Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all 6883 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA TANO WA JUMUIYA YA MADOLA NA WAKUU WA TAASISI ZA KUPAMBANA NA RUSHWA BARANI AFRIKA, JIJINI DAR.

$
0
0
 ha1
Makamau wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Mkutano Mkuu wa tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, uliofanyika leo Mei 25 kwenye Hoteli  ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
ha
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia, kufungua rasmi mkutano wa tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, uliofanyika leo kwenye Hoteli  ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
ha3
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia, kufungua rasmi mkutano wa tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, uliofanyika leo kwenye Hoteli  ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
ha4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akifurahia jambo na baadhi ya Viongozi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
ha5ha6ha7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo baada ya kufungua rasmi leo kwenye Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
ha8ha9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, uliofanyika leo Hoteli  ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CHADEMA ,JAFARY MICHAEL AFUNGUA MATAWI MAPYA MOSHI

$
0
0

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema na meya
wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza wakati wa uzinduzi wa
tawi katika kata ya Longuo mjini Moshi.




Ofisi mpya ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kata ya Longuo B .

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema taifa
na meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael akikata utepe kufungua
ofisi mpya ya kata ya Longuo B.
Meya Michael akitia saini katika kitabu cha
wageni mara baada ya kufungua ofisi ya kata ya
Chadema.
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Basil
Lema akitia saini katika kitabu cha wageni wakati wa ufunguzi wa ofisi
ya kata ya Longuo B.

Diwani wa kata ya Longuo B,Ray Mboya akitia
saini katika kitabu hicho.

Baadhi ya makada wa Chadema manispaa ya
Moshi wakishuhudia zoezi hilo.
Ofisi mpya ya Chadema kata ya, Longuo
manispaa ya Moshi ikafunguliwa rasmi.
Na Dixon

Busagaga wa globu ya Jamii kanda ya Kasakazini.

Edward Lowassa azungumza na waandishi wa habari Dodoma

$
0
0

Waziri Mkuu aliyejiuzulu Mh Edward Lowassa leo amezungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake eneo la Area C mkoani Dodoma ambapo amebainisha dhamira yake ya kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).
Katika Mkutano huo na waandishi wa habari, Mh Lowassa amevunja ukimya kwa kusema kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake kuhusu sakata la Richmond si za kweli na hakuhusika.
Mbunge huyo wa Monduli amebainisha kuwa alishangaa kuona kamati ya Dr Harrison Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji.
Ameituhumu kamati hiyo kwa kushirikina na spika wa bunge wakati huo Mh Samwel Sitta kuwa ilikuwa na lengo la kumchafua ili aachie cheo cha uwaziri mkuu.
Mh Lowassa Amesisitiza kuwa hicho hakiwezi kuwa kikwazo kwake kuingia Ikulu.
Mh Lowassa ambaye anaonekana kujipanga vyema, amesema kuwa anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono hivyo haoni tatizo kuwatambulisha baadhi ya watu wanaomuunga mkono.
Mbunge huyo wa Monduli pia amebainisha iwapo chama chake kitamteua na hatimae kushinda nafasi ya Urais, lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu.
Pia amesema kuwa anaamini atafanikiwa kutimiza ndoto yake ya kuingoza nchi hii na kuindoa kwenye dimbwi la umasikini huku akitoa shukrani kwa marafiki zake wanaomuunga mkono.
Amewataka wananchi kuwa tayari kwa mkutano mkubwa atakaoufanya jijini Arusha May 30, ambapo amesema katika mkutano huo ataanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi na mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi ijayo.
Mh Lowassa pia amewaonya wapinzani wake kuwa wasitegemee kama atakihama chama cha Mapinduzi(CCM), ataendelea kuwa ndani ya CCM na harakati zake atazifanya CCM.

Familia ya mtoto aliyegongwa na fuso na kukatwa miguu anaomba msaada wa kisheria

$
0
0

Naibu Kamanda wa UVCCM ,Innocent Melleck akiwa na mama mzazi wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima mara baada ya kukabidhi kiti cha walemavu cha magurudumu kwa ajili ya kusaidia kutoka eneo moja hadi jingine.
Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Melleck akikabidhi Pempers kwa mama wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo aliyepata ulemavu wa miguu miwli baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso.(Na Dixon Busagaga).
Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini ,Innocent Melleck akiwa amembeba mtoto Felista Shirima(3) aliyekatwa miguu yote miwili baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso jirani na nyubani kwao.

Akizungumzia sakata la mtoto huyo Naibu kamanda huyo alisema kuwa ataumia kila aina ya uwezo na nguvu zake kwa kushirikiana na ofisi ya umoja wa vijana wa chama chama mapinduzi UVCCM ili kuhakikisha kuwa  haki ya mtoto huyo inapatikana.
Awali akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada wa baiskeli  ya magurudumu matatu na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba na kamanda huyo, mama mzazi wa mtoto huyo Beatrice Kelvin,aliiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza na kumsaida mwanae ili kuhakikisha haki inapatikana. 

Alisema kesi iliyokuwepo mahakama kwa ajili ya kudai haki za msingi za mwanae imeisha bila haki yake kupatikana licha ya kuhangaika sehemu mbalimba na kuomba vyombo husika vinavyo jishughulisaha na haki za binadamu kuingilia kati suala hilo hatua ambayo itasaida kupata haki.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yatoa Ratiba Rasmi ya Uchaguzi Mkuu.

$
0
0

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali  unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian  Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,  Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa  Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na  kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka - Oktoba 24 mwaka huu.
Halikadhalika siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

SERIKALI YA TANZANIA NA UNESCO KUADHIMISHA WIKI YA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO





IDARA YA HABARI (MAELEZO)

S.L.P.  8031, Dar es Salaam, Simu: 2110585, 2122771/3, Fax: 2113814, e-mail: maelezopress@yahoo.com

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



SERIKALI YA TANZANIA NA UNESCO KUADHIMISHA WIKI YA

UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA NA KUZINDUA MRADI WA NYARAKA ZA URITHI WA TANZANIA



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) itaadhimisha Wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika kuanzia tarehe 25 hadi 29 Mei, 2015 kwa kufanya maonesho ya picha na kumbukumbu mbalimbali zinazoonesha na kuelezea harakati za ukombozi wa bara la Afrika pamoja na midahalo mbalimbali itakayowahusisha wasomi na baadhi wa watu mashuhuri walioshiriki katika harakati za ukombozi.



Maadhimisho hayo yatatanguliwa na uzinduzi wa Mradi wa Nyaraka za Urithi wa Tanzania (TAHAP) utakaofanyika tarehe 25 Mei, 2015 katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam. Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mhe. Bernard Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.



Mradi wa Nyaraka za Urithi wa Tanzania unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na UNESCO ukikamilika unaatarajia kuweka na kutunza  kumbukumbu na nyaraka mbalimbali zinazohusu harakati za ukombozi wa bara la Afrika na ushiriki wa Tanzania kama mwenyekiti wa iliyokuwa Kamati ya nchi za mstari wa Mbele katika kuzikomboa nchi na kuvijengea uwezo vyama vya wapigania uhuru kusini mwa bara la Afrika.



Miongoni mwa matukio muhimu katika maadhimisho hayo ni mdahalo utakaohusu Mchango wa vyama vya Siasa katika harakati za Ukombozi utakaoongozwa na Mhe. Salim Ahmed Salim na Wazungumzaji Wakuu watakuwa ni Prof. Issa Shivji na Mhe. Ibrahimu Kaduma, aliyewahi kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.



Mdahalo mwingine Utajikita katika kuangalia "Mchango wa Wapiganaji/Wanajeshi katika harakati za Ukombozi" tarehe 26 Mei, 2015 utakaofanyika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam utakaoongozwa na Prof. Penina Mlama na Wazungumzaji Wakuu watakuwa Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Brigedia Jenerali Ananias Mwanga.



Tarehe 27 Mei, 2015 kutakuwa na mdahalo mwingine kuhusu "Mchango wa Wanawake katika harakati za ukombozi" utakaoongozwa na Prof. Ruth Meena na wazungmzaji wakuu watakuwa ni Dkt. Alexander Mkulilo na Mhe. Balozi Getrude Mongela (MB). Mdahalo huu utafanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.



Mdahalo kuhusu "Mchango wa vyombo vya habari Wakati wa Harakati za ukombozi" utafanyika Chuo Kikuu  Huria Cha Tanzania tarehe 28 Mei, 2015 na kufuatiwa na  mdahalo kuhusu "Mchango wa Wasanii na Watunzi katika Harakati za Ukombozi" tarehe 29 Mei, 2015 utakaofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. Mdahalo huo utaongozwa na Mzee Walter Bgoya. Wazungumzaji wakuu katika mdahalo huo watakuwa Prof. Penina Mlama na Bw. Zahiri Zahoro.



Maadhimisho hayo yatafungwa Rasmi na Mhe. Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo tarehe 29 Mei, 2015.



Vyombo vya habari vinaombwa kushiriki kwa kuandika na kutangaza Matukio hayo muhimu katika kutunza kumbukumbu za ukombozi wa bara la Afrika katika mikono ya wakoloni na utawala dhalimu wa Afrika Kusini.


MKURUGENZI IDARA YA HABARI (MAELEZO)

Rais Kikwete ateua mkuu wa Wilaya mwingine apangua vituo vya Kazi

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, kuanzia leo, Jumatatu, Mei 25, 2015.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini.

Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole Lenga kutoka Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera. 

Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict Kulikela Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu, 2015.

Wakuu wengine wa wilaya ambao Rais Kikwete amewahamisha ni Elizabeth Chalamila Mkwasa kutoka Wilaya ya Dodoma kwenda Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Dkt. Jasmine Tisike kutoka Wilaya ya Mpwapwa kwenda Wilaya ya Dodoma, Agnes Elias Hokororo kutoka Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma kwenda Wilaya ya Tunduru, mkoani humo humo na Fadhili Nkurlu kutoka Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Mkalama.

Wengine ambao wamehamishwa ni Chande Bakari Nalicho kutoka Wilaya ya Tunduru kwenda Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka Wilaya ya Mvomero kwenda Misenyi, Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Biharamulo, mkoani humo humo, Elias Choro John Tarimo kutoka Wilaya ya Biharamulo kwenda Chunya, Mkoa wa Mbeya na Deodatus Lukas Kinawiro kutoka Wilaya ya Chunya kwenda Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Mei, 2015

PSPF YAUNGANA NA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KATIKA HAFLA YA KUENDELEZA UMOJA WA WAJASIRIAMALI DAR ES SALAAM

$
0
0

  Meneja msaidizi wa uchangiaji wa hiari Matilda Nyallu wa mfuko wa pensheni wa (PSPF) akieleza namna ya mfuko wa Hiari unavyo kuwa na ni jinsi gani utafaidika pindi unapo jiunga na kuwa mmoja wa wadau wa (PSPF)
 Kushoto Muandaaji wa sherehe ya wanawake wajasiliamali Shamimu Mwasha ambaye ni mdau wa (PSPF) akitoa ufafanuzi wa sherehe hiyo na kuwakaribisha wageni walioweza kuhudhuria pembeni ni mshereheshaji wa sherehe hiyo Jokate Mwegelo.
 Baadhi ya wanawake wajasiriamali wakiwa wameketi pamoja huku wakiendelea kupokea ujumbe mbalimbali kutoka kwa wanawake tofauti tofauti waliokuwepo katika sherehe hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Wanawake wajasiriamali Dar es salaam washerehekea pamoja katika hafra fupi iliyo andaliwa na Mjasiriamali Shamimu Mwasha kwa lengo la kuendeleza kuwa na mahusiano mazuri katika shughuli zao za kuijenga nchi kwakutumia  vipaji na ubunifu walionao ili kuhakikisha bidhaa mbalimbali zakitanzania hazikosekani katika soko la hapa nyumbani hata nje ya nchi.

Mfuko wa jamii wa (PSPF) umeweza kuwaunga mkono wajasiriamali hao kwa kuwa miongoni mwa mfuko unaotoa huduma mbalimbali kupitia mafao yao kwakuwa kunamafao mbalimbali katika  mfuko wa pesheni ambayo wao kama wajasiriamali wanaweza kuyamudu na hatimaye kufikia malengo waliyo jiwekea.

Akizungumza wakati wa sherehe hiyo Meneja msaidizi wa uchangiaji wa hiari Matilda Nyallu amesema mfuko wa jamii wa (pspf) ni mfuko unao jali kila mmoja na nimfuko ambao unakupatia wewe mtanzania faida maradufu kutokana na huduma zinazo tolewa kuwa za kiwango cha hali ya juu amesema kupitia mafao mbalimbali likiwemo fao la mikopo ya elimu,fao la ujasiriamali,nyumba na mengine mengi pia aliweza kuwaeleza kuhusu uchangiaji wa hiari ambapo kupitia uchangiaji huo mtu yeyyote anaweza akaumudu kutokana ni rahisi na inakiwango cha kawaida cha kuchangia .

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU DODOMA

$
0
0

jk2
Mwenyekiti wa CCM Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua juu nakala za kanuni za Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu kuzizindua rasmi wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Shirikisho hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kilimani mjiini Dodoma jana. Kulia ni katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,watatu kulia ni Makamu Mweyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula na kushoto ni mlezi wa shirikisho hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknologia Ndugu January Makamba.
jk1
Rais Kikwete akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa kwanza wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu mjini Dodoma.
jk3
Rais Kikwete akisalimiana na baadahi ya wanafunzi baada ya kufungua mkutano(picha na Freddy Maro).

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA MABENKI YA AKIBA DUNIANI (WSBI) KANDA YA AFRIKA

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akifafanua jambo
wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, kuhusu
mkutano wa mabenki ya Akiba 
Duniani (WSBI) Kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia kesho jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa benki hiyo, Mystika Ngongi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akifafanua jambo
wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu
mkutano wa mabenki ya Akiba Duniani (WSBI) Kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa benki hiyo, Mystika Ngongi na kushoto ni Mundakweli Kaniki Meneja Mwandamizi wa Mipango Mkakati ya TPB. Mkutano huo utashirikisha zaidi ya washiriki 100 kutoka nchi mbalimbali Afrika na viongozi wa Dunia wa Taasisi hiyo ya WSBI ambapo pia TBP ndio Benki mwenyeji wa mkutano huo.

HATMA YA CCM IPO MIKONONI MWA VIJANA

$
0
0
  • Shirikisho lina Wajumbe 683
  • Wanachama 31000
  • Vijana wafurahi kupiga picha pamoja na Nape.
Wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu nchini wakifurahi kupiga picha na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Kila mwanafunzi alipenda apate ukumbushokwa kupiga picha na na Katibu wa NEC Npe Nnauye.
Wajumbe kutoka mikoa mbali mbali wakiimba na kucheza nyimbo za hamasa.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza meza kuu kuimba wakati wa kufungua kwa mkutano wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania.
Kikundi cha burudani kikitumbuiza.
Wajumbe wakishangilia
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Hamis Ngomero kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula na Katibu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Kikwete akiwapungia wajumbe kwenye mkutano huo
Wajumbe wakisikiliza.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania.

WIKI YA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA YAZINDULIWA RASMI

$
0
0
wi1
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga aliyesimama akiongea na washiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana
wi2
Naibu Waziri Wizara ya Dkt. Mahadh Juma Maalim (Mb) akifungua Maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika iliyoanza jana jijini Dar es Salaam.wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na katikati ni Balozi kutoka Umoja wa Ulaya Mh. Filiberto Sebrigondi.
wi3
Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi. Zulmira Rodrigues akiongea na washiriki waliohudhuria katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Bara la Afrika hawapo pichani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
wi4
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (Mb) Dkt. Mahadh Juma Maalim akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waliohudhuria katika Hafla ya Maadhimisho ya Wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
wi5
Mhadhiri wa Sheria na wanaharakati wa haki za binadamu, Prof. Issa Shivji akiongea na washiriki waliohudhuria katika Maadhimisho ya Wiki wa Ukombozi wa Bara la Afrika hawapo pichani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Daud Manongi

UPENDO NKONE, MIKE KALAMBAY WANOGESHA TAMASHA LA GOSPEL COLUMBUS, OHIO

$
0
0
Mwimbaji wa nyimbo za injili wa Columbus, Ohio Enock Mwamba(kati) akiimba moja ya nyimbo za injili huku akiwashirikisha Mike Kalambay aliyekuja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Upendo Nkone aliyekuja toka Tanzania maalum kunogesha tamasha la Gospel lililofanyika siku Jumapili May 24, 2015 na kuhitimisha tamasha hilo lililokua la siku 3 mjini humo lililoanzia siku ya Ijumaa May 22, 2015.
Mike Kalambay akiimba huku akitoa neno la Mungu kwa Kifaransa kilichochanganyika na lingala huku mchungaji Fayes (kulia) akitafsiri kwa kiingereza na Kiswahili.
Mike Kalambay akiimba moja ya nyimbo za injili kwenye tamasha la gospel lililofanyika siku ya Jumapili May 24, 2015 mjini Columbus, Ohio.
Mike Kalambay toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akishambulia jukwaa na nyimbo za injili.
Mwimbaji mahili wa nyimbo za Injili Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zake kwenye tamasha hilo.
Upendo Nkone na mchungaji Donis Nkone wakifuatilia tamasha Mike Kalambay (hayupo pichani).
Mchungaji Donis Nkone na mke wake Nnunu Nkone wakiwa wamepiga magoti wakati Mike Kalambay akiwashukuru kwa kufanikisha ujio wake ikiwa ndio mara ya kwanza kwa yeye kufika mjini humo.

JUMA NATURE NA WENZAKE KULITIKISA JIJI LA DAR TAMASHA LA KOMAA JUMAMOSI NDANI YA UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA

$
0
0
Msanii Juma Nature ‘Kiroboto’ akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la kuadhimisha miaka 16 ya kazi zake za muziki nchini  pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za Kituo cha Redio cha EFM linalofahamika kwa jina la Komaa Concert litakalofanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi Ukumbi wa Dar Live Mbagala kuanzia saa 12 jioni. 

Kushoto ni  Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo, ambao ni waandaaji wa tamasha hilo. Kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Msanii Said Christopher ‘Mucky), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo,Msanii  Juma Nature, Msanii, Semani Jabiri ‘Msagasumu’ na Msanii Snura Mushi.
Wasanii watakaotoa burudani la nguvu siku hiyo ya tamasha. Kutoka kulia, Fredy Felix ‘Fredwayne’ Juma Nature, Snura Mushia, na Said Christopher ‘Mucky)
Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Lydia Moyo (kushoto), akiperuzi simu yake katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.

BENKI YA CRDB YAKABIDHI HUNDI YA SH. MILIONI 20 KWA MEYA WA KINONDONI

$
0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni alipowasili ofisini kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda, (katikati). Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa. 
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei muda mufupi kabla hajakabidhi hundi ya sh.
milioni 20 baada ya meya huyo kupata tuzo ya Meya Bora
Afrika iliyotolewa na Rais Jose Eduardo do Santos wa Angola.
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mussa Natty. 
Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi hundi ya sh. milioni 20 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda zilizotolewa na benki hiyo baada ya  meya huyo kupata tuzo ya Meya Bora Afrika iliyotolewa na Rais Jose Eduardo do Santos wa Angola. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi hundi ya sh. milioni 20
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda zilizotolewa na benki hiyo baada
ya
  meya huyo kupata tuzo ya Meya Bora Afrika iliyotolewa na Rais Jose Eduardo do Santos wa Angola. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Meya wa Kinondoni Yusuf Mwenda akitoa shukrani zake kwa uongozi wa Benki ya CRDB kwa kutambua juhudi wanazofanya katika utendaji kazi na masuala ya usafi na ukusanyaji wa mapato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles kimei akizungumza katika hafla hiyo.
Meya wa Kinondoni Yusuf Mwenda akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Picha ya pamoja.
Dk. Charles Kimei akimpongeza Meya wa Kinondoni kwa tuzo aliyopata.
Picha ya pamoja.
Dk. Charles Kimei akiambatana na Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) na Naibu Meya, Songoro Mnyonge.
Dk. Kimei akibadilishana mawazo na Meya wa Kinondoni.
Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MANJANO FOUNDATION YAKAMILIKA

$
0
0
 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser (Katikati)  akizungumza na Vyombo vya Habari jijini Dar es salaam wakati akelezea Mandalizi ya Uzinduzi wa Manjano Foundation Ambao ni Mpango unaolenga kuwawezesha Kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wasichana wa Kitanzania. Mpango Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 6 mchana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Utatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi..Mgeni Rasmi anategemewa Kuwa Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda
 Meneja Mradi wa Manjano Foundation Mama Gugu Ndolvu Akieleza jambo jana wakati wakiongea na wanahabari kuhusu Mradi huo ambao ni Mkombozi kwa wakinamama wasio na Ajira Akiwa samabamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser  Pamoja na  Aunty Sadaka Gandi
 Aunty Sadaka Gandi akiwa ni dada mkuu wa Atakayewashauri wasichana watakaopata mafunzo ya ujasiriamali kupitia Manjano Foundation. 
Wasichana waliochaguliwa kunufaika na Mpango hup wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser.
…………………………….
Shear Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua
vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!
Uzinduzi
huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kwenye Ukumbi wa Diamond
Jubilee VIP Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa
kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua
kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi.
Mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu atakuwa
ni Balozi Mwanaidi Majaar.
Shear
Illusions, imeweza kutambulisha urembo na muonekano wa mwanamke wa kitanzania
kwa Zaidi ya miaka kumi. Wamebaisha urembo kuanzia kujipodoa, nywele, vipodozi
na vito hadi blog na jarida inayoelezea masuala ya urembo. Baada ya kuuza
bidhaa mbali mbali ya urembo toka nchi mbali mbali, Shear Illusions inazindua
rasmi bidhaa yake ya LuvTouch Manjano.
LuvTouch
Manjano ni maalum kwa ajili ya kumpendezesha mwanamke wa kitanzania. Kuna aina
kumi ya vipodozi msingi kuanzia Mwanzi na Mpodo hadi kahawa na ardhi. Bidhaa
hizi zimezingatia hali ya hewa ya joto. Vipodozi hivi vinalengo la kuongeza
muonekano wako kwa hali yoyote.
Shear Illusions inazishukuru kampuni zifuatazo waliojitokeza kusaidia hafla hii ya kuwawezesha
wanawake; NSSF, TCRA, Clouds Media, Maxcom, A1 Outdoor, Mr. Price, Cassandra
Lingerie, Amina Design, Maznat Bridal, Advertising Dar, Beauty Point, Hugo
Domingo, I-View Media, FAIDIKA, Benchmark Productions, Fasta Fasta, TENSHI,
Jardin Modeling Agency na mashirika mbali mbali hapa Dar es Salaam.

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA NNE WA MABALOZI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mhe. Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo “Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025″
.
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)
Wajumbe wengine wakiwemo Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani.)
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine aliwakumbusha Mabalozi  kuwathamini Watanzania waishio nje ya nchi, kuendelea kusaidia upatikanaji wa misaada ya maendeleo, masoko ya bidhaa za Tanzania, wawekezaji na teknolojia bora. 
Mhe. Rais Kikwete akiteta jambo na Waziri Membe kabla ya kuwahutubia Mabalozi.
Waziri Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula huku Balozi Sefue akisikiliza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Sekretarieti ya Mkutano wa Nne wa Mabalozi. 
Mhe. Rais Kikwete akiongozana na Balozi Mulamula kuelekea eneo la kupata picha ya pamoja.
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na Waziri Membe, Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Balozi Sefue,  Balozi Mulamula, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba Yahya, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mhe. Mussa  Zungu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wote.
Mhe. Rais Kikwete na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

MUSWADA WA VYOMBO VYA HABARI; MOAT YAUNDA KIKOSI KAZI KUONANA NA KAMATI YA BUNGE YA SHERIA NA KATIBA

$
0
0

Menyekiti wa chamacha wamiliki wa vyombo vya habari nchini, MOAT, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, (kushoto), akijadili jambo na Mkurugenzi wa New Habari 2006 Limited, Rostam Aziz, walipokutana kwenye kikao cha MOAT kujipanga na kujadili namna ya kukabiliana na mpango wa serikali wa kuwasilisha muswada wa habari kwa mara ya pili. Mkutano huo ulifanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na umeazimia kuunda timu ya watu watatu ambao watasafiri kwenda Dodoma, ili kukutana na kamati ya bunge ya katiba na sheria ili kuitaka kamati hiyo kuzuia serikali kuwasilisha muswada huo kwa mara ya pili. Duru za habari zinaeleza kuwa Muswada huo pamoja na mambo mengine, utalazimisha vituo vya runing vya kibinafsi, kujiunga na televisheni yha taifa (TBC) kwa taarifa ya habari ya saa mbili usiku (2;00), hatua ambayo inapingwa vikali na wamiliki wa vyombo binafsi ambao wanasema ni uonevu katika ushindani huru hususan ikizingatiwa TBC ambayo ni televisheni ya Watanzania wote kupitia kodi wanazolipa, nayo "inagombea" matangazo ya biashara kama vyombo binafsi

Dkt. Mengi, Tido Muhando, kutoka Azam TV, (katikati) na mkurugenzi wa Mwanachi Communications Limited, Francis Nanai

Kutoka kushoto, Rostam Aziz, Dkt. Mengi, Godfrey Mpandimizi, mwanasheria kutoka LHRC, na Mkurugenzi wa Sahara Media Group, Samwel Nyalla

Mpandimizi, Nyalla, na Mkurugenzi wa Hali Halisi, Saed Kubenea



PICHA ZOTE ZA KHALFAN SAID 

WAZIRI LUKUVI AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TABORA

$
0
0
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali mkoani Tabora leo kuhusiana na masuala yanayohusu sekta ya ardhi mkoani humo katika ukumbni wa mikutano wa Isike. Kulia ni mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya  na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua. 
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora, kuhusiana na mgogoro wa Ardhi unaowakabili wananchi hao ambao unaotokana na Manisapaa kutowalipa fidia ya maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya akijadiliana jambo wakati Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvu alipotembelea eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora kusikiliza matatizo ya Ardhi yanayo wakabili wananchi wa eneo hilo leo.  

Picha/Clarence Nanyaro

Article 2

$
0
0

SERIKALI YAMKARIBISHA MWAKILISHI MKAZI MPYA WA JICA NCHINI


 Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kushoto) na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kulia) wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga  Bw. Tomonari Shinya iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo .
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kulia) na aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (wa pili kutoka kulia) katika hafla fupi ya kumuaga Bw. Shinya iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.Wengine ni Afisa Tawala Msaidizi wa JICA Bw. Nasibu Hamisi (wa tatu kutoka kulia) na Afisa Tawala  wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi. Mwanamridu Jumaa (wa nne kutoka kulia).
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kushoto) alipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akipeana kadi za mawasiliano na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kushoto) wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Katikati ni Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi akishuhudia.
Kaimu katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kulia) katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.
Viewing all 6883 articles
Browse latest View live