Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all 6882 articles
Browse latest View live

MAOMBI YA MCHANGO WA UJENZI WA MSIKITI

$
0
0

Katika Maisha yetu Wanaadamu Ibada ni Jambo Muhimu saana. 
Uzuri , Usafi wa sehemu ya kuabudu ni Moja katika mambo mazuri yenye kupendeza katika kila Nafsi ya Binaadamu.

Katika Nyumba (Msikiti)  huu , Ndugu zetu wanafanya Ibada ya Swala 5 kwa siku , Msikiti huu upo Mkoa wa Pwani , Wilaya ya Mkuranga , Kijiji cha Mlamleni Kitongoji cha Kimbangulile. 

Wenzetu wameanza kwa Nguvu zao  Ujenzi wa Msikiti kama Mnavyo uona.
Jitihada nyengine wameweza kuwa na Matofali yasiyo pungua 300 kwa Ajili ya kuanza Ujenzi Mpya. 

Ukiwa Umeguswa na hili tunaomba kutoka kwako MCHANGO WAKO WA VIFAA VYA UJENZI.

Kwa Mwanzo Tunahitaji 
1.Cement 
2.Tofali
3.mchanga
4.Vifaa vya Kuchimbia Majembe, Panga , chepe N.k

Maazimio yetu tuanze Ujenzi pale tu tutakapo pata uwezo wa kulifanya hili.

Tunawakaribisha mtembelee eneo la tukio kwa wale ambao Mtakuwa na  Na Muda wa kufanya hivyo.

Michango yenu tunaomba muwasilishe kwa Namba ya Simu.
0715800772( Tigo Pesa ) GHALIB MONERO.

Kwa wale waliopo Nje ya Tanzania : WESTERN UNION : GHALIB NASSOR MONERO 

Waliopo KENYA tafadhali wasiliana ALI BAJIY NASOR no' 0725113783 M-PESA.

More Update kuhusu Michango ya Msikiti huu Tafadhali Tutembelee : facebook : Kijana wa Kiislam Dsm or Whatssap Number : +255689604780

Au Piga Simu : +255715800772

Tunawashukuru kwa Michango yenu na Ubalozi wenu Mzuri wa kuitangaza kheri hii . 

WABILLAHI TAUFIQ WENU KATIKA UTUMISHI WA DINI KATIKA JAMII.

GHALIB N MONERO.

WAZIRI NYALANDU ASAINI MKATABA MSUMBIJI KULINDA SELOUS

$
0
0
 Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akibadilishana hati za makubaliano ya  kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji na waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini Celso Coreia, ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili , utaalamu na vifaa, jana mjini Maputo Msumbiji.
  Waziri wa maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu akimsikiliza waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini, Celso Coreia jana mjini Maputo kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji ambapo mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili , utaalamu na vifaa.
 Waziri wa Maliasii na Utalii, Lazaro Nyalandu na waziri wa Ardhi na Maendeleo vijijini wa Msumbiji Celso Coreia wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la selous nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji ambapo  mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili, utaalamu na vifaa. 

MOAT WAPINGA MUSWADA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI

MADKTARI BINGWA WA WA TIBA YA MIFUPA, WAANZA MKUTANO WAO DAR

$
0
0
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,  (MOI), Dkt. Othman Kiloloma (kulia) akifungua mkutano wa tatu  wa madaktari bingwa wa mifupa uliyofanyika katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaa , Mei 26, 2015
Daktari Bingwa wa Mifupa wa Taasisi hiyo Dk. Edmund Ndalama (kulia)  akizungumza na Madaktari bingwa kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania na Marekani ambapo lengo ni kubadilishana ujuzi kwa nadharia na vitendo na unatarajia kumaliza Mei 29
 Dkt. Zehrabanu Zulfikar akizungumza na  wakati wa 
mkutano huo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othman Kiloloma (kulia) akisalimiana na Rais  wa Fracture Care International  Dkt Lewis Zirkle, ambaye ametoa msaada kwa hospitali 10 za Tanzania ikiwemo na Taasisi ya mifupa, ambapo kila chuma kimoja ni Dola 600/= na Moi hadi sasa imesaidiwa vyuma vya tiba 4000
washiriki wakifuatilia kwa makini

 Dkt. Bingwa na Rais  toka Maerkani na Muasisi wa Fracture Care International, Dkt Lewis Zirkle (kulia) akiwa na Dkt. Bingwa wa Taasisi ya Mifupa Moi Dk. Rabi Ndeserua
 Dk. Edmund Ndalama (mbele) akiwa na madaktari bingwa wa mifupa wakifuatiliamkutano huo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kushoto) akifatiliajambo wakati wa mkutano huo wa madkt. wa Mifupa  kwenye Mkutano huo wakati alipokuwa akizungumza  Dkt. Bingwa na Rais wa  Fracture Care International toka Marekani na Muasisi  Dkt Lewis Zirkle,
 Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa
 Makt. wakiwa katika picha ya pamoja Baada ya kufanya Upasuaji wa Mifupa kwa mgonjwa

 Dkt. wa Mifupa Moi Dkt. Billy Haonga akielekeza jambo kwa madkt. Bingwa wenzake toka Nchi mbalimbali    kabla ya kumfanyia mgonjwa mwingine
 Wauguzi wa Taasisi ya Mifupa Moi wakimwangalia mgonjwa kwa ukaribu baada ya kufanyiwa Upasuaji katika Taasisi hiyo
 Dkt. Bingwa na Rais wa  Fracture Care International toka Marekani na Muasisi  Dkt Lewis Zirkle (kulia), akijadiliana na Madkta wenzake kabla ya Kumfanyia mgojwa huyo
 Dkt. Bingwa na Rais wa  Fracture Care International toka Marekani na Muasisi  Dkt Lewis Zirkle (wa pili kushoyo), akijadiliana na Madkta wenzake kabla ya Kumfanyia mgojwa huyo wakipitia Fail lake

ZIARA YA VIONGOZI WA CHADEMA KANDA YA ZIWA

$
0
0
tun1
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Halmashauri, mjini Bariadi, mkoani Simiyu hivi karibuni alipokuwa mkoani humo kwa ajili yakuzindua mpango maalum uitwao ‘Changia Chadema Kanda ya Serengeti ili Kushinda Uchaguzi 2015′ unaolenga kukusanya fedha kampeni za wagombea wa ubunge na udiwani mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara.
tun2
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Halmashauri, mjini Bariadi, mkoani Simiyu
tun3
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Salum Mwalim akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni mjini Magu, mkoani Mwanza, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya chama kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kujiandaa kupiga kura uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
tun4
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Salum Mwalim akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni mjini Magu, mkoani Mwanza

MAKONGORO NYERERE KUTANGAZA NIA BUTIAMA JUNI 1 2015

$
0
0
Makongoro Nyerere
Mtoto wa Muasisi wa Taifa la Tanzania, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarange Nyerere, Makongoro Nyerere anataraji kutangaza nia ya kuwania kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Juni mosi mwaka huu, kijijini Butiama, mkoani Mara. 
 
Makongoro ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki ameweka hadharani hilo na kutoa mwaliko kwa watu wa kada mbalimbali wakiwepo wanahabari kuhudhuria mkutano wake huo utakao anza majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana.
 
Endapo Makongoro atashinda kinyang’anyiro hicho ambacho hadi sasa ndani ya CCM kimeonesha kuwavuta wanasisa wengi akiepoWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe,  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na  Mawaziri kadhaa wa serikali ya sasa atakuwa miongoni mwa watoto wa marais wanayaongoza mataifa ya Afrika.
 
Miongoni mwa watoto wanaoongoza nchi za Afrika na baba zao waliwahi kuwa marais ni Rais Joseph Kabila wa Congo DRC aliyemrithi babayake Laurent Kabila, Rais Uhuru Kenyata wa Kenya aliyefuata nyayo za babayake Mzee Jomo Kenyata na pia aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar, Amain Abeid Karume aliyefuata nyayo za Muasisi wa Muungano wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume.

TANZANIA KUTOA NAFASI ZAIDI KUWEZESHA WAKIMBIZI KUWA NA MAISHA YA KAWAIDA

$
0
0
DSC_0009Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa ndege Kigoma akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia) na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto) kwa ajili ya kutembelea na kuona changamoto katika maeneo maalum wanapohifadhiwa Wakimbizi. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Juma Abdulla Saadala.
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
DSC_0014Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akisamiana na  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui (kulia) pamoja na viongozi wengine wa usalama wa mkoa wa Kigoma mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma akiwa na mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto).
DSC_0016Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiendelea kusamiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kigoma waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma.
DSC_0019Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui mara tu baada ya kuwasili akiwa amefuatana na Waziri Chikawe (hayupo pichani).
DSC_0018Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akifurahi jambo na Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma mara tu baada ya kuwasili.
DSC_0024Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux (kulia) mara tu baada ya kuwasili mjini Kigoma tayari kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.
DSC_0027Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akifafanua jambo kwa viongozi wenzake mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma. Wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux.
DSC_0036Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux kuelekea chumba maalum cha mapumziko mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma.
DSC_0049Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akimsikiliza Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (katikati) walipokuwa kwenye chumba cha mapumziko.
DSC_0071Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kabla ya kusomewa kwa taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi mkoani Kigoma.
DSC_0099Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru akisoma taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini Kigoma.
DSC_0113Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza kwenye mkutano wa kupokea taarifa fupi ya hali ya wakimbizi katika mji wa Kigoma na changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
DSC_0128Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia jitihada zilizofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi katika kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa haraka zaidi ili wakimbizi nao wafarijike kama binadamu wengine sambamba na sheria za Umoja wa Mataifa zinavyotaka. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na watatu kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
DSC_0134Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma.
DSC_0146Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akizungumza katika mkutano huo ambapo ameipongeza serikali ya Tanzania kwa moyo wake wa upendo na kutenga maeneo maalum ya kuhifadhi Wakimbizi kutoka nchi za jirani.
DSC_0163Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katika picha ya pamoja ya viongozi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa mkoa wa Kigoma sambamba wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yaliyopiga kambi mkoani Kigoma kuhudumia Wakimbizi.
…………………………………………………………………………….
Na Modewjiblog team, Kigoma
Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Tanzania itatoa nafasi zaidi kuliko ya sasa ili kuweza kuwaweka wakimbizi wa Burundi wanaoingia nchini katika mazingira ya kuishi maisha ya kawaida.
Kauli hiyo ameitoa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma jana kabla ya kuelekea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na kujionea hali ilivyo akiambatana na watendaji wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini.
Alisema kama taifa wameona uwingi wa Wakimbizi na watatoa nafasi zaidi ili kuwezesha Wakimbizi hao kupata mahitaji yao ya msingi kwa mujibu wa taratibu za Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi.
Alisema katika kufanikisha suala la kuhudumia Wakimbizi wanaomiminika kwa sasa serikali itashirikiana na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuhakikisha mahitaji ya msingi kwa Wakimnbizi hao yanapatikana.
“Wakimbizi wanahaki ya kulindwa na kuthaminiwa kama wananchi wa Tanzania, kwa hiyo serikali itatoa nafasi zaidi na tunashukuru msaada tunaopata kutoka kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kukabiliana na tatizo hili …,” alisema.
Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja wa Mataifa unatiwa shaka na hali ya kisiasa ilivyo nchini Burundi na kusema kuyumba kwa hali ya kisiasa kunaweza kuleta Wakimbizi wengi nchini.
Alisema kwa sasa Umoja wa Mataifa unafanya kazi na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika na wanachama wengine wa jumuiya za kimataifa kuhakikisha kwamba hali ya usalama inarejea nchini Burundi.
Aidha aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia kutatuliwa kwa mgogoro wa Burundi.
Rodriguez alisema Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa namna inavyoshughulikia Wakimbizi na kusema Umoja wa Mataifa unaangalia hali inayojitokeza Burundi kwa makini ili kusaidia Tanzania isilemewe na Wakimbizi.
Aidha alisema kwamba kitendo cha serikali ya Tanzania kutoa nafasi zaidi ya kuwezesha kusiwepo na msongamano wa Wakimbizi Nyarugusu kunaonesha ushirika wa kweli kati ya serikali ya Tanzania na jumuiya ya Kimataifa katika kushughulikia matatizo ya Wakimbizi.
Alisema hata hivyo kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya ni gharama kubwa na kuitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya.
Aidha alisema kwamba Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakifanyakazi kama shirika moja, chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR) wameitikia wanavyostahili pamoja na changamoto nyingi walizokumbana nazo.
Changamnoto hizo ni pamoja na uwingi wa Wakimbizi waliokuwa wakimiminika, umbali uliopo wa kambi ya Kagunga ambako walikuwa wanafikia huku waliowengi wakiwa wanawake na watoto.
Alisema hata hivyo UNHCR walifanikiwa kuwasajili Wakimbizi hao na kuandaa mazingira ya ukazi wao katika kambi ya Nyarugusu. Aidha wamewezesha usafiri kwa Wakimbizi kutoka Kagunga hadi Kigoma.
Pia alisema IOM walifungua njia kutoka Kagunga hadi eneo jirani ambako Wakimbizi walipakia katika mabasi na kufika katika vituo walivyotakiwa kuwepo.
Pia UNICEF waliweza kusaidia maji na vifaa vya usafi kwa watoto na WFP wao walihakikisha chakula kinafikishwa hasa biskuti za kuongeza nguvu.
Aidha WHO wao walikuwa wanaisaidia serikali katika kukabiliana na mlipuko wa Kipindupindu.
Aidha UNFPA walishughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Mratibu huyo alisema kwamba hata hivyo mambo yote hayo yasingefanikiwa kama si kwa msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa.
Mratibu huyo alisema kuwa Mashriika ya Umoja wa Mataifa yameanza kupata fedha za kusaidia katika shughuli zao na kwamba kuna ahadi ya dola za Marekani milioni 12.
Alisema kwamba Umoja wa Mataifa umeona kwamba kutitirika kwa Wakimbizi hao kumeleta hali ngumu kwa serikali ya Tanzania na wakazi wa Kigoma.
Alisema wanatambua changamoto zinazoambatana na kuwa na kundi kubwa la Wakimbizi lakini wataendelea kuhitaji msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika kipindi hiki kigumu.

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR CHAANDAA MAFUNZO YA HAKI ZA BINAADAM NA SHERIA ZA WANDISHI WA HABARI UNGUJA

$
0
0
hg1
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar Bi. Maryam Hamdani akifungua mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari kuhusu Haki za binaadamu na sheria za waandishi wa Habari katika kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kiliopo Migombani.

hg2
Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mohd Khamis akiwasilisha mada ya Chimbuko, Historia na Maendeleo ya Haki za Binadamu Kimataifa, Kikanda na Tanzania katika mafunzo ya waandishi wa Habari yaliyofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Migombani.
hg3
Mwenyekiti wa mafunzo hayo Salma Saidi akitoa muongozi kwa washiriki wa mafunzo hayo.
hg4
Mwandishi Mkongwe wa habari Tanzania Salim Said Salim akiwasilisha mada ya Kanuni, Miiko na Maadili ya Waandishi wa Habari Kimataifa na kitaifa katika semina ya waandishi wa Habari iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria Zanzibar.

hg5
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
hg6
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji akiwasilisha mada juu ya Mapitio ya sheria za uandishi wa Habari Zanzibar.
hg7

Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo Bi. Maryam Hamdani (wa pili kulia) na washiriki wa mafunzo hayo.
Picha Na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAALIMU TANZANIA(CWT)

$
0
0
kjj1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Chama Cha Waalimu TANZANIA( CWT) uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto nje kidogo ya mji wa Arusha jana. Wakati wa mkutano huo wanachama wa CWT ulitarajia kuwachagua viongozi wapya wa chama Hicho. Akizungumza katika  mkutano huo Rais Kikwete ameahidi kutatua changamoto moto mbalimbali zinazowakabili waalimu nchini(picha na Freddy Maro)
mr1
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akisalimiana na walimu waliofika katika mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) unaoendelea  jijini Arusha .Jumla ya walimu 1000 wanahudhuria mkutano huo kutoka sehemu mbalimbali nchini. Picha na Mahmoud Ahmad
mr2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akiteta jambo na mmoja kati ya Waasisi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Thom Abieko jana wakati alipofungua mkutano mkuu wa chama hicho jijini Arusha.Jumla ya walimu 1000 walihudhuria mkutano huo kutoka sehemu mbalimbali nchini.Picha na Mahmoud ahmad
mr3
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akiwasili katika ukumbi wa mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) unaoendelea  jijini Arusha. Jumla ya walimu 1000 walihudhuria mkutano huo kutoka sehemu mbalimbali nchini ambapo Rais Kikwete alihutubia. Picha na Mahmoud Ahmad
mr4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete akizungumza jambo  na mmoja kati ya Waasisi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Thom Abieko jana wakati alipofungua mkutano mkuu wa chama hicho

TANZANIA YATILIANA SAINI NA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA ( AFDB ) MJINI ABIDJAN- IVORY COAST.

$
0
0
1
Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Servicus B.Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. AlyAbou- Sabaa wakisaini mkataba wa Tsh 137.5 Billion kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo kwa serikali ya Tanzania.Sherehe hiyo ilifanyika hapa Mjini  Abidjan- Ivory coast.
2
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw.AlyAbou – Sabaa na Gavana wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicius Likwelile wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba wa Tshs 137.5 Billoni wa kusaidia kwenye sekta ya umeme na nishati nchini Tanzania.
3
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. AlyAbou-Sabaa na Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaa mbaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicius Likwelile pamoja na wajumbe waliohudhuria katika hafla ya kutia saini mkataba wa kiasi cha Tsh. 137.5 Billion kwaajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo hasa umeme nchini Tanzania.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AFUNGA MKUTANO WA NNE WA SIKU TATU WA MABALOZI WA TANZANIA

$
0
0
Balozi Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa Mabalozi wa Tanzania uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Ramada Mjini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mabalozi wa Tanzania katika Mataifa mbali mbali Duniani walioshiriki Mkutano wao wakifuatilia Hotuba ya Ufungaji wa Mkutano huo iliyosomwa na Balozi Seif kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. ASli Mohammed Shein.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Tanzania Nchi mbali mbali Duniani mara baada ya kufunga Mkutano wao wa Nne ulifanyika Ramada Hoteli Jijini Dar es Salaam. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Bernard Membe, Katibu Mkuu Mpya wa Wizara hiyo Balozi Lebereta Mula mula na kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mhadhi Juma Maalim.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Jamuhuri ya Watu wa China Balozi Abrahaman Nyimbo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania Mjini Dar es salaam.
 Picha na – OMPR – ZNZ. 
………………………………………………………………………
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema Mabalozi wanayoiwakilisha Tanzania katika Mataifa tofauti Duniani wanapaswa kuitekeleza vilivyo Sera ya Mambo ya Nje inayolenga katika Diplomasia ya uchumi ambayo ndiyo muongozo wao katika utekelezaji wa jukumu lao la msingi.
Alisema Sera hiyo ni vyema ikatumika vizuri wakati huu ambao Taifa la Tanzania linatekeleza Dira ya kuelekea uchumi wa Kati na kati ifikapo mwaka 2020 kwa upande wa Zanzibar na Mwaka 2025 kwa Tanzania Bara.
Dr. Ali Mohammed Shein alisema hayo wakati akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa Mabalozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.
Alisema katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje yenye kuweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi Tanzania imepiga hatua kubwa vikiwemo Visiwa vya Zanzibar.
Dr. Shein alifahamisha kwamba matunda ya Sera hii yanadhihirisha wazi ukuaji wa sekta ya Utalii, miradi mengine ya kiuchumi ikiwemo pia ile mikubwa inayotekelezwa na wahisani kwa upande wa Zanzibar.
“ Mikakati mipya ya muda mfupi na mrefu mliowekeana katika Mkutano huu ni msingi mzuri kabisa kufuatana na mabadiliko ya uchumi yanayotokea Duniani na kufikia malengo ya Dira ya 2020 na 2025 “. Alisema Dr. Shein.
“ Nina hakika kuwa katika Mkutano huu mmeweza kuziba nyufa zote zilizojitokeza katika utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 inayolenga katika Diplomasia ya Uchumi ambayo ndio muongozo wetu katika utekelezaji wake na ni jukumu letu la msingi “. Alisisitiza Dr. Shein.
Rais wa Zanzibar alieleza kwamba licha ya mafanikio makubwa ya kiuchumi na maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa kwa upande wa Zanzibar lakini bado iko haja kwa Mabalozi hao wa Tanzania kuongeza juhudi za kuitangaza Zanzibar katika Mataifa waliyopangiwa kutekeleza majukumu yao ya Kidiplomasia.
Alisema mafanikio ya Zanzibar katika kukuza sekta ya Utalii , uwekezaji na utekelezaji wa mipango mengine ya maendeleo hutegemea sana juhudi za Ofisi za Kibalozi katika kuitangaza Zanzibar nchi za Nje.
Dr. Shein alifahamisha kwamba baadhi ya wakati Serikali imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wawekezaji, watalii na wageni wanaofika Zanzibar juu ya ukosefu wa taarifa za kutosha kuhusu Zanzibar katika Ofisi za Kibalozi za Tanzania.
Aliwakumbusha Mabalozi hao kwamba katika kutekeleza majukumu yao ni vyema kila wakati wakazingatia kuwa Ofisi zao zinaweka taarifa za kutosha juu ya sekta zote muhimu za kiuchumi na kijamii za pande zote mbili za Jamuhuri hasa zile fursa za uwekezaji vivutio vya utalii.
“ Suala hili nimekuwa nikilikumbusha kila ninapopata fursa ya kuzungumza nanyi, hasa wakatia mbao Mabalozi huja kunitembelea na kuniaga kabla ya kuripoti katika vituo vyao vya kazi “. Alifafanua Dr. Shein.
Alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kupokea mawazo ya Mabalozi hao ili kupata fursa nzuri ya nini Wanadipomasia hao wakitangaze kuhusu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar alihimiza kwamba katika kipindi hichi ambapo Nchi mbali mbali Duniani zimekumbwa na misukosuko ya kutetereka kwa hali ya amani na utulivu Mbalozi hao wanapaswa kuzitangaza fursa ya kiuchumi zilizopo Nchini na kuzihusisha na hali ya amani na utulivu uliopo Nchini Tanzania.
Alieleza kuwa amani na utulivu ni miongoni mwa vigezo muhimu vya awali vinavyozingatiwa na wawekezaji pamoja na wageni wanaotaka kwenda nje ya nchi zao kwa nia ya kuwekeza na kufanya biashara.
Mapema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mh. Bernard Membe alisema utekelezaji wa sera ya mambo ya nje inayolenga katika Diplomasia ya Uchumi umeleta faida kubwa katika uchumi wa Taifa ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Waziri Membe alisema ipo miradi kadhaa ya kiuchumi iliyotokana na sera hiyo kufuatiwa kutanganzwa na Ofisi za Kibalozi za Tanzania akiitaja kuwa ni pamoja na misaada ya maendeleo iliyofadhiliwa na mpango wa Milenia wa Marekani MCC na mradi wa chuma wa Mchuchuma.
Mh. Membe alisisitiza pia kuwa ipo miradi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Tanzania kusamehewa mikopo tofauti kutoka kwa baadhi ya wafadhili, mradi wa huduma za maji safi unafadhiiwa na Serikali ya Japan pamoja na mradi wa Kilimo kwa upande wa Visiwa vya Zanzibar.
Alisisitiza kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya nje itahakikisha kwamba inaendelea kuchangia vikosi vya kulinda amani Barani Afrika.
Akitoa shukrani kwa niaba ya washiriki wa Mkutano huo wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania Nchi Mbali mbali Duniani Dini wa Mabalozi hao Balozi Kijazi alisema Maalozi hao wakirudi vituoni mwao watakuwa na kazi moja tu ya kutekeleza yale waliyoyajadili na kukuibaliana katika Mkutano huo.
Balozi Kijazi alilihakikishia Taifa kwamba Mabalozi hao wana nia safi ya kutekeleza majukumu yao kwa ufasini uliotukuka, lakini lakuzingatia zaidi ni uwezeshwaji wao ili kutekeleza vyema kazi yao hiyo ya Kidiplomasia.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

MISA YA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA KUFANYIKA JUMAMOSI MAY 30, 2015

$
0
0
MZEE SAMUEL NTAMBALA LUANGISA
 
Familia ya Marehemu Mzee Luangisa na New York Tanzania Community, inawakaribisha kwenye MISA ya kumuaga Marehemu Mzee wetu, Baba yetu na Kiongozi wetu Mzee Samuel Ntambala Luangisa (83), kabla ya kwenda Bukoba kwa mazishi Siku Jumamosi MAY 30th, 2015
kuanzia Saa: 1pm – 5pm
 
Address: LEE’S Funeral Home L.L.C
160 Fisher Avenue
White Plains, NY 10606
 
Baada ya Misa sote tutajumuika nyumbani kwa Wafia The Luangisa Residence: 
 
374 Hawthorne Terrace, 
Mt. Vernon, NY 10552
 
Kwa taarifa zaidi wasikiana na:
 
1. Prof. K. Lwiza 631-273-3859
2. Dr. Abas Byabusha 914-584-7502
3. Shabani Mseba 347-712-8539
4. Hajj Khamis 347-623-8965
 
Ukitaka kutoa rambirambi yako unaweza kutumia number hizi hapa chini.
Luangisa na Kwame Luangisa. Bank ni Bank of America. Account# 9504210977. Routing# 021000322. Swift code ni BOFAUS3N. 
 
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake la Bwana litukuzwe. Amen!

YAMOTO BAND, MASHAUZI KUWASHA MOTO MANGO GARDEN LEO

$
0
0

KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kupitisha wikiendi bila burudani yoyote, leo usiku ‘utawaka moto’ wakati Yamoto Band na Mashauzi Classic zitakapotoa shoo kabambe hapo.
Wasanii wa yamoto band.

Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.

Kesho, Ijumaa,  Malaika Band ambao hupiga hapohapo Mango Garden, kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini wakitoa burudani.
Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani 'Isha Mashauzi'.

Vilevile,  Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, wasanii hao Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.  Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi
Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la Nyama Choma.

DR. MENGI AZINDUA MPANGO WA AIRTEL FURSA 'TUNAKUWEZESHA' JIJINI DAR.

$
0
0
  Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pilikulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (kulia) na Menejawa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi wakiwa wameshika bango kamaishara ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, katika haflailiyofanyika jijini Dar es Salaam  jana.
  Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya pasi na meza yake kwa muuza mitumba RashidSeleman (wa pili kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango  huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji    wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma  Mwapachu (wa tatu kushoto) na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
 Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya mashine ya kutengeneza juisi kwa Abdulkarim  Ramadhan (wa tatu kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
 Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi
akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa
‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

RAIS KIKWETE AWAAPISHA KATIBU MKUU, NAIBU KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE NA BALOZI WA TANZANIA SAUDIA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha  Balozi Liberata Mulamula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Balozi Mulamula anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kuongoza Wizara hiyo na kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi  Mulamula  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha. 
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mulamula Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Hassan Simba Yahya  kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huo Balozi Yahya alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
 Mhe. Rais Kikwete akishuhudia Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Yahya  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha. 
Mhe. Rais Kikwete akimpongeza Balozi Yahya mara baada ya kumwapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha, Mhe. Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi  wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mgaza alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu  na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
Rais  Kikwete akishuhudia Balozi  Mgaza  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha.
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mgaza Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya na Balozi Mgaza mara baada ya kuwaapisha katika nyadhifa zao mpya
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja  na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa nne kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (wa tatu kutoka kulia), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya na Balozi Mgaza muda mfupi baada ya kuapishwa.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya,  Balozi Mgaza na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mabalozi wa Tanzania.

MKAPA - ZERO HIV AND AIDS IN TANZANIA IS POSSIBLE

$
0
0

 Dr. Fatma Mrisho, Executive Director for Tanzania Commissions for AIDS (TACAIDS), joined by Former President Hon. Benjamin Mkapa (centre) and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability and their colleagues during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam. TACAIDS received a cheque worth two hundred million so as to facilitate the eradication of HIV and AIDS in Tanzania.
 DC of Geita, Hon. Manzie Mangochie receive TZS 100M on behalf of Geita District Hospital from the Former President Hon. Benjamin Mkapa and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam.
 The Former President Hon. Benjamin Mkapa and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability at AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam.
Some of the participants joined by the Former President Hon. Benjamin Mkapa and The Managing Director of AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine Mr. Terry Mulpeter and Mr. Simon Shayo Vice President of Sustainability at AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine during the launch of Kilimanjaro Challenge 2015 campaign in Dar es Salaam.

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA,GAUDENSIA KABAKA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA(NHIF) JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) jijini Arusha jana, kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Michael Mhando na kulia ni Makamu Mwenyekiti  aliyechaguliwa wa Baraza la Wafanyakazi, Deudedit Rutazaa.
 Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini(NHIF),Michael Mhando akitoa hotuba yake jana wakati wa mkutano wa uchaguzi na uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa mfuko huo.
 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Taifa, Deusdedit Rutazaa akizungumza baada ya kuchaguliwa na kuhaidi kutoa utumishi uliotukuka.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) wakiimba wimbo wa Mshikamano kuhamasisha umoja na  maslahi bora kazini.
 Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
 Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
 Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya NHIF.
Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Mameneja wa mfuko wa  NHIF.

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YASAINI MKATABA WA KUBORESHA HUDUMA ZA UFUNDI WA VIFAA TIBA

$
0
0
af1
Dkt. Mmbando akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkataba huo  toka serikali ya korea ya kusini katika kutoa mafunzo kwa mafundi wa vifaa na vifaa tiba walioajiriwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya hapa nchini ili waweze kuongeza ujuzi katika matengenezo na kuboresha huduma ya ufundi.Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Otilia Gowele
af2
Katibu mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii na naibu meneja toka KOFIH wakisaini mkataba huo. Mkataba huo  utasaidia pia  kuboresha huduma za ufundi wa vifaa tiba katika karakana za ufundi wa vifaa tiba zilizopo katika hospitali za rufaa za kanda, rufaa za mikoa na hospitali za wilaya.
af3
Dkt. Mmbado akikabidhiwa mkataba huo toka kwa Naibu Meneja Gong, In Jae .
…………………………………………………………..
Dkt. Mmbando amesema ,  serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya imeendelea kuboresha upatikanaji na uwepo wa huduma ya vifaa tiba na mashine mbalimbali za teknolojia za kisasa katika ngazi zote za vituo vya kutolea huduma za Afya kuanzia zahanati hadi hospitali ya Taifa. Ili kusimamia matumizi bora na kutunza raslimali hii kumehitajika kuweka juhudi za maksudi kuandaa wataalam wa ufundi wa vifaa tiba kwa kuwajengea uwezo katika kufahamu wa namna ya matengenezo ya mashine zilizopo na zinazo endelea kununuliwa; Pia kuwapa  vitendea kazi(tools kits, measuring and calibration equipment) vyenye kuwezesha mafundi kuhakiki ubora wa ufanyaji kazi kwa baadhi ya vifaa tiba mara baada ya kufanyiwa matengenezo.
“Kwa ushirikiano huu kati yetu na Korea ya Kusini ikiwa ni nchi iliyopiga hatua kubwa kiuchumi na teknolojia au miundombinu kwa ujumla wake ninaimani tutajifunza mambo mengi na kutoa mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya hapa nchini”.
Alisema kikubwa wamelenga kupata ujuzi zaidi kutoka kwao ingawa watagharimia masuala mengi katika mchakato mzima. Tunahitaji sisi wenyewe serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya, Manispaa na Halmashauri zote nchini kuhakikisha vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za Afya vinapatikana na vinatumika kutoa huduma kwa wagonjwa muda wote vinapohitajika.|” Hili litawezekana kama tutatenga bajeti za matengenezo kinga(Planned Preventive maintenance) na kutumia wataalam wa ufundi wa vifaa tiba wanaotambulika “.

HOSPITALI YA POLISI KILWA ROAD YAPATA VIFAA VYA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI

$
0
0

Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto), kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road. Wa kwanza kushoto ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahmani Kaniki.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto), akiongozana na Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam (kulia), kuelekea kwenye jengo litakalotumika kwa ajili ya kuhifadhia maiti  katika hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akizungumza  wakati wa hafla ya makabidhiano ya kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti vilivyotolewa na Serikali ya Misri kwa Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road Jijini Dar es Salaam.


 Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahman Kaniki akizungumza  wakati wa hafla ya makabidhiano ya kontena lenye vifaa vya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, Richard Malika akitoa maelezo kuhusu mchoro wa jengo la kuhifadhia maiti linalojengwa  katika Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na Balozi wa Misri Nchini, Hossam Moharam wakimsikiliza.


SOURCE - Issa Michuzi

Diamond Platinumz aibukia programu ya Mziiki

$
0
0

Nyota wa muziki wa bongo flava nchini Diamond Platinumz amewataka wasanii wa Tanzania kusambaza nyimbo zao kwa njia ya teknolojia kama vile Mziiki iliyozinduliwa hivi karibuni ili ziweze kuwafikia watu wengi na kwa wakati huohuo wanamuziki pia kunufaika na jasho lao.

Diamond anasema kuwa  ameamua kazi zake kuziingiza sokoni tofauti na kazi zake za nyuma ambapo baada ya  kushauriana na wadau anaoshirikiana nao kikazi ameamua aingie sokoni kwa njia ya kidigitali kupitia programu ya Mziiki iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo pia yeye ni balozi anayeitangaza.

Anasema Tanzania ina wanamuziki wengi wenye vipaji lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiwafanya wasifike mbali zaidi ya muziki wao kusikika hapa nchini na wengi wao kutamba kwa muda mfupi na kupotea katika ulimwengu wa muziki huku wakiwa hawajanufaika na kitu chochote kimaisha na kushauri kuwa  wasibaki nyuma kiteknolojia hasa wakati wa kupeleka kazi zao sokoni iwapo watataka kujikwamua.

“Licha ya kuwepo na changamoto kubwa kama vile kutokuwepo sheria ya hakimiliki inayopelekea wasanii kuibiwa kazi zao na kazi za muziki kutumiwa na vyombo vya habari kama redio na televisheni  bila kuwalipa wahusika chochote. Tatizo lingine linalodumaza muziki wa Tanzania ni uoga wa wanamuziki kubadilika na  kuogopa teknolojia za kisasa kama  hii programu ya kupakua muziki kwenye simu kwa kupitia Mziiki” Alisema.

 Amesema  sababu kubwa iliyopelekea kuamua kufanya biashara ya muziki kupitia progamu hii ni kwamba nyimbo zake ziweze kuwafikia washabiki wake popote na muda wowote kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi na anakuwa na uhakika wa kupata mapato tofauti na kama zinavyosambazwa na wasambazaji wa mtaani.

“Duniani kwa sasa hivi kuna ushindani  mkali katika nyanja zote. Sisi kama wanamuziki wa Tanzania tunapaswa kuhakikisha tunatoa muziki wa viwango vya juu na kuhakikisha tunalenga zaidi katika masoko ndani na ya nje kama wenzetu wanavyofanya kusambaza kazi zao kupitia kampuni zinazotumia teknolojia ya kisasa na kumnufaisha msanii kama ilivyo program hii ya Mziiki. Kuna umuhimu mkubwa wa kujiamini, kufanya vizuri ili tuweze kutangaza Tanzania, kutangaza lugha ya Kiswahili na kupata mapato ya kutosha kutokana na kazi ya muziki ambayo ikifanywa kitaalamu inalipa kwa kiasi kikubwa” anasema Diamond Platinumz

Aliwaomba wapenzi wa muziki nchini kuwaunga mkono wanamuziki wa hapa nchini kwa kupakua nyimbo zao kwenye Mziiki  kwa kuwa njia hii iko wazi na inamuwezesha mwanamuziki kujua kirahisi  jinsi kazi zake zinavyokubalika sokoni na inamuwezesha kujua mapato yake tofauti na njia nyingine kama uuzaji wa CD kwenye maduka na mitaani.

Programu ya Mziiki ambayo ilizinduliwa na Vodacom kwa kushirikiana na  Spice VAS Africa  imeanza kufanya kazi na wanamuziki wa hapa nchini na nje ya nchi na katika  kipindi cha muda mfupi tayari imesajili wanamuziki wapatao 1,000  ambao kazi zao  hususani zile mpya zitasambazwa kwa njia ya kidigitali na malengo yake makubwa ni kuhakikisha wanamuziki wanapeleka kazi zao sokoni kwa haraka na kunufaika na jasho lao hususan pale ambapo wananchi wengi watatumia mtandao kwenye simu zao kupakua nyimbo wazipendazo za wanamuziki ambao wamejiunga kwenye tovuti ya kampuni hiyo ambayo inapatikana kwa kubofya tovuti ya www.mziiki.com.
Viewing all 6882 articles
Browse latest View live