Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwakaribisha wageni katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi kwa waajiriwa wapya Leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mafunzo hayo na kuwataka washiriki kushiriki kikamilifu kwenye kipindi cha mafunzo ili waweze kuwa na mbinu thabiti za ukusanyaji kodi kwa maslahi ya Taifa.
Naibu Mkurugenzi kitengo cha Rasilimali Watu Bw. Victor Kimaro akiwaeleza washiriki wa Mafunzo namna mchakato ulivyofanyika na kuwataka kuthibitisha ubora wao katika kipindi chote cha mafunzo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Rished BADE akiongea na washiriki wa Mafunzo ya ukusanyaji kodi na kuwataka kufanya kazi kama watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na kutumia fursa hiyo kujiimarisha kiutendaji kabla ya kuanza kazi rasmi ya ukusanyaji kodi inayohitaji uadilifu na ueledi wa hali ya juu katika kuitekeleza, wakati wa hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akikata utepe kwenye boksi lililokuwa na Mtaala utakaotumia katika mafunzo hayo wakati wa ufunguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo