Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Andymicheel Grimany akifungua semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyoandaliwa na Bodi ya chakula na Dawa iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula wakifuatilia mada zilizowakilishwa kwenye semina hiyo.
Meneja wa Kiwanda cha Maziwa cha Azam Zanzibar Kirtikumar Dave akichangia katika semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyoandaliwa na Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Mkuu wa Idara ya Huduma za Maabara Bodi ya chakula, Dawa na Vipodozi Nadir Khamis Hassan akitoa mada katika semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
Mrajisi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othman Simai akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuala yaliyoulizwa katika semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni, (kulia) Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andymicheel Grimany.
Mshiriki wa semina ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni Saleh Mohd Haji akitoa amchango wake.
Afisa Mipango Idara ya Sera na Utafiti katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi Omara Ali Omar akitoa mada ya Usalama wa chakula katika uzalishaji kwa upande wa Mifugo katika Semina ya siku moja ya ushajishaji juu ya usalama wa chakula iliyoandaliwa na Bodi ya chakula na Dawa Zanzibar iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani.
……………………………………………………………………..
Na Fatma Kassim
MWAKILISHI wa Shirika la afya ulimwenguni WHO Zanzibar Dk Andymicheel Grimany amesema kuwa maradhi mengi yanayotokea kwa binaadamu chanzo chake ni ukosefu wa usalama wa chakula.
Amesema kuwa kunaumuhimu wa kuzingatia uimarishaji wa chakula tokea kikiwa shambani uhifadhi wake hadi kufikia walengwa hakizingatii ubora na usalama wa chakula.
Hayo ameyaeeleza katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya Afya Duniani uliowakusanyisha wadau mbali mbali katika uliofanyika katika Zanzibar Beach Resort ambapo ujumbe wa mwaka huu ni ubora wa usalama wa chakula.
Alisema kuwa chanzo kikubwa cha maradhi yanayotokana na chakula ni pamoja na Ebola iliyotokea katika nchi za Afrika Magharibi pamoja na miripuko ya maradhi mabali mbali yanayotokea hapa nchini ikiwemo maradhi ya kuharisha.
Alifahamisha kuwa hivi sasa ulimwenguni kote kunaongozeko kubwa la matatizo yanayotokana na ukosefu wa ungalizi mzuri wa vyakula vinayotokana na kilimo, Mifugo na hata katika utaarishaji wake na kusababisha maradhi kwa watumiaji.
Kwa upande wa Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar Dk Burhan Othman Simai amesema kuwa ni vyema wafanyabiashara hapa nchini kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa ili kupunguza ongezeko la matatizo ya kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.
Alisema hivi sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uekezaji wa bidhaa ya mifugo zikiwemo minofu ya kuku ambao baadhi yao hawafati taratibu za uuzaji kwa kuwahifadhi kwenye mafriji na badala yake baadhi yao husambaza kwa kutumia baskeli jambo ambalo linahatarisha afya za wananchi
Alifahamisha kuwa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi itaendelea kufanya uchunguzi pamoja na kudhibiti bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya mwanadamu sambamba na kuzitaka taasisi zote pamoja na wananchi nchini kujenga ushirikiano kwa lengo la kudhibiti bidhaa zisizofaa.
Wakitoa mada walufunzi mbali mbali wa mkutano huo walisema kuwa kunachangamoto mbali mbali zinaikabili Bodi hiyo ikiwemo Zanzibar kugeuzwa jaa la bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya mwanadamu, ongezeko wa ghala zisizosajiliwa pamoja na uelewa mdogo wa jamii juu ya kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.
Walisema ni jukumu la wafanyabiashara wa chakula kujua sheria mbali mbali zinazosimamia masuala ya chakula sambamba na kutambua kuwa jukumu la usalama wa chakula ni lao.
Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi ni chombo halali kilicho chini ya Wizara ya Afya na kina mamlaka ya udhibiti wa ubora wa usalama wa Chakula Dawa na Vipodozi pamoja na vifaa Tiba.
Tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo mwaka 2007 zaidi ya tani 1000 zimeangamizwa na zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa ya chakula hutegemewa kutoka nje ya nchi.