![]() |
Waandisi wa habari wakifuatilia mkutano huo |
↧
JIJI LA MWANZA LAFIKIWA NA HUDUMA ZA INTANETI YA KASI YA TIGO 4G LTE
↧
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AKUTANA NA MKURUGENZI WA RADIO FRANCE INTERNATIONALE
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akimkaribisha Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie ofisini kwake alipomtembelea kwa ajili ya kufahamiana na kuboresha mahusiano yaliyopo kwa miaka saba sasa.Ujumbe kutoka Radio France International (RFI) wakifurahia jambo wakati wa kikao na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(Hayupo pichani).Mkurugenzi wa Radio France Internationale (RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura kuhusu msaada ambao wameipa shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) ili kusaidia katika kufikisha matangazo yake mbali Zaidi.Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(kulia) akimpa zawadi ya kahawa kutoka Tanzania Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) baada ya mazungumzo mafupi ofisini kwa Naibu Waziri uyo kuhusu kuimarisha mahusiano baina ya nchi izi mbili katika masuala ya Habari kati ya TBC na RFI.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akimkaribisha Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie ofisini kwake alipomtembelea kwa ajili ya kufahamiana na kuboresha mahusiano yaliyopo kwa miaka saba sasa.
Ujumbe kutoka Radio France International (RFI) wakifurahia jambo wakati wa kikao na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(Hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Radio France Internationale (RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura kuhusu msaada ambao wameipa shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) ili kusaidia katika kufikisha matangazo yake mbali Zaidi.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(kulia) akimpa zawadi ya kahawa kutoka Tanzania Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) baada ya mazungumzo mafupi ofisini kwa Naibu Waziri uyo kuhusu kuimarisha mahusiano baina ya nchi izi mbili katika masuala ya Habari kati ya TBC na RFI.
↧
↧
WAZIRI MKUU AWAHAKIKISHIA FURSA ZA UWEKEZAJI WA VIETNAM
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewahakikishia wawekezaji kutoka Vietnam kuwepo kwa fursa za uwekezaji nchini.
Majaliwa ameyasema hayo jana katika kongamano la ujumbe wa Rais wa Vietnam Mheshimiwa Troung Tan Sang pamoja na wadau wa uwekezaji kutoka nchini humo ambapo wanatarajia kufanya ziara ya siku nne nchini wakitazamia fursa za uwekezaji nchini.
“Nchi yetu inamazingira mazuri ya uwekezaji, usalama wakutosha na pia kuna uhahika wa soko kwani ipo mikataba ya kikanda ya kukuza masoko katika nchi wanachama kama EAC na SADC kwani katika nchi hizo kuna watu zaidi ya milioni 300”, alisema Majaliwa.
Akiendelea kuzungumza na wawekezaji hao Waziri Mkuu alisema serikali ya Tanzania imekuwa ikiboresha Mazingira ya uwekezaji nchini na hiyo imechangia ongezeko la wawekezaji.
Mbali na hayo Majaliwa alisema serikali imekuwa ikiboresha sheria na kuimarisha ushirikishwaji wa wadau wa sekta binafsi lengo likiwa ni kuchochea mazingiraya uwekezaji ikiwa ni kuimarisha uchumi wa taifa pamoja na kukuza kipato cha kila mtanzania.
Hata hivyo Waziri Mkuu aliipongeza Kampuni ya VIETTEL Tanzania Ltd kutoka Vietnam ambayo imewekeza katika Sekta ya Mawasiliano kwani imewasaidia watanzania wengi wa vijijini kupata mawasiliano.
↧
RAIS WA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNAM TRUONG TAN SANG ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CCM MTAA WA LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, jana. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya faragha ofisini kwake na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, jana. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini
Waziri wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga akizungumza na Katibu wa NEC anayeshughulikia Uchumi na Fedha wa CCM, Zakiah Megji wakati wa mazungumzo ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na mgeni wake, Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.
Katibu wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akiwa na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatibu wakati wa mazungumzo hayo ya Kikwete na Rais wa Vietnam. Kulia Ni Kaim Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Shaka Hamidu Shaka
Viongozi na Maofisa wa CCM wakiwa kwenye mazungumzo hayo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, jana. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, jana. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, jana. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga na kulia ni Dk. Asha-Rose Migiro.
Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo hayo
↧
SERIKALI KUUNDA MAMLAKA KUU YA MAPATO YA TAIFA

………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi, MAELEZO
Serikali ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuweza kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka hiyo.
“ Napenda kuwambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano inawajali watu wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda Mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika Halmashauri zetu”Alisema Kidata.
Kamishna Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo imechaguliwa na wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika jambo lolote lile hivyo basi kwa sasaserikali ipo katika mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya.
Kamishna huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo zimekuwa kero na hazina tija. Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo hayatokani na kodi toka katika wizara, mashirika,tasisi za serikalina Halmashauri zote nchini.
↧
↧
RAIS WA VIETNAM ATEMBELEA KAMPUNI YA SIMU YA HALOTEL JIJINI DAR ES SALAAM
Rais Truong Tang San akizindua Sanamu ya kiongozi wa zamani wa Vietnam iliyopo kwenye Kampuni ya Simu ya Halotel.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tang San akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Simu za mikononi kutoka nchini Vietnam ya Halotel inayofanya kazi hapa nchini Tanzania. Kampuni hiyo inatoa huduma ya simu Vijijini kwa gharama nafuu. Rais Truong Tang San anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku nne leo na kuelekea nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara nchini humo.
Viongozi mbalimbali walioambatana na Rais Truong Tang San, wakiwa pamoja na Balozi wa Vietnam, Mhe. Vothanh Nam (katikati) wakisikiliza kwa makini mazungumzo aliyokuwa yakiendelea kati ya Rais Tang San (hayupo pichani) na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel
Viongozi wa Halotel na Viongozi walioambatana na Rais Tang San (hayupo pichani) wakishangilia wakati uzinduzi ukiendelea
Rais Truong Tang San akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel.
Picha na Reginald Philip
↧
ZIARA YA KUSHITUKIZA YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) NA HAYA NDIO ALIYOAMUA YATENDEKE
Rais Dkt Magufuli akizungumza na Uongozi wa juuu wa Benki Kuu
↧
WAZIRI WA MAJI AIAGIZA BODI YA DAWASCO KUWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WAKE KWA TUHUMA MBALIMBALI
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (katikati) akiongozana na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) , Meja General (mstaafu), Samuel Kitundu (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Cyprian Luhemeja , wakati Waziri huyo alipoitembelea Dawasco leo na na kisha kutangaza watumishi tisa ambao ameiagiza bodi kuwasimamisha kazi kupisha uchunguzi dhidi yao kufuatia tuhuma mbalimbali. Mhandisi Lwenge alitembelea leo.
WATUMISHI AMBAO WAZIRI AMEAGIZA BODI IWASIMAMISHE KAZI NI:-
Meneja Rasilimali Watu, Mvano Mandawa, Meneja Ufuatiliaji na Tathmini, Reinary Kapera, Teresia Mlengu, Emmanuel Guluba, Peter Chacha, Fred Mapunda, Reginald Kessy, Jumanne Ngelela na Bernard Nkenda.
Aidha Waziri Lwenge aliagiza pia kuchunguzwa kwa CEO wa zamani Jackson Midala.
Miongoni mwa tuhuma zao ni pamoja na kufanya maunganisho ya maji yasiyofuata utaratibu kwa kampuni ya STRABAG inayotekeleza mradi wa mabasi yaendayo kasi na kusababisha kulikosesha shirika mapato yenye thamani ya sh Bilioni 2.8 (2,887,577,134/=).
Mameneja wa Dawasco wakiwa katika mkutano huo.Baadhi yao walisimamisha kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazo wakabili.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (kulia) akizungumza na bodi pamoja na menejimenti ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) wakati Waziri huyo alipotembelea makao makuu ya shirika hilo Dar es Salaam jana na kuiagiza bodi kusimamisha kazi watumishi tisa.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (aliyesimama) akizungumza na bodi pamoja na menejimenti ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam (DAWASCO) wakati Waziri huyo alipotembelea makao makuu ya shirika hilo Dar es Salaam jana na kuiagiza bodi kusimamisha kazi watumishi tisa.
↧
SPIKA AKUTANA NA WABUNGE KUTOKA UJERUMANI
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimkabidhi zawadi Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen. Anayeshuhudia kulia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson.Wabunge hao walimtembelea Spika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea zawadi Kutoka kwa Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen. Wabunge hao walimtembelea Spika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Kiongozi wa Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen (wa pili kushoto) waliomtembelea Spika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na wa Kwanza kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Bw. Egon Kochake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiagana na Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen waliomtembelea Spika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia wa kwanza kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na wa Kwanza kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Bw. Egon Kochake.
Spika wa Bunge (wa pili kutoka kulia kwa walio kaa) akiwa katika picha ya Pamoja na Wabunge la Ujerumani waliomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson, Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Jens Koeppen na Balozi wa Ujerumani nchini Bw. Egon Kochake.(Picha na Ofisi ya Bunge)
↧
↧
SEMINA YA KUWANOA WADAU WA SEKTA YA SANAA, YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Kwa mara ya kwanza, wadau wa Sanaa nchini wamepata fursa ya kukutana
na Makampuni, Mashirika na Vyombo mbalimbali katika mafunzo
yaliyofanyika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. Semina hii
iliongozwa na Maria Sarungi Tsehai, ambaye ni mdau mkubwa katika sekta
hii
na Makampuni, Mashirika na Vyombo mbalimbali katika mafunzo
yaliyofanyika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. Semina hii
iliongozwa na Maria Sarungi Tsehai, ambaye ni mdau mkubwa katika sekta
hii
Mafunzo hayo yalifanywa na wataalam kutoka sekta mbalimbali kama
Nyumba, Urembo, Saikolojia, Sanaa na Wasanii n.k
![]()
Nyumba, Urembo, Saikolojia, Sanaa na Wasanii n.k

Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba, Arden Kitomari,akitoa
mafunzo ya namna ya kuwekeza katika Sekta ya Nyumba nchini
Tanzania,hususan kupitia miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa
mafunzo ya namna ya kuwekeza katika Sekta ya Nyumba nchini
Tanzania,hususan kupitia miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa
Wadau wa Sanaa pia walipata mafuzo ya Namna ya kubalansi maisha yao ya
Sanaa na yale ya Familia, kutoka kwa mwanasaikolojia maarufu, Aunt
Sadaka Gandi.
Sanaa na yale ya Familia, kutoka kwa mwanasaikolojia maarufu, Aunt
Sadaka Gandi.
Semina hii iliyopewa jina Celebrity Corporate Conference &
Cocktail iliwahusisha pia COSOTA na BASATA ambao ni wasimamizi wakuu
wa kazi za sanaa na taratibu zake
Cocktail iliwahusisha pia COSOTA na BASATA ambao ni wasimamizi wakuu
wa kazi za sanaa na taratibu zake
Ms Doreen Anthony Sinare, CEO wa COSOTA akitoa somo kuhusu usajili wa
kazi, masharti ya kuzingatiwa na Sheria zinazomlinda Msanii
aliyesajiliwa
kazi, masharti ya kuzingatiwa na Sheria zinazomlinda Msanii
aliyesajiliwa
Sekta lengwa katika semina hii ni wadau kutoka Filamu, Muziki, Urembo,
Habari, na Wajasiriamali mashughuri
Habari, na Wajasiriamali mashughuri
Bwana Aristides kutoka BASATA aliwaelekeza wadau kuhusu Taratibu mpya
za kujisajili na chombo hiki, pamoja na faida zake.
za kujisajili na chombo hiki, pamoja na faida zake.
Je, Unafahamu namna ya kuifanya Talanta yako kuwa Biashara? Hii ndio
ilikuwa mada iliyoongozwa na Mjasiriamali mashughuri, Shekha Nasser wa
Shear Illusions
ilikuwa mada iliyoongozwa na Mjasiriamali mashughuri, Shekha Nasser wa
Shear Illusions
Baada ya mada zote kukamilika, wadau walipata fursa ya kubadilishana
mawazo na kujadili walichojifunza, kwa kushiriki Tafrija mchapalo
iliyoandaliwa
mawazo na kujadili walichojifunza, kwa kushiriki Tafrija mchapalo
iliyoandaliwa
Huu ukawa wakati muafaka wa wasanii kuuliza maswali na kutoa dukuduku
zao kwa Makampuni, Mashirika na vyombo vinavyohusika na Sanaa na
Wasanii. Mrembo na Mjasiriamali Jokate Mwegelo akiteta jambo na afisa
kutoka BASATA
zao kwa Makampuni, Mashirika na vyombo vinavyohusika na Sanaa na
Wasanii. Mrembo na Mjasiriamali Jokate Mwegelo akiteta jambo na afisa
kutoka BASATA
Mwanahabari Maimuna Kubegeya hakuwa nyuma kuuliza maswali na
kufahamiana na CEO wa COSOTA, Ms Doreen Anthony Sinare
kufahamiana na CEO wa COSOTA, Ms Doreen Anthony Sinare
MwanaBlog maarufu John Bukuku akifurahia jambo na Meneja Masoko wa
NHC, Arden Kitomari
NHC, Arden Kitomari
Antu Mandoza akisisitiza jambo
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Popular Links ambao ndio waandaaji
wa Semina hii akiwa katika pozi na Mkurugenzi Ruge Mutahaba kutoka
Clouds Media
wa Semina hii akiwa katika pozi na Mkurugenzi Ruge Mutahaba kutoka
Clouds Media
Warembo katika picha ya pamoja
Wasanii wa kutengeneza muonekano kutoka LuvTouch Manjano ya Shear
Illusions, wakiwaonesha baadhi ya wageni, namna ya kupaka makeup
Illusions, wakiwaonesha baadhi ya wageni, namna ya kupaka makeup
Mariam Ndabagenga, Mkurugenzi wa Popular Links akitoa neno la Shukran
kwa wageni waalikwa wote na kuwakaribisha kwenye awamu ya pili ya
Semina hii itakayofanyika mwezi Oktoba.
kwa wageni waalikwa wote na kuwakaribisha kwenye awamu ya pili ya
Semina hii itakayofanyika mwezi Oktoba.
Semina hii ya Celebrity Corporate Conference & Cocktail
imeandaliwa na Kampuni ya Popular Links kwa udhamini wa Heineken, The
Guardian, Nipashe, Leteraha, Hyatt Regency hotel, Ndovu Special Malt,
Cocacola, NHC, COSOTA, Jamii Media, BASATA, Shear Illusions, Clouds
Media na Slide Visuals.
imeandaliwa na Kampuni ya Popular Links kwa udhamini wa Heineken, The
Guardian, Nipashe, Leteraha, Hyatt Regency hotel, Ndovu Special Malt,
Cocacola, NHC, COSOTA, Jamii Media, BASATA, Shear Illusions, Clouds
Media na Slide Visuals.
↧
OFIS YA BUNGE YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ZA KUKAMATWA KWA MH.ESTER BULAYA
↧
MWANAMAPINDUZI YA ZANZIBAR, MZEE IBRAHIM AMAN AZIKWA LEO KATIKA KIJIJI CHA KWALE
Viongozi wa Kitaifa waliohudhuria mazishi ya Marehemu Mzee Ibrahim Amaan wakikamilisha hitma ya kumuombea kiongozi huyo Mwanamapinduzi ya Zanzibar huko Kijijini kwake Nymanzi Wilaya ya Magharibi “B”.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakisubiri ibada ya sala ya Maiti kwa ajili ya kumuombea Dua zee Ibrahim Amaan kwenye Msikiti wa Ijumaa aliokuwa mioingoni mwa watu waliouanzisha Kijijini kwake Nyamanzi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiongozwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Ngwali walimsalia Mzee Ibrahim kwenye msikiti wa Kijiji hicho.
Picha na – OMPR – ZNZ.
MWANAMAPINDUZI ya Zanzibar ya Mwaka 1964 ambae pia ni mwanzilishi wa Chama cha Mapinduzi Mzee Ibrahim Aman aliyefariki Dunia jana mchana amezikwa leo Kijijini kwake Nyamanzi Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.
Mzee Ibrahim aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya baridi pamoja na Uzee alilazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja akipatiwa matibabu kutokana na afya yake.
Mamia ya Wananchi, waumini wa dini pamoja na Viongozi wa Kitaifa walihudhuria mazishi hayo yaliyojumuisha pia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu wa SMT Dr. Mohammed Gharib Bilal.
Mzee Ibrahim Amaan alizaliwa mwaka 1930 katika Kijiji cha Nyamazi na alipofikia umri wa kusoma Wazazi wake wakampelekea kupata elimu ya Quran iliyoambatana na ile ya Dunia katika ngazi ya Msingi.
Wakati wa ujana wake marehemu Mzee Ibrahim Amaan alijishughulisha na kazi za ukulima na uvuvi ili kujipatia kipato kilichomuezesha kuanza kujitegemea katika maisha yake ya kawaida.
Mwaka 1957 Mzee Ibrahim alijiunga na Chama cha Afro Shirazy Party ambapo kutokana na uzalendo pamoja na umakini wake alifanikiwa kuwa muanzilishi wa Umoja wa Vijana wa ASP Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika Uhai wake marehemu Mzee Ibrahim aliwahi kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Chama cha Afro Shirazy Party na kushiriki kuuangusha Utawala wa kisultani Mwaka 1964 na baadaye kujiunga na Jeshi la Ukombozi la Unguja akifikia cheo cha Kanal.
Akisoma Risala ya wakfu wa Marehemu Mzee Ibrahim Makungu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dr. Miwinyihaji Makame alisema Chama cha Mapinduzi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zimepokea kwa masikitiko kifo cha Mwanamapinduzi huyo aliyejitolea muda wake wa maisha kulitumikia Taifa hili.
Dr. Mwinyihaji alisema Ushujaa wa Mzee Ibrahim ulimpelekea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kumtunukia Nishani ya Ushujaa wa Mapinduzi kwenye sherehe hizo za mwaka 2014.
Alisema Mzee Ibrahim miongoni mwa majukumu yake kwa Taifa aliwahi pia kuwa Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu wa CCM Idara ya Umma Afisi kuu ya CCM Kisiwandui pamoja na Mwenyekiti wa kazi za njia na nnguvu za umeme.
Dr. Mwinyihaji alifafanua zaidi kwamba Mzee Ibrahim alikuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee la Chama cha Mapinduzi wadhifa ambao aliendelea nao hadi mauti yalipomfika.
Mzee Ibrahim Amaan aliyezaliwa mwaka 1930 na kufikisha umri wa Miaka 86 ameacha kizuka Mmoja na Watoto Thalathini.
Yarabi aiweke roho ya Marehemu Mzee Ibrahim Amaan mahali pema Peponi amin.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
12/3/2016
↧
RAIS DKT. MAGUFULI ATEUA WAKUU WAPYA WA MIKOA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.
Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1.Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
2.Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita.
3.Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
4.Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
5.Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
6.Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
7.Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
8.Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
9.Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
10. Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa wa Singida.
11. Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
12. Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
13. Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
14.Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa Mkoa Dodoma.
15.Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
16.Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
17.Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa Mbeya.
18.Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa Mwanza.
19.Mh. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
20.Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
21.Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
22.Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
23.Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
24.Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
25.Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
26.Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Machi, 2016
↧
↧
Rais Magufuli awathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za serikali.
Waliothibitishwa ni Bw. Alphayo Kidata, aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambaye anakuwa Kamishna Mkuu wa TRA, na Bw. Valentino Mlowola aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambaye anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU).
Watendaji hawa wamethibitishwa kuanzia leo tarehe 13 Machi, 2016
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
13 Machi, 2016
↧
SERIKALI KUNUNUA MELI MPYA - WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanza kukusanya fedha kwa ajili ya kununua meli mpya kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye Ziwa Victoria.
“Rais John Pombe Magufuli kasema ununuzi wa meli mpya uko pale pale. Tutanunua meli ya kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria kama ambavyo aliahidi wakati wa kampeni,” alisema huku akishangiliwa.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Machi 13, 2016) wakati akitoa maelekezo baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Kagera ambako amewasili leo kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukagua masuala ya wakimbizi pamoja na mwenendo wa ranchi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na jinsi zinavyotumika.
Mbali ya ununuzi wa meli hiyo, Waziri Mkuu alisema Serikali pia imejipanga kununua ndege mbili ili kuimarisha usafiri wa anga hapa nchini. “Tuna dhamira ya kununua ndege walau mbili kwa ajili ya shirika letu la ndege la ATC. Tumelazimika kuwaomba Watanzania wenzetu warudi nyumbani ili kusaidia kuendesha shirika letu,” alisema.
Waziri Mkuu alisema suala hilo limeshafika mbali na utekelezaji wake hautachukua muda mrefu kuanzia sasa.
Alitumia fursa hiyo kuwaarifu wana Kagera kwamba hivi karibuni Serikali itaanza mradi wa kujenga bomba la kusafirisha mafuta ambalo litapita kwenye mkoa huo na hivyo ktoa ajira kwa wakazi wake. “Bomba litaanzia Tanga, kupitia Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Simiyu, Geita, Kagera hadi Uganda. Na humu njiani litakuwa na vituo vya kusukumia mafuta, kwa hiyo tuna uhakika wa kupata ajira kwa ajili ya watu wetu,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, MACHI 13, 2016.
↧
WARSHA YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI NA UDHIBITI WA NDANI KWA AJILI YA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU MAKATIBU WAKUU
Makatibu Wakuu kutoka Wizara tofauti wakihudhuria mafunzo ya ‘Warsha ya Usimamizi wa Vihatarishi na Udhibiti wa Ndani’ (Risk Management and Internal Control Systems Workshop) yaliyoandaliwa kwa ajili ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu na Taasisi ya UONGOZI tarehe 8 mpaka 9 Machi 2016 Dar Es Salaam.
Mwezeshaji akiongoza kipindi cha maswali na majibu kwa Makatibu Wakuu baada ya kuwasilisha mada yake.
Baadhi ya Makatibu Wakuu wakishiriki kwenye mijadala ya mafunzo hayo kwa kusikiliza kutoka kwa Wawezeshaji tofauti.
↧
MH. PAUL MAKONDA AMSHUKURU MUNGU KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA KAZINI
Mhe.Paul Makonda siku ya leo (jana) alikuwa anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Walaya Kinondoni,asubuhi ya leo katika Ibada Kanisani Living Water Center Ministry Kawe alipolelewa kiroho na anapo abudu alikuja kumshukuru Mungu na kutoa sadaka ya shukrani kwa hatua ambayo amefika.
Katika Ibada hiyo Mh Paul Makonda aliongozana na Mkee wake alipopewa kuzungumza alisema anamshukuru Mungu kwa kutimiza mwaka tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni,alisema haikuwa raisi kwake ila Mungu amemuwezesha,akaongeza kwa kusema "usishindwe kufanya mambo ya kimaendeleo kwa changamoto za kimazingira au chochote kama kwake ambavyo imekuwa ikionekana".
Mapema akimkaribisha kuzungumza Mhe.Paul Makonda Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi alikuwa anaelezea jinsi ambavyo amemlea kiroho Mh.Makonda hata kabla ya kuingia kuwa mtumishi wa serikali jinsi alivyokuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali hivyo kinachofanyika leo sio kipya kwake.
Baada ya Ibada hiyo ya shukrani Bwana akatenda zaidi kwa kumfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
Hongera Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es saam
Maombi yalifanyika kwake na mke wake ili Mungu amtangulie katika utumishi wake serikalini .
Apostle Onesmo Ndegi,Mke wake Lilian Ndegi na Mch. Peace Matovu wakifanya maombi kwa Mh. Makonda .
↧
↧
AIRTEL FURSA YAINGIA DODOMA YATOA MSAADA WA SHS MILIONI 9
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (katikati), akijaribisha moja ya mashine mashine walizomkabidhi kijana Fikiri Chinji (kushoto), anayejishughulisha na ufundi seremala, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii. Anayeshuhudia (kulia) ni Meneja mauzo manispaa ya Dododma Hendrick Bruno.
Kijana Fikiri Chinji anayejishughulisha na ufundi seremala, akionyesha jinsi mashine yake mpya aliyokabidhiwa na Airtel Tanzania, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, inavyofanyakazi katika hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa Ng’ong’o na manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii. Anayeshuhudia ni Meneja masoko manispaa ya Dodoma Saidimu Ngalesoni (kulia) akifuatiwa na Meneja mauzo manispaa ya Dodoma, Hendrick Bruno (wa pili kulia)
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa nne kulia), akimkabidhi kijana Fikiri Chinji (wa tano kushoto), anayejishughulisha na ufundi seremala, msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi na kujengewa karakana mpya kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni wanakijiji wa Ng’ong’ona na wafanyakazi wa Airtel waliofika kushuhudia tukio hilo.
Wanakijiji wa Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma wakiangalia banda alilokabidhiwa Kijana Fikiri Chinji (hayupo pichani) anayejishughulisha na ufundi seremala, pamoja na msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, mwishoni mwa wiki hii.
↧
GSM FOUNDATION YAIPIGA JEKI TIMU YA TAIFA YA RIADHA ILIYOKO KAMBINI WEST KILIMANJARO



↧
RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA KAMPUNI YA TOTAL AFRIKA MASHARIKI JAVIER RIELO ALIYEAMBATANA NA UJUMBE WAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wajumbe walioambatana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.
↧
N