Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu na mkewe Mariam Mtemvu na Binti yao Sitti Mtevu -kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wao kutoka vyuo vikuu viwili vya Marekiani vya State University of New York na University of Buffalo, baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, jana kuanza ziara yao ya siku mbili katika jimbo hilo, kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya kijamii na maendeleo. Kulia ni Mkuu wa Msafara huo Mtanzania, Profesa Dan Nyaronga wa Chuo Kikuu cha Buffalo nchini Marekani.
Mtemvu akiwa na mdau wa maendeleo katika jimbo loa Temeke, Fiona Barretto wakati wa mapokezi ya ugeni huo kwenda wa mkuu wa wilaya ya Temeke
Profesa Dan akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Temeke, baada ya ujumbe huo kukutana na mkuu huyo wa wilaya, Sophia Mjema, wa pili kushoto,
Mkuu huyo wa wilaya akizungumza
Ugeni huo kutoka Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Temeke jana
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Photidas Kagimbo akisalimiana na Binti wa Mtemvu, Siti Mtemvu wakati msafara ulipoingia ofisini kwa mkurugenzi huyo jana
Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja ana viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
Wanahisa wa Mfuko wa wa Kupambana na Umasikini Temeke -TFP, wakiulaki ugeni wa Mtemvu na Wamarekani hao ulipowasili kwenye Ofisi za TFP jana
Mtemvu akizungumza na wadau wa PFT
Profesa Dan Nyaronga akizungumza na wadau wa mfuko huo wa PFT
Binti wa Mtemvu Sitti akisalimia wanachama wa mfuko huo
Mtemvu na ugeni wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Mfuko wa PFT baada ya mazungumzo ya kubadilishana uzoefu wa anamna ya kuondoa aumasikini katika jamii
Mkurugenzi wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, akiwa na baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vikuu hivyo ya Marekani ambao ni miongozi mwa waliokuwa katika ugeni huo wa Mtemvu, hapa ilikuwa kwenye ofisi za PFT.
Mbunge wa Temeke, Mtemvu akipata chakula cha mchana na ugeni wake katika jengo la Quality Centre