
1
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt Seif Rashid akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2015/2016 leo mjini Dodoma.
2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Jenista Mhagama (mwenye nguo nyekundu) akimfariji Mwenyekiti wa Bunge Bi. Lediana Mng’ong’o mara baada ya bunge kuahirishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Bi. Mary Nagu na kushoto ni wabunge James Mbatia na Goodluck Ole Medeye.
3
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjela Kairuki (kushoto) akitoka nje ya ukumbi wa bunge akiwa ameambatana na wabunge Bi. Mary Mwanjelwa na Rita Kabati baada ya bunge hilo kuahirishwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa.
45
Baadhi ya wabunge wakiwa kwenye hali ya simanzi baada ya kutangazwa kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa kilichotokea usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma.
6

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO NA WAFANYABIASHARA

$
0
0
1
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwaeleza wafanya biashara kuendelea kutoa ushirikiano, utakaojenga uhusiano wa kudumu kati yao na Serikali kwa maslahi na maendeleo ya Taifa, wakati akitoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam.
2
2- Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade akimshukuru Waziri wa Fedha kwa ushirikiano wanaoendelea kuuonyesha kwa mamlaka hiyo hasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala la ukusanyaji Kodi nchini.
3
3- Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja akimueleza Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum kuridhishwa na utendaji wa serikali katika utatuzi wa changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kufikia malengo ya taifa ya kuwa na uchumi imara kupitia ukusanyaji wa Kodi.
4
4- Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchomvu akipongeza kazi iliyofanywa Kamati ya uhamasishaji wa matumizi ya mashine za kielektroniki(EFDs) na kuwaasa kuendelea kutoa ushirikiano kwa maslahi ya Taifa kwa Ujumla.
5
 Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja wafanyabiashara alipotoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki (EFDs) leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara Bw. Johnson Minja na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu.
…………………………………………………………..
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Serikali yafikia muafaka katika mgogoro wake na wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine za kieletroniniki EFD’s.
Hayo ameyasema jana Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari juu ya Serikali kufikia muafaka wa makubaliano yaliyofanyika kwa ushirikiano wa Kamati kuu ya Taifa iliyoshirikisha wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara katika ngazi ya Taifa.
“Matumizi ya mashine za EFD yalipoanza yalileta changamoto kwa wafanyabiashara ,hivyo niliunda kamati ya kitaifa pamoja na kamati katika ngazi za Mikoa na Wilaya pamoja na wenyeviti wakuu wa mikoa kutafuta suluhu la suala hili”alisema Mhe.Mkuya.
Waziri Mkuya aliendelea kusema Kamati imetoa mapendekezo mbalimbali kwa Serikali ikiwemo ya muda mfupi ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi na mengine ni yakisera ambayo yatahitaji muda mrefu yatafuata utaratibu unaopaswa katika utekelezaji wake,kwa ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu,kupitia kamati ya Kitaifa itakayodumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw.Johnson Minja aliipongeza serikali kwa kubali kukaa meza moja na wafanyabiashara katika kutatua mgogoro huo uliyokuwepo katika matumizi ya mashine za EFD na kuakukubali kupokea changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuzifanyia kazi.
“Serikali imekubali kupitia mfumo wa utozwaji kodi kuanzia ngazi ya bandarini na kuongeza uwazi ilikuleta uelewa kwa wafanyabiashara na kuepuka kutozwa kodi kubwa kutoka na kukosa uelewa wa gharama za ulipaji kodi”,alisema Bw.Minja.
Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara aliendelea kusema ni wajibu wa kila mmoja kulipa kodi na hii ni kwa maendeleo ya nchi na pia ni kosa kwa mfanyabiashara yoyote kuendesha biashara yake bila kuwa na namba ya utambulisho wa mlipakodi (Tin Number),tunataka namba ya walipakodi iendelee kuongezeka na kuondoa kabisa wafanyabiashara wasio lipa kodi.
Mbali na hayo nae Kamishana Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Rished Bade aliipongeza kamati kwa kuweza kufika mwafaka na kuweza kuzitambua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwasumbua wafanyabiashara na ameahidi ,kuwa ofisi yake itaendelea kuwawajibisha watu wote wanao kiuka taratibu za ulipaji kodi.

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AFUNGUA MKUTANO WA TANO WA WADAU WA NSSF MKOANI ARUSHA

$
0
0
5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akifungua mkutano wa tano wa wadau wa Mfuko wa Hifadhi za Jamii wa  NSSF kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Juni 2, 2015. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Tibenda, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ,Dr. Ramadhani Dau na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Abubakari Rajab.
(Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)
4
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tano wa Mfuko wa hifadhi ya jamii, NSSF wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipofungua mkutano huo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha  Arusha,  AICC mjini Arusha Juni 2, 2015.
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mdau wa Mfuko wa Hifadhi za Jamii wa NSSF, Bw.Clement Lori na mkewe Margareth  baada ya kufungua mkutano wa wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha AICC mjini Arusha Juni 2, 2015.

BLATTER AJIUZULU URAIS FIFA

$
0
0

Rais wa FIFA, Sepp Blatter ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.
Sepp Blatter akiwapongeza wajumbe wa FIFA baada ya kushinda nafasi hiyo siku sita zilizopita.
Maafisa wakuu wa FIFA waliokamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi.
MTIKISIKO, Rais wa FIFA Sepp Blatter (79) ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Urais wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kufuatia kashfa ya rushwa.
Taarifa iliyotolewa leo makao makuu ya FIFA mjini Zurich, Uswisi, Blatter amesema anaondoka baada ya miaka 17 kama mtu mwenye nguvu katika soka. 
Blatter ataendelea kubaki madarakani hadi hapo Fifa itakapofanya uchaguzi mkuu mpya wa viongozi na unatarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Blatter alichaguliwa tena wiki iliopita baada ya kumshinda Prince Ali licha ya maafisa wake saba wakuu kukamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi.
Blatter alijiunga na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) mwaka 1975 kama mkurugenzi wa kiufundi, akawa katibu mkuu (No.2) mwaka 1981, na baadaye kutawazwa kuwa urais.

KUCHUKUA FOMU ZA URAIS CCM NI LEO MJINI DODOMA, SEIF KHATIBU NDIYE KAPEWA JUKUMU LA KUKABIDHI FOMU

$
0
0

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM IDARA YA OGANEZESHENI DR MOHAMED SEIF KHATIBU AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MAKAO MAKUU DODOMA KUHUSHU RATIBA YA KUCHUKUA FOMU LEO  WAGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA HICHO ALIWATAJA KUWA ATAANZA PROF MARK  MWANDOSYA ,STEPHEN WASIRA,EDWARD LOWASSA, BALOZI AMINA SALUMU ALI NA CHARLES MAKONGORO NYERERE  NA KHATIBU NDIYE ALIYEPEWA JUKUMU NA CHAMA HICHO KUTOA FOMU HIZO.

WANASIASA WATANO  WANATARAJIA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS  KATIKA MAKAO MAKUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) DODOMA.

KWA MUJIBU WA KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM (NEC) WA OGANAIZESHENI, DK MUHAMMED SEIF KHATIB, UCHUKUAJI WA FOMU HIZO UNAANZA RASMI LEO.

AMESEMA KWA MUJIBU WA ORODHA WALIYONAYO, WANACHAMA WATANO WATACHUKUA FOMU HIZO KUANZIA SAA NNE ASUBUHI HADI SAA 10:30 JIONI, NA KILA MMOJA AMEPEWA SAA MOJA NA WAMETENGA MUDA WA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWA WAGOMBEA AMBAO WATAONA INAFAA KWAO. AMEMTAJA WA KWANZA KUCHUKUA FOMU KUWA NI WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (KAZI MAALUMU), PROFESA MARK MWANDOSYA KUANZIA SAA 4 KAMILI HADI SAA 5:30.

PROFESA MWANDOSYA ATAFUATIWA NA WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA STEPHEN WASSIRA KUANZIA SAA 5:30 NA ATAFUATA WAZIRI MKUU WA ZAMANI, EDWARD LOWASSA ATACHUKUA FOMU KUANZIA SAA SABA KAMILI. WA NNE ATAKUWA WAZIRI WA ZAMANI WA MUUNGANO, BALOZI AMINA SALUM ALI KUANZIA SAA 8:30 MCHANA NA PAZIA LA UFUNGUZI LITAFUNGWA SAA 9:30 ALASIRI NA MTOTO WA BABA WA TAIFA, MWALIMU NYERERE, CHARLES MAKONGORO NYERERE.

BAADA YA KUMALIZA KUCHUKUA FOMU  KWA KUNDI LA KWANZA WANASIASA  WENGINE AMBAO WAMETANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS NI LAZARO NYALANDU, FREDERICK SUMAYE, PROFESA SOSPETER MUHONGO, JANUARY MAKAMBA, MWIGULU NCHEMBA NA LUHAGA MPINA.WANAOTAJWA NI PAMOJA BERNARD MEMBE, WILLIAM NGELEJA, DK TITUS KAMANI, LUHAGA MPINA, MIZENGO PINDA, DK ASHA-ROSE MIGIRO, SHAMSI VUAI NAHODHA, DK EMMANUEL NCHIMBI NA DK HAMIS KIGWANGALLA.

KATIBU HUYO WA OGANAIZESHENI AMESEMA UCHUKUAJI HUO WA FOMU UTAZINGATIA TARATIBU ZILIZOWEKWA NA CCM NA KUTAKUWA NA FOMU TATU ZITAKAZOPEWA WAGOMBEA.FOMU  YA KWANZA  ITAHUSU MAELEZO BINAFSI YA MGOMBEA, ITAHUSU UZOEFU NA UJUZI WAKE, NYINGINE ITAKUWA YA KUJAZA ORODHA YA WADHAMINI WAKE NA NYINGINE YA MASHARTI KAMA YALIVYOKUBALIWA NA HALMASHAURI KUU YA TAIFA.

KWA UPANDE WA WADHAMINI  AMESEMA, MGOMBEA ATATAKIWA KUPATA WADHAMINI 450 KUTOKA KATIKA MIKOA 15 YA TANZANIA BARA NA MIKOA MINGINE MITATU YA TANZANIA ZANZIBAR. WAGOMBEA HAO WATAKAPOFIKA KUCHUKUA FOMU, WANAPASWA KUWA NA ADA YA SH MILIONI MOJA NA WATASAINI DAFTARI MAALUMU KUONESHA NDIO WALIOCHUKUA FOMU.

AMEWATAKA  WAGOMBEA WENGINE WANAOTAKA KUCHUKUA FOMU HIZO KUWASILIANA MAPEMA NA OFISI YAO KWANI ALISEMA WANGEPENDA KAZI YA UCHUKUAJI FOMU KUDUMU KWA SIKU ZISIZOZIDI TANO ILI SHUGHULI NYINGINE ZIENDELEE

HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA(TANAPA) KUPITIA UJIRANI MWEMA WAKABIDHI MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA ASHIRA WILAYA YA MOSHI

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro,Leonidas Gama
akikaribishwa na Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro
(KINAPA)Erastus Rufungulo katika makabidhiano ya mradi wa maji wa
ujirani Mwema uliotolewa na hifadhi za taifa nchni
TANAPA.


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika tanki la maji la mradi wa ujirani mwema uliotolewa na TANAPA kwa wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama
akisoma kilichoandikwa katika vibao mara baada ya uzinduzi wa mradi
huo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama
kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi huo.
RC ,Gama akinywa maji kwa kutumia mkono mara
baada ya kufungua bomba la maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya
Moshi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,akimtwisha ndoo
ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ashira katika wilaya ya Moshi
ikiwa ni ishara ya kukabidhi mradi huo wa maji ulifadhiliwa na TANAPA
kupitia mradi wa ujirani mwema.
Tanki la Maji la mradi wa ujirani mwema
uliofadhiliwa na Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA).
Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro (KINAPA) Erastus Rufungulo akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi wakati wa kukabidhi mradi wa maji wa ujirani mwema uliofadhiliwa na TANAPA.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Ashira
wilaya ya Moshi vijijini.
Meneja Ujirani mwema wa Hifadhi za Taifa
,Tanzania(TANAPA) Ahmed Mbugi akizungumza kuhusu miradi ya ujirani mwema ambayo TANAPA imekuwa ikiitoa kwa jamii katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ashira
katika wilaya ya Moshi .
Kaimu Mkurugenzi mkuu TANAPA,Ibrahim Musa
akitoa taarifa mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
kuhusu ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya
Moshi ,
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga
akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji uliofadhiliwa na
TANAPA kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Ashira wilaya ya
Moshi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
akiwahutubia wananchi waliofika katika makabidhiano ya mradi wa maji
katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi ,uliofadhiliwa na hifadhi za
taifa Tanzania (TANAPA) .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya
Jamii,Kanda ya Kaskazini, 

MAANDALIZI YA HAFLA YA MH SAMUEL SITTA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS YAIVA!

$
0
0

Adama Fundikira akiwa na mama yake mdogo Mh Samuel Sitta aitwaye Ndisha Said Fundikira
Wayege wakicheza ngoma
Habari na picha kwa hisani ya 
Mkala Fundikira wa TBN central zone

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA MAJI KIJIJI CHA MAGOZA, MKURANGA

$
0
0

 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akikata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa gharama ya sh. mil 56, katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda, Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Karu Karavina na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (wa pili kulia).
 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto kwake) pamoja na Diwani wa Kata ya Kiparang’anda, Karu Karavina (kushoto) wakifurahi baada kukabidhi mradi wa  kisima cha maji kwa wananchi wa Kijiji cha Magoza, wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL gharama ya sh. mil. 56.
 Akina mama wakicheza kwa furaha wakati wa hafla ya kukabidhiwa kisima chas maji na TBL
 Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akitoa utambulisho wakati wa hafla hiyo
 Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akimtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda, wilayani Mkuranga, Pwani, wakati wa hafla ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kilichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 56 kijijini hapo. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
 Mmoja wa akina mama akifurahia baada ya kuteka maji kwenye kisima hicho
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akielezea mikakati ya kuisaidia jamii katika uboreshaji wa sekta ya maji nchini kutoka  sehemu na faida inayopatikana katika mauzo ya vinywaji vyao
Diwani wa Kata ya Kiparang’anda, akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada huo wa kisima.
 Wakifunua pazia kuzindua mradi huo wa kisima
 Mgeni rasmi, Benjamin Majoya akifungua maji ya bomba badaa ya kuzindua kisima hicho
 Steve Kilindo wa TBL, akinywa maji baada ya kuzindua kisima hicho
Akina mama wakazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda,Mkuranga, wakiwa wamebeba ndoo za maji waliyoteka katika Kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kijiji hicho kwa gharama ya sh. mil. 56. Hafla ya TBL kukabidhi kisima hicho cha maji ilifanyika mwishoni mwa wiki.

SAMUEL SITTA ATANGAZA RASMI NIA YAKE KUGOMBEA URAIS

$
0
0

Mh Samuel Sitta akitangaza nia jana mchana Itetemia Tabora

Mheshimiwa Samuel Sitta leo hii alitangaza rasmi nia yake kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alitangaza nia yake hiyo mbele ya mamia ya wakazi wa kata ya Itetemia, Tabora mjini na wilaya za jirani na mji wa Tabora.
Mambango nayo yalikuwepo!
Mh Sitta akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Tabora jana mchana.
Mh Magreth Sitta akisalimia wananchi wa Itetemia
1.Muungano
Toka pande zetu mbili za muungano zinatolewa kauli na pia vitendo vyenye kuashiria nchi zetu zilizomo katika muungano yaani Tanganyika na Zanzibar zitengane. Kutoka Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai kuwa Zanzibar itanufaika zaidi ikiwa nje ya muungano na kuwa na uhuru kamili kama nchi. Na kutoka bara tunasikia.
2. Mchakato wa katiba
Pamoja na kuwa na muafaka kamili kuhusu katiba mpya haujapatikana, lakini katiba inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi ambayo yanaweza kutuleta karibu ikiwa ni hatua ya awali inayotuwezesha kusonga mbele kwa amani.
Mama Magreth Sitta akiwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tabora Mama Mchemba.
Mtemi wa Unyanyembe Mtemi Msagata Fundikira, Mh Samuel Sitta na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini
Binafsi naamini kuwa pande zinazosigana kuhusu katiba zina wazalendo ambao wanaweza kukubaliana kuwa na kipindi cha mpito cha utulivu na maelewano kitakachotuwezesha kama taifa kusonga mbele. Viongozi a kijamii na ki saisa washawishiwe kukubali hoja mbili.

3.Mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda
Ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umasiikini kwa haraka na huku tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya aserikali kutosheleza  huduma za ubora wa huduma za jamii kama vile afya , elimu na maji,hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshaji uwe ni wa motisha kwa wazalisha mali. Mifumo ya nchi zilizopiga hatua za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira  chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii haijatimia hapa kwetu.
4.Mikakati ya dhati ya kupambana na rushwa
Rushwa kubwa zimekuwa na athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi yetu. Mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hata rushwa katika ajira, vimesababisha hasara ya matrilioni ya shilingi kwa taifa. Uchumi unakosa afya kutokana na kubanwa na rushwa ambayo sasa imeenea mpaka vijijini.

5. Kuimarisha CCM kiuchumi
Chama tawala madhubuti ni nyenzo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zote kwa ufanisi zilizoahidiwa kwenye ilani. Katika hili ni wajibu wa mwenyekiti wa chama kuhakikisha kwamba vitengo na vitega uchumi vya chama vinakuwa na tija inayokiwezesha chama kuendesha shughuli zake  kwa kujitegemea badala ya kutegemea ruzuku toka serikalini. Chama tawala kinachojitegemea ki uchumi ni kinga dhidi ya rushwa kwa sababu itazuia mazoea yaliyopo ya wafanyabiashara wasio waaminifu kujijenga kwa mwanya wa kuwa ni “wafadhili” 
Mh Magreth Sitta akifuatiwa na Mussa Ntimizi mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui
Magreth Sitta Kijo akiwa na mumewe Kefa Kijoh Itetemia jana

MWILI WA MHE. EUGEN MWAIPOSA ALIYEKUWA MBUNGE WA UKONGA WAAGWA BUNGENI

$
0
0
1
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue (kulia) akisalimiana na Waziri wa Fedha wa zamani na Mbunge wa Kilosa Mhe. Mustafa Mkulo alipowasili kwenye viwanja vya bunge jana.
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu (kulia) akizungumza jambo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai jana mjini Dodoma kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga jijini Dar es Salaam.
3
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni waliofika kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika jana katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
4
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Mhe. Anna Abdallah akimfariji mume wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa mbunge wa Ukonga aliyefariki usiku wa kuamkia Juni 2 nyumbani kwake mjini Dodoma.
5
Waheshimiwa Wabunge na baadhi ya watu mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya bunge jana mjini Dodoma kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga.
6
Mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga ukiwasili kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa.
11
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akitoa salam za bunge kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
14
Mchungaji Mshana Samweli wa KKKT Jimbo la Dodoma akitoa neno kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa mjini Dodoma.
7
Baadhi ya Wabunge wakiwa kwenye hali ya majonzi mara baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
8
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bibi Chiku Galawa wakiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa
9
Wabunge Mhe. Anna Abdalla (kushoto) na Mhe. Ester Bulaya wakiaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
10
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu kwenye viwanja vya bunge jana mjini Dodoma wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa.
12
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Martha Mlata akiimba kwa hisia wimbo wa maombolezo kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika jana katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
13
Baadhi ya wabunge wakitoa pole kwa wanafamilia wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge jana mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA FATMA SALUM – MAELEZO

KATIBU MKUU WA CCM TAIFA ABDULRAHMAN KINANA AANZA ZIARA

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenye basi kuwasalimia wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa wa Morogoro akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa mkoa wa Morogoro waliojitokeza kuwasalimu wakati wa safari ya kuelekea Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi waliojitokeza kwenye kituo cha mabasi mjini Morogoro maarufu kama Msamvu ambapo aliwaambia wananchi hao huu ni wakati wa kuchagua kiongozi wa kutuongoza hivyo ni vyema wananchi kupima na kuacha ushabiki.

WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA VIWANDA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WANAOKUSANYA TAARIFA ZA SENSA YA VIWANDA NCHINI

$
0
0
1
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mkoani Dodoma kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika nchini. Kushoto kwake ni Idd Mruke, Meneja Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mkoa wa Dodoma.
2
Meneja wa Takwimu za Biashara na Utalii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, ambaye ni Msimamizi wa Sensa ya Viwanda nchini akiwaelezea waandishi wa habari leo mkoani Dodoma kuhusu vigezo vilivyotumika katika kuchagua sampuli ya viwanda vilivyochaguliwa kufanyiwa utafiti. Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda.
3
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda wakati akizungumza nao leo mkoani Dodoma kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika nchini.
…………………………………………………
Na Veronica Kazimoto, Dodoma
Wito umetolewa kwa wamiliki wote wa viwanda kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wasimamizi na wadadisi wanaokusanya taarifa za Sensa ya Viwanda inayoendelea hapa nchini.
Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dododoma ambapo amesema ukusanyaji taarifa kwa nchi nzima umefikia wastani wa asilimia 80.5.
“Hadi kufikia tarehe 24 Mei, 2015 jumla ya viwanda vidogo 9,540 sawa na asilimia 82 pamoja na viwanda vya kati na vikubwa 1,158 sawa na asilimia 79 vilikamilika kukusanywa taarifa zake. Hii inafanya ukusanyaji Takwimu kwa nchi nzima kuwa wastani wa asilimia 80.5″, amesema Dkt. Kigoda.
Aidha, Waziri Kigoda amesema licha ya mafaniko hayo, bado kuna kazi kubwa ya kukamilisha viwanda vilivyobaki ambavyo ni takriban 2,032 sawa na wastani wa asilimia 19.5.
“Hivyo, nawaasa wamiliki wote wa viwanda hususani katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Morogoro, Tabora, Kigoma na Manyara kutoa ushirikiano zaidi na wa kutosha kwa zoezi hili ili ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Juni, 2015, tuweze kuhitimisha”, amesisitiza Dkt. Kigoda.
Waziri Abdallah Kigoda amesema lengo kuu la Sensa ya Viwanda ni kukusanya takwimu sahihi zinazohusu Sekta ya Viwanda nchini ambazo zitawezesha kupata viashiria sahihi vya uchumi pamoja na taarifa muhimu za viwanda kama vile orodha ya viwanda kimkoa, anuani na mahali vilipo, aina ya umiliki na utaifa wa wamiliki.
Taarifa nyingine ni pamoja na mwaka ambao viwanda hivyo vimeanza uzalishaji, shughuli kuu ya viwanda husika, idadi ya wafanyakazi, gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mapato yanayotokana na uzalishaji na gharama za uzalishaji.
Lengo lingine la Sensa ya Viwanda ni kupima na kufuatilia mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Viwanda ili kuiwezesha Serikali kuboresha sera na programu za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya Tanzania, 2025, Malengo ya MKUKUTA na Mpango wa Taifa wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN).
Jumla ya Wadadisi 198 wameajiriwa kwa ajili ya kufanya kazi ya kukusanya Takwimu na taarifa viwandani ambapo wanasimamiwa na Mameja Takwimu wa Mikoa, Watakwimu kutoka Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Maafisa kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA MAREHEMU KAMISHNA MKUU MSTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA, ONEL MALISA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye ameagwa leo Kijeshi Juni 04, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga Jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwa mazishi kwao Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
2
Mwili wa Marehemu, Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ukiwa umebebwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza tayari kwa zoezi la kuagwa Kijeshi katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
3
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiwa amesimama wakati mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ulipokuwa ukiwasili katika Viwanja vya Chuo Cha Maafisa Magereza Ukonga(katikati) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kulia) ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu.
4
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisaini katika Kitabu cha Maombolezo kabla ya kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu wa Magereza Mstaafu Onel Malisa.
5
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini salaam mbalimbali za rambirambi zilizokuwa zikitolewa katika hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu, Onel Malisa.
6
Kiongozi Mwakilishi wa Wastaafu wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, John Nyoka akitoa salaam za rambirambi.
7
Gadi Maalum ya Maafisa wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya paredi la kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa.
8
Umati wa ndugu na Jamaa waliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa.

DC ILALA, ORIJINO KOMEDI WASHIRIKI WIKI YA MAZINGIRA KATA YA KIVUKONI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akishiriki zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala jana asubuhi. Wa pili kushoto ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.
 
 Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (kushoto) akifanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni karibu na maeneo ya Aga Khan sambamba na wafanyakazi wenzake pamoja na Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi,Sekioni David ‘Seki’ (wa kwanza kulia) katika kuadhimisha wiki ya Mazingira.
 
 
Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Katikati niMeneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.
 Wadau mbalimbali kutoka Green WastePro Ltd, Manispaa ya Ilala, Forum CC pamoja na wasanii mbalimbali wakiendelea kufanya usafi kwenye fukwe ya bahari ya Hindi kata ya Kivukoni katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira.
 
 Hali ilivyokuwa kabla ya kufanya usafi.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shay o(kulia) wakati wa zoezi la kusafisha fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Kushoto ni Msanii maarufu wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi, Lukac Mhavile “Joti”
 
 Wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd wakiendelea zoezi la usafi katika fukwe za bahari ya Hindi eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akizungumza jambo na Afisa Mazingira Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda wakati wa zoezi la kufanya usafi kwenye fukwe ya bahari ya Hindi eno la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira.
Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo ( wa tatu kutoka kulia) akifaya usafi na wadau mbalimbali kwenye wiki ya Mazingira eneo la Agha Khan jijini Dar, wa pili kutoka kulia ni Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw. Abdallah Mbena.
 Afisa Mazingira Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda akizungumza jambo baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi kwenye fukwe za bahari ya Hindi.
 Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati) ili kuzungumza na wadau mbalimbali waliokuja kujumuika katika zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Agha Khan katika wiki ya mazingira, wa kwanza kulia ni Afisa Usafishaji Manispaa ya Ilala, Bw. Charles Wambura.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akisitiza jambo kwa wadau walioshiriki zoezi la usafi katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Aga Khan na kuwaomba waendelee na kufanya usafi na hata kuwahamasisha watu wengine kuwa mabalozi wa mazingira ili kufikia malengo waliyojiwekea katika manispaa ya Ilala.
 Baadhi ya wadau waliofika kwenye zoezi la usafi katika wiki ya Mazingira lililoendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd.

TAASISI KUTOKA INDIA YAWAPIGA MSASA WAKAGUZI WA MIGODI NCHINI

$
0
0

????????????????????????????????????

Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini (Kushoto) akijadiliana jambo na Mtaalam mwelekezi kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh (Kulia) kwenye mafunzo yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodini nchini  yaliyofanyika  mjini Bagamoyo mkoani  Pwani.
????????????????????????????????????
Sehemu ya washiriki wa mafunzo yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodini nchini  yaliyofanyika  mjini Bagamoyo mkoani Pwani  wakishiriki katika zoezi la kuandaa mpango wa mazingira kwa vitendo katika mafunzo hayo.
……………………………………..
Na Greyson Mwase, Bagamoyo
Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka nchini India (Centre for Science and Environment) kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini, imekamilisha mafunzo ya siku nne yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodi nchini ambapo wakaguzi walijifunza jinsi ya kuandaa miongozo mbalimbali kwa ajili ya kutumika kwenye ukaguzi wa mazingira kwenye migodi.
Akizungumza katika mahojiano maalum wakati wa mafunzo hayo, Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje alisema lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa uelewa wakaguzi wa mazingira na migodi nchini wa kuandaa, kuchambua na kupitia taarifa za athari kwenye mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini. 
Mhadisi Samaje alisema kuwa uelewa huu utawapa uwezo wakaguzi wa migodi kuchangia kikamilifu taarifa za athari kwa mazingira zinazowasilishwa na wawekezaji katika sekta ya madini kupitia Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC).
Mhandisi Samaje ambaye pia ni Mkaguzi Mkuu wa Migodi aliendelea kusema kuwa mbali na kuwapa wakaguzi wa migodi uelewa wa kupitia taarifa za athari kwenye mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini nchini, mafunzo hayo yanawapa uwezo zaidi wa kukagua shughuli za utunzaji wa mazingira katika migodi kwa kuzingatia masharti ya mpango wa utunzaji wa mazingira ili kuhakikisha kuwa mazingira yanatunzwa ipasavyo.
Alisema nchi ya Tanzania inahitaji miongozo mbalimbali iliyo bora katika usimamizi wa mazingira, na kusisitiza kuwa ili kukidhi haja hiyo, Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikiandaa mafunzo yanayohusiana na ukaguzi wa mazingira kwenye migodi ili kuhakikisha kuwa uchimbaji madini unakuwa ni salama.
“ Kama Serikali tunataka kuhakikisha kuwa mbali na wachimbaji madini nchini kunufaika na kipato kutokana na shughuli za uchimbaji madini, tunataka wafanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa mazingira,” alisema Mhandisi Samaje.
Alisisitiza kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine nchini katika kuhakikisha kuwa mazingira hususan kwenye maeneo ya migodi yanatunzwa ipasavyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo, walisema mafunzo hayo yaliwapa uelewa mpana katika usimamizi na ukaguzi wa mazingira kwenye migodi.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Mhandisi Migodi Jones Mushi kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini alisema kuwa mafunzo hayo yamewawezesha kujifunza jinsi ya uandaaji wa taarifa za mazingira, pamoja na vigezo vinavyotumika katika kuchambua taarifa za mazingira.
Mhandisi Mushi alisema mafunzo hayo yamewawezesha kufanya kazi kwa kujiamini kutokana na uzoefu walioupata kutoka nchi ya India ambao utawawezesha kuboresha utendaji kazi wao.
Naye Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Cuthbert Cyprian aliongeza kuwa mbali na kujifunza uandaaji wa miongozo mbalimbali katika ukaguzi wa mazingira kweye migodi, wamejifunza namna ya uandaaji wa hadidu za rejea kwa ajili ya kuandaa tathmini ya athari za mazingira
Mhandisi Cyprian alisema mafunzo hayo yaliwawezesha kujifunza jinsi ya kukabiliana na athari za mazingira kwenye migodi pamoja na ulipaji fidia kwa waathirika pindi migodi mipya inapoanzishwa.
“Zoezi la ulipaji fidia lina changamoto zake, lakini uzoefu tulioupata kutoka nchi ya India kupitia mafunzo haya ninaamini utatuwezesha sisi kama wataalam kuboresha maeneo yenye kuhitaji maboresho ili kumaliza changamoto hizo,” alisema Cyprian.
Cyprian aliiomba Serikali kuendelea kutoa mafuzo zaidi katika ukaguzi wa mazingira kwenye migodi pamoja na uboreshaji wa sheria na kanuni za mazingira ili kuhakikisha kuwa wachimbaji madini wanafanya shughuli zao katika mazingira ambayo ni bora na salama.
Naye Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Fadhili Kitivai alisema kuwa mafunzo hayo yaliwawezesha kujifunza mikakati mbalimbali ya utunzaji wa mazingira hasa baada ya shughuli za madini kumalizika.
Alisema mara nyingi baada ya shughuli za uchimbaji madini kumalizika nchini, migodi mingi imekuwa ikijitahidi kurudisha maeneo yake katika uasilia wake na kusisitiza kuwa kupitia mafunzo hayo, walijifunza mbinu mbadala za kuendeleza maeneo yaliyoachwa na migodi.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

$
0
0
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani moja ya fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati alipofika Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo Juni 4, 2015 kwa ajili ya kuchukua fomu hizo. Kushoto ni Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni ,
Seif Khatib. Picha na OMR
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, baada ya kukabidhiwa mkoba huo na Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni , Seif Khatib, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo, Juni 4, 2015.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa Fomu hizo. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuchukua fomu, leo Juni 4, 2015. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.
9
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria Mkutano wa Makamu wa Rais Dkt. Bilal. alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
101112
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanachama wa CCM na wanahabari, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu za kuwania urais.
14
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Fomy za kusaka wadhamini, mmoja kati ya vijana waliojitolea kusambaza fomu za kutafuta wadhamini, Saada Ilasi, baada ya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma.
Viewing all 6902 articles
Browse latest View live