↧
WAZIRI MKUU MAJALIWA AMPA POLE RAIS MSTAAFU.
↧
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, WAKUU WA WILAYA YA ILALA NA TEMEKE WATEMBELEA SHULE ZA MSINGI.
Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) na Menejimenti leo iliungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Wakuu wa Wilaya wa Ilala na Temeke kutembelea shule za Msingi za Majimatitu, Mbande na kisongola ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia.
Hii ni katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanapewa elimu ya msingi bure. Wanachama wataendelea kupatiwa utaratibu wa namna ya kushiriki kuchangia juhudi hizi.
Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) na Menejimenti leo iliungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick na Wakuu wa Wilaya wa Ilala, Raimond Mushi na Mkuu wa Wilaya ya Temeke walipotembelea shule za Msingi za Majimatitu, Mbande na kisongola ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia.
↧
↧
UNDP WAFANYA KONGAMANO LA VIJANA, LENGO NI KUWASAIDIA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo, kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam limefanya kongamano la vijana na maendeleo kujadili jinsi vijana wanavyoweza kutumika kusaidia kuleta maendeleo nchini na kubadili mfumo wa vijana katika kufanya maamuzi yaliyo sahihi.
Akizungumzia kongamano hilo limelofanyika siku ambayo UNDP imetiza miaka 50 tangu kuanzishwa, Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini, Amon Manyama alisema kuwa vijana wana nafasi kubwa katika jamii na kama wakitumika vizuri wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo na hivyo kupitia kongamano hilo wanataraji kuwapa mbinu mpya.
Alisema mbali ya kuangala jinsi wanavyoweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo pia wanajadili kwa pamoja ili kuona jinsi gani wanaweza kubadili mfumo wa vijana wa kufanya maamuzi ambao wengi wao wamekuwa wakifanya maamuzi ambayo baadae yanaonekana kutokuwa sahihi.
“Tunafanya kongamano hili na vijana kutoka vyuo mbalimbali ili kuona mustakabali wa vijana wa Tanzania, kuona jinsi gani wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo Tanzania na hata kubadili mfumo wao wa kufanya maamuzi,” alisema Manyama.


Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini na mshereheshaji wa kongamano hilo, Amon Manyama akizungumza katika kongamano la vijana na maendeleo.
Nae Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo alisema vijana wana nafasi kubwa kusaidia uapatikanaji wa maendeleo nchini na wao kama UNDP wamekuwa wakisaidia na serikali ili kuwasaidia vijana kwa kuwapa mbinu ambazo wanaweza kutumia ili kufikia malengo waliyonayo.
Alisema licha ya kuwepo changamoto zilizopo katika sera ya vijana lakini pia vijana wamepoteza udhubutu wa kufanya maamuzi na hivyo kongamano hilo wanaweza kukuza uwezo wao wa kujiamini na kufanya maamuzi ambayo yanakuwa ni sahihi.
“Vijana wanatakiwa kuwa na malengo na kukuza uwezo wa kujiamini … vijana wanaweza kusaidia kupatikana maendeleo Tanzania na wana hamasa ya kusaidia kupatikana maendeleo hivyo wanatakiwa kupewa nafasi katika kufanya maamuzi,” alisema Bi. Dabo.

Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo, kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Sehemu ya vijana kutoka vyuo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo wakati akitoa neno la ufunguzi wa kongamano hilo.
Kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Uchumi, Jehovaness Aikaeli alisema vijana wanaweza kutumiwa kama fursa hasa katika kipindi hiki ambacho kunakuwa na vijana wengi ambao wanatoka vijijini na kukimbilia mijini na hivyo kama wakishirikishwa wanaweza kusaidia kupatikana maendeleo.

Mkuu wa Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jehovaness Aikaeli akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano hilo.
Nae mmoja wa vijana aliyeshiriki katika kongamano hilo, Ncheye Revina alisema mifumo inayotumika sasa nchini inawabana vijana kusaidia kupatikana kwa maendeleo na kama watakuwa wanataka vijana wahusike kikamilifu basi wawatolee vikwazo vinavyowabana kushiriki akitolea mfano katika ajira kwa ajili wengi kutaka wafanyakazi walio na uzoefu mkubwa wa kazi jambo ambalo ni ngumu kupata vijana.

Mmoja wa vijana aliyeshiriki katika kongamano hilo, Ncheye Revina.

Benedict Kikove kutoka Ubalozi wa Japan nchini akiwaelezea vijana fursa zilizopo kwa vijana na changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kongamano la vijana na maendeleo lililoandaliwa na UNDP.

Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akifuatilia kwa makini kongamano la vijana na maendeleo.

Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) nae alikuwa ni miongoni mwa watoa mada katika kongamano hilo.

Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama (wa kwanza kulia) akifuatilia kilichokuwa kikiendelea katika kongamano hilo lililoandaliwa na UNDP.

Fatma Mohamed kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV) akizungumzia changamoto wanazokutana nazo vijana katika kutafuta mafanikio.

Mwakilishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kutoka Zanzibar, Saleh Mubarak akielezea washiriki jinsi serikali inavyowasaidia vijana katika kongamano la vijana na maendeleo.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo ambao ni vijana na wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali nchini lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).



Afisa wa Utawala Bora kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Godfrey Mulisa akielezea jinsi washirika wa maendeleo wanavyotoa fursa kwa vijana na jinsi fursa hizo zinavyoweza kuwasaidia vijana wa Tanzania.

Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem akizungumza wakati wa kongamano hilo.

Pichani juu na chini ni vijana kutoka vyuo mbalimbali nchini wakishiriki kutoa maoni kwenye kongamano hilo.


Makamu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Titus Osundina akitoa neno la hitimisho la kongamano la vijana na maendeleo.
↧
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA UK SPORT
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo na mshauri wa maendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Uk sport Bi.Clare Barell.Kampuni iyo ni mshirika wa Tanzania katika maendeleo ya Michezo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshauri wa maendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Uk sport Bi.Clare Barell(wa pili kushoto) alipomtembelea ofisini kwake.Wengine pichani ni Kaimu mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge(wa pili kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kulia) akizungumza na mshauri wa maendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Uk sport Bi.Clare Barell juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya michezo na kumuomba mwakilishi uyo kuwekeza kupitia kampuni yao katika miundombinu ya michezo hapa nchini.
↧
KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM KUANZA KAZI HIVI KARIBUNI
Rais Dk. John Pombe Magufuli akikagua kivuko cha MV Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Kivuko cha Mv Dar es Salaam maarufu kama kivuko cha Rais Magufuli kipo katika matengenezo ya kawaida na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kama kawaida siku za hivi karibuni.
Akitoa ufafanuzi juu ya madai ya kutelekezwa kwa kivuko cha Mv Dar es Salaam katika maegesho yaliyopo kigamboni Jijini Dar es Salaam ,Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Manase Le-Kujan amesema sio kweli kwamba kivuko hicho cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa bali kimepumzishwa kutokana na matengenezo yaliyohitajika kufanywa katika kivuko hicho ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wasafiri.
“Sio kweli kwamba Kivuko cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa katika maegesho ya Kigamboni bali kimepumzishwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo yake ya kawaida, hii ikiwa ni juhud
i ya kukiwezesha Kivuko hiki kuwa katika ubora unaotakiwa katika kutoa hudumazake”
“Mbali na matengenezo pia kuwepo kwa upepo mkali katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea imetufanya tukipumzishe kwa muda kivuko hicho” Alisema Mhandisi Manase.
Akifafanua zaidi,Mhandisi Manase amesema kuwa wapo katika mchakato wa kukipeleka kivuko hicho kwa ajili ya matengenezo makubwa Mjini Mombasa ili kukiongezea mwendo kasi na uhimili wake ili kiweze kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika usafirishaji kwa kutumia vivuko na kuhuimili mabadiliko ya hali ya hewa.
Aidha amesema hakuna mvutano wa watendaji wakuu TEMESA wala madai yoyote ya kukisimamisha kwa makusudi kivuko hicho bali ni mpango wa TEMESA katika kukiboresha ili kiweze kuhudumia wananch iipasavyo.
Kivuko cha Mv Dar es Salaam hufanya safari zake za kusafirisha abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Bagamoyo ikiwa ni juhudi za serikali za kupunguza tatizo la usafiri wa majini na kwa sasa kimesimama kwa muda kwa ajili ya matengenezoambayo yakikamilika kitaendelea kutoa huduma kama kawaida.
Ufanisi wa kivuko hiki utapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa Bagamoyo, Mbweni, Ununio, Boko, Bunju, Kunduchi na Msasani wanaofanya safari zao kwenda Posta nakurudi sehemu wanakotokea. Na pia kitapunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwani baadhi ya watu wataacha kutumia magari yao binafsi na kupanda kivuko hicho.
↧
↧
WAZIRI MKUU, MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA TANO WA BUNGE LA AFRIKA YA MASHARIKI
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashriki, Kanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga akiapa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki katika Mkutano wa Tano wa Bunge hilo uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim majliwa kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Machi 8, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge Job Ndugai wakiwa katika picha ya pamoja na Spikia wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Daniel Fredrick Kadega (katikati) baada ya kuhutubia Mkutano wa Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Daniel Fredrick Kadega baada ya kuhutubia Mkutano wa Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Shyrose Bhanji baada ya kuhutubia Mkutano wa Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
↧
WAZIRI UMMY MWALIMU AONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI JIJINI DAR ES SALAAM
Waziri wa Afya,Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.![]()
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangalla akitoa maelezo ya ushiriki wa Mbunge wa Njombe Kusini, Edward Mwalongo kwa kupaza sauti katika bunge juu ya mtoto wa kike kupewa dhana ya kujikinga wakati wa hedhi ili aweze kusoma katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi tuzo Mbunge wa Njombe Kusini, Edward Mwalongo kwa kwa kupaza sauti katika bunge juu ya mtoto wa kike kupewa dhana ya kujikinga wakati wa hedhi ili aweze kusoma katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi hundi ya sh.milioni tano, Dereva wa Bodaboda, Sikudhani Daudi zilizotolewa na Benki ya DCB ikiwa na lengo ya kukuza biashara katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Wanawake kutoka Shirika la Nyumba la Taifa wakishiriki katika maandamano ya siku ya wanawake iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Wanawake kutoka Shirika la Nyumba la Taifa wakishiriki katika maandamano ya siku ya wanawake iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Wanawake kutoka Shirika la Nyumba la Taifa wakishiriki katika maandamano ya siku ya wanawake iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Wanawake kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper (TSN) Limited na Standard Printer wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habari Leo na Habarileo Jumapili pamoja na gazeti la Spoti Leo wakishiriki katika maandamano ya siku ya wanawake iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wanawake kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper (TSN) Limited na Standard Printer wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habari Leo na Habarileo Jumapili pamoja na gazeti la Spoti Leo wakishiriki katika maandamano ya siku ya wanawake iliyofanyika jijini Dar es Salaam
.
Wanawake katika vikundi vilivyopata mkopo katoka kwa benki ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na hundi zao jana katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja Biafra .
↧
MKUU WA MKOA WA MTWARA MH. HALIMA DENDEGU AZINDUA RASMI SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2016 KATIKA UWANJA WA MASHUJAA.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akitoa Hotuba yake kwa wakazi wa Mtwara na Kuzindua Rasmi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2016 linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa
la OXFAM Tanzania
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh. Fatma Ally akizungumza na wakazi wa Mtwara,wageni mbalimbali na wadau pia kufungua rasmi sherehe hizo wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani na Uzinduzi wa Shindano la Mama wa Chakula kwa Mwaka 2016
Meneja wa Programu ya Uwazi na Utawala Bora kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Bi. Betty Mlaki akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika Hilo Jane Foster wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani na uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2016
Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoa wa Lindi Renatha Mzinga akizungumzia nafasi ya Mwanamke katika kujenga Taifa wakati wa siku ya Maadhimisho ya Sikukuu ya wanawake Duniani.
Kamishna Msaidizi wa Polisi Tatu Abdallah Mfaume ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es salaam, akizungumzia juu ya Dawati la Jinsia linavyofanya kazi
Mshereheshaji akiendelea na kutoa Utaratibu
Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya Mwasiti akitumbuiza wakati wa Sherehe za Siku ya Mwanamke Duniani
Bi. Jovitha Mlay Kutoka Shirika la Kimatafa la OXFAM Tanzania akizungumza na wakazi wa Mtwara juu ya wanawake na uziduaji
Bw. Mohammed Mapalala kutoka Morogoro anayehusika na Maswala ya Ardhi akizungumzia juu ya Haki ya Ardhi kwa wanawake
Meneja wa Utetezi Kutoka Shirika la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akitoa Maelezo ya kina kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo Msimu huu wa Tano linatarajiwa kuanzi mwezi Septemba na kurushwa katika Runinga ya ITV
Mwanamuziki Vitaris Maembe akitoa Burudani ya Nguvu wakati wa Sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani na Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akitembelea katika Mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani a Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa Mwaka 2016
Mwanamuziki matata wa Miondoko ya Taarabu Jike la Simba Bi. Aisha Mashauzi akitoa Bonge la Burudani wakati wa kilele cha Siku ya wanawake Duniani
Burudani ikiendelea
Mamia ya wakazi wa Mtwara wakiwa katika Sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani na uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka 2016, katika Uwanja wa Mashujaa.
…………………………………………………………………………………………………………………………………………
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la kimataifa la OXFAM limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mh Halima Dendegu na kuwataka washiriki kuuletea ushindi katika Mkoa wao wa Mtwara.
Mh Halima Dendegu alitoa hamasa hiyo katika uzinduzi huo uliokwenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huku akiwataka washiriki ambao ni wanawake wajitahidi kadiri wawezavyo mshindi wa shindano hilo atokee mkoani mtwara.
Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali, Taasisi za Umma, Mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wakazi wa Mkoa wa Mtwara pia Mh. Halima Dendegu alipata nafasi ya kugawa fomu za ushiriki kwa wakina mama watatu wa shindano hilo na kupata nafasi ya kuwaandikisha katika fomu hizo.
Pia katika hatua hiyo mkuu wa mkoa huyo amewaomba wakina mama wajasiriamali kujiokeza kwa wingi katika ushiriki wa shindano hilo ili kuongeza muamko wa shindano hilo na kujiongezea uwezo wa kushinda na kuwataka wanawake wajasiriamali kujaza fomu za ushiriki kwa wingi na bila ya kuogopa.
Sanjali na hatua hiyo mkuu wa mkoa amesema kuwa licha ya kuwepo na harakati za wanawake kujikwamua kiuchumi ambao wengi wao wanaotegemea kilimo kama njia ya kujipatia mazao lakini bado kumekuwepo na changamoto kubwa kwa mwanamke ya kumiliki Ardhi ambapo ametaja kama moja ya changamoto ya ukandamizaji wa kijinsia na kuwataka wanawake kusimama kidete katika kutetea haki hiyo kama moja wapo ya
msingi.
msingi.
Naye Meneja wa Utetezi wa Shirika la Kimataifa la OXFAM, Eluka Kibona alieleza kuwa Shindano la Mama
Shujaa wa Chakula kwa mwaka huu 2016 linatarajiwa kuanzaSeptemba na litakuwa linaoneshwa kupitia kituo cha runingacha ITV.
Shujaa wa Chakula kwa mwaka huu 2016 linatarajiwa kuanzaSeptemba na litakuwa linaoneshwa kupitia kituo cha runingacha ITV.
Meneja wa mradi kutokea shirika la OXFAM, Bi. Jovitha Mlay amewatoa hofu washiriki watakaoshiriki katika
shindano hilo kwa kuwataka kujitokeza kwa wingi na hasa ikiwa kama bahati kwa shindano hilo la Mama shujaa wa chakula kuzinduliwa mkoani mtwara na hivyo kuwataka wakina mama wajasiriamali wakubwa na wadogo kujitokeza kwa kuchukua fomu za ushiriki kwa wingi.
shindano hilo kwa kuwataka kujitokeza kwa wingi na hasa ikiwa kama bahati kwa shindano hilo la Mama shujaa wa chakula kuzinduliwa mkoani mtwara na hivyo kuwataka wakina mama wajasiriamali wakubwa na wadogo kujitokeza kwa kuchukua fomu za ushiriki kwa wingi.
Aidha baadhi ya wanawake wadau wa OXFAM kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wametumia nafasi hiyo
zaidi kwa kuwataka wajasiriamali wakina mama wa Mtwara kutumia fursa mbalimbali ili kuongeza kipato chao na kuacha suala la utegemezi kotoka kwa waume zao. Uzinduzi wa Mama shujaa wa chakula ulihudhuriwa na wasanii mbalimbaliwaliotoa burudani kwa wakazi waliofika katika uzinduzi wa shindano hilo; alikuwepo Valis Maembe, Mwasiti na Isha Mashauzi.
zaidi kwa kuwataka wajasiriamali wakina mama wa Mtwara kutumia fursa mbalimbali ili kuongeza kipato chao na kuacha suala la utegemezi kotoka kwa waume zao. Uzinduzi wa Mama shujaa wa chakula ulihudhuriwa na wasanii mbalimbaliwaliotoa burudani kwa wakazi waliofika katika uzinduzi wa shindano hilo; alikuwepo Valis Maembe, Mwasiti na Isha Mashauzi.
Shindano la mama shujaa wa chakula lililoanzishwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam lililoanzishwa hapa nchini mnamo mwaka 2011 lenye lengo zaidi ya kumsaidia mwanamke kujitambua zaidi katika haki zake mbalimbali na kujitambua kama mwanamke na kumuinua kiuchumi.
↧
RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG AWASILI TANZANIA
Ndege iliyombeba Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. |
Ndege iliyombeba Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang ikiwa imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe wakishuka kutoka kwenye ndege mara walipowasili katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. |
(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)
↧
↧
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI TUKIO LA KIHISTORIA LA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa risala yake ya ufunguzi kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni katika tukio lililoandaliwa na Kazi Services Ltd kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri nchini (ATE) na kudhaminiwa na mdhamini Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Balozi Dk Asharose Mtengeti Migiro akitoa ushuhuda wake wa namna alivyoweza kufanikiwa katika maisha pamoja na vikwazo vingi kwenye mfumo dume, kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni katika tukio lililoandaliwa na Kazi Services Ltd kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri nchini (ATE) na kudhaminiwa na mdhamini Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wakuu wa tukio hilo la kihistoria kupata kutokea kwa kina mama Shirika la Nyumba la Taifa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, Susan Omari akisalimiana na washiriki wenzake kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni katika tukio lililoandaliwa na Kazi Services Ltd kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri nchini (ATE) na kudhaminiwa na mdhamini Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, Susan Omari katika picha ya pamoja na washiriki wenzake kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni katika tukio lililoandaliwa na Kazi Services Ltd kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri nchini (ATE) na kudhaminiwa na mdhamini Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Washiriki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa katika meza ya pamoja kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni katika tukio lililoandaliwa na Kazi Services Ltd kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri nchini (ATE) na kudhaminiwa na mdhamini Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Washiriki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa katika meza ya pamoja kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni.Washiriki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa katika meza ya pamoja kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni.
Washiriki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa katika meza ya pamoja kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasilia ukumbini na kusalimiana na kina mama.
Washiriki kina mama kutoka kada mbalimbali wakifuatilia jambo kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni
Washiriki kina mama kutoka kada mbalimbali wakifuatilia jambo kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni
Washiriki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa katika meza ya pamoja kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni
Washiriki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa katika meza ya pamoja kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Shirika la Nyumba, Lilian Reuben akiwa na mmoja wa watoa mada kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni.
Mkuu wa Kittengo Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Nyumba la Taifa, Fatuma Chillo akitoa neno la mdhamini mkuu wa Shughuli hiyo Shirika la Nyumba la Taifa ambapo aliwahimiza kina mama kujiimarisha kwa kumiliki nyumba kama uwekezaji wenye tija katika familia.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, Susan Omari akipokea cheti cha utambuzi wa udhamini mkuu wa tukio hilo kubwa kabisa kupata kutokea nchini.
Mwakilishi kutoka NBC akipokea cheti cha utambuzi wa udhamini wa tukio hilo kubwa kabisa kupata kutokea nchini.
Washiriki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa katika meza ya pamoja kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni
↧
PROF. MBARAWA; TUMIENI DATA CENTRE KUTUNZA TAARIFA ZENU
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akionesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mfumo wa ufatiliaji wa kielektroniki katika jengo la kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitizama kwa karibu mtambo wa kuratibu usalama katika kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha kwanza kujengwa nchini kitatunza taarifa za Serikali na sekta binafsi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo hicho cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa (data centre) kutunza taarifa zao ili kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia wakati wote.
Akizungumza baada ya kukagua kituo hicho kinachosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sekta ya Mawasiliano amesema asilimia 75 imetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na asilimia 25 itatunza taarifa za Serikali.
Waziri Mbarawa amezitaka taasisi za Benki, Simu, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA) kutembelea kituo hicho kujifunza mifumo ya uhifadhi taarifa na kujiunga ili kunufaika na huduma za kituo hicho.
Amesema huduma ya mtandao katika kituo hicho imeimarishwa kutokana na kuunganishwa na mkongo wa taifa na hivyo itawarahisishia wateja wake kuweka na kuchukua taarifa kwa haraka.
Kituo hicho ambacho ni cha kwanza kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni fursa mpya kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji kinalimikiwa na Serikali.
↧
BAADHI YA WAFANYAKAZI WANAUME WA VODACOM TANZANIA WAELIMISHWA JINSI YA KUWEKEZA KWA MTOTO WA KIKE.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Evans Lyimo(kushoto)akimuuliza swali mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Chris Mauki(hayupo pichani)wakati alipokuwa akiongea na wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo kuhusiana na jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Chris Mauki(kulia)akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa Vodacom Tanzania ya jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki(kulia)baada ya kutoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo ya jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike ikiwa katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakimsikiliza Mtaalamu wa Masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki(hayupo pichani)wakati wa kuelimishwa kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo,Jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike ikiwa katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
↧
KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI CHA MKOA WA LINDI CHAFANYIKA
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Jordan Rugimbana akisoma hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa wa Lindi.
Wajumbe wa Kikao cha Ushauri cha mkoa wa Lindi.
Mbunge wa Jimbo la Lindi mjini Mhe. Hassan Kaunje akichangia maoni yake kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Lindi.
↧
↧
RAIS WA ZANZIBAR AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA VIETNUM, AKUTANA NA MAALIM SEIF
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akipofika kwa mazungumzo na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake (kushoto) wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Truong Tan Sang jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwa nchini kwa ziara ya Kikazi,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akiagana na mgeni wake Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(katikati) mawair mbali mbali wa Vietnum walioungana na Rais Truong,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akifuatana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Augustin Mahiga,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam jana akiwa katika mapumziko baada ya kuugua kwa matatizo ya kiafya,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad jana katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam alipofika kuonana nae kiwa katika mapumziko baada ya kuugua kwa matatizo ya kiafya,[Picha na Ikulu.]
↧
DKT. POSSI AZINDUA KITABU CHA JINSI YA KUONDOKANA NA UMASIKINI
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (Katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (wa pili Kushoto) akionesha kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi katika uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dare s Salaam Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli wa pili kulia ni Prof Lician Msambichaka Mhariri Mkuu wa kitabu hicho na kulia ni Prof Delphin Rwegasira kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi ( wa pili kulia) akionesha kitabu pamoja na Mhariri Mkuu wa kitabu hicho nkwa washiriki na waandishi wa habari Prof Lician Msambichaka katika uzinduzi wa kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli na kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sayansi na Jamii(UDSM) Prof Godius Kahyarara.
Baadhi ya washiriki toka Idara ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (Hayupo Pichani) wakati kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa uchumi kutoka Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam mara baada ya kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
………………………………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi ,MAELEZO
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi amezindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dkt Abdallah Possi amesema amefurahishwa sana kuona wasomi wa Tanzania wakijitolea muda wao na nguvu zao kushirikiana na Serikali katika kuondokana na umasikini ili tuelekee katika ustawi wa taifa.
“ Kitabu hiki kimekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya awamu ya tano imejikita katika mapinduzi na maendeleo katika sekta ya viwanda ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi nyingi duniani kwa sasa, hivyo tunaahidi kushirikiana na watafiti mbalimbali katika kutoa ufumbuzi wa changamoto zinazotukabili katika kuondokana na umasikini,”Alisema Dkt. Possi.
“ Nimekisoma hiki kitabu kwa ufupi na kuonda ni jinsi gani kitaweza kutusaidia katika mapambano dhidi ya umasikini lakini napenda kuwapa changamoto kuwa kazi hii ya kupambana na umasikini isiwe katika vitabu tu na sera bali iwe katika utekelezaji” Aliongeza Dkt Possi.
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa watafiti wa mambo ya uchumi wanatakiwa kuwashirikisha pia watu wenye ulemavu katika harakati za kuondokana na umasikini kwa kuwashirikisha katika uundwaji wa sera na utekelezaji wake katika kuleta maendeleo ya taifa.
Aidha Mhariri mkuu wa kitabu hicho, Prof Lucian Msambichaka amesema dhima kubwa ya kitabu hicho ni utekelzaji wa Sera,Mipango, Sheria na majukumu mbalimbali yahusuyo maendeleo kwa taifa na kuongeza kuwa kitabu hicho pia kimetoa njia bora na muafaka wa kukuza sekta ya viwanda, kuboresha huduma za jamii, kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na jinsi gani Tanzania inavyoweza kunufaika na maliasilia zake katika kujileta maendeleo.
Kitabu hiki kimeandaliwa na Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kudhaminiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Kimeshirikisha waandishi zaidi ya 20 na kina kurasa zaidi ya 400 ambazo zimeelezea kwa kina namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kuondokana na umasikini na kuelekea katika ustawi.
↧
WATANZANIA WAMEASWA KUWA NA TABIA KUWEKEA AKIBA BENKI.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma
Watanzania wameaswa kujenga tabia ya kujiwekea akiba kupitia mabenki kwa manufaa yao na taifa kwa kwa ujumla ikiwa ni mchango wao katika kutekeleza kaulimbiu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kufikia malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo endelevu.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Fedha na Utawala kutoka Bodi ya Bima na Amana (DIB) iliyo chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Richard Malisa wakati akitoa mada juu ya bodi hiyo katika semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi hao katika kuandika, kutoa na kusambaza habari za sekta ya uchumi biashara na fedha.
“Pesa zinapowekwa na kuwa benki hutumika kuchangia kuinua na kuimarisha usalama wa akiba ya mtu binafsi na kwa upande wa nchi zinatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuinua sekta ya elimu, afya, maji, ujenzi wa barabara na kilimo” alisema Malisa.
Katika kuonesha umuhimu wa bodi hiyo nchini, Malisa alisema kuwa taasisi ama mtu binafsi anapoweka pesa zake benki, hiyo ni amana kubwa na muhimu kwa kuwa tabia hiyo ya uwekaji pesa ina tija na inaongeza usalama wa pesa ambayo ni njia salama ikilinganishwa na kutumia njia za zamani za watu kuweka pesa kwenye godoro ambayo sio salama.
Faida nyingine za mtu binafsi ama taasisi kuweka pesa zao benki ni kuongeza mtaji wake kwa kupata riba kulingana na muda pesa hizo zinapokuwa benki na mteja anauhakika pesa yake ipo salama kwa kuwa ipo mikononi mwa Bodi ya Bima na Amana endapo litatokea tatizo lolote kwenye benki alipoweka pesa zake.
Katika kufanikisha na kutekeleza majukumu yake, DIB inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uelewa mdogo wa mtu mmoja mmoja katika masuala ya kibenki na fedha kwa undani wake ili aweze kufanya maamuzi yatakayomfanya awe bora zaidi kiuchumi ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kufahamu masuala ya kibenki na fedha ikiwemo kuongeza nidhamu ya matumizi.
Akitolea mfano Malisa amewaasa Watanzania wawe makini wanapochukua mikopo ambapo alisema kuwa watu wasikope kwa kufuata mkumbo ama kwa shinikizo fulani, bali wakepo kwa lengo la kuwekeza ili kuinua hali zao za kiuchumi katika maisha.
Hadi kufikia Juni 30, 2015 Bodi ya Bima na Amana ina akiba ya jumla ya kiasi cha Sh. biloni 220.5 ikilinganishwa na wakati ilipokuwa inaanzishwa na Serikali mwaka 1994 ambapo kianzio kilikuwa kiasi cha Sh. bilioni 1.5.
Aidha, katika semina hiyo Bw. Bernard Dadi kutoka Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa alisema kuwa BoT itaendelea kuboresha mifumo ya malipo ya hundi, kielektroniki ili kuongeza ufanisi kwenye mifumo hiyo, kuongeza usalama, kuongeza njia mbalimbali za malipo ili kupunguza malipo kwa fedha taslimu na kuongeza kasi ya malipo yaweze kuwa ya wakati kwa wateja popote walipo ndani na nje ya nchi.
Ili kuendana na wakati BoT kupitia Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa katika kuwahudumia wananchi katika masuala ya fedha na mabenki, imeanza kutumia mfumo wa TACH unaohusisha malipo ya hundi na malipo madogo ya kielektroniki (EFT) ambao umeanza kutumika tarehe 30 Aprili 2015 nchini.
Mfumo wa TACH unatumika na mabenki kutuma na kupokea hundi za wateja wao ikiwemo kulipa malipo madogo madogo yaliyojumishwa pamoja, mishahara, pension na hata malipo ya mtu mmoja mmoja.
Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa TACH nchini, awali hundi zilikua na muda tofauti wa siku za kuhakiki kulingana na kanda hali iliyopelekea muda wa siku za kuhakiki za hundi ulikua ni siku 3, 7 na 14 kutegemeana na kanda.
Baada ya kuanzishwa mfumo wa TACH hali imekuwa tofauti ambapo kwa mfumo huo sasa, hundi zote za Tanzania popote zitakapowasilishwa zitakuwa zinafanyiwa kazi ndani ya siku moja ya kuzihakiki hundi hizo (T+1) mpaka hapo itakapolipwa.
Hatua hiyo imewapunguzia muda wateja ili waweze watapata hela zao mapema na hivyo kuzitumia kwenye shughuli zao za kiuchumi.
Aidha, Bw. Dadi aliongeza kuwa nchi washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zenyewe zinatumia unaojulikana kama EAPS ikiwa ni jitihada za kuunda umoja wa kiuchumi miongoni mwa nchi hizo.
Mfumo huo wa malipo umeunganisha mifumo ya malipo (RTGS) ya nchi washiriki wa Afrika Mashariki ili kurahisisha malipo kati ya nchi washirika.
Kwa maana hiyo mabenki ya kibiashara ya nchi husika zina uwezo wa kutumiana na kupokea pesa za wateja wao kwa kutumia sarafu za nchi wanachama kufanya muamala.
Hadi sasa, mfumo huo umeunganishwa kwa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, wakati Burundi na Sudan ya Kusini wako mbioni kujiunga.
↧
UZINDUZI WA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOA WA SHINYANGA
Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma unaojulikana kwa jina la Public Sector Systems Strenghening (PS3) unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Lengo la mradi huo ni kuimarisha mifumo ya ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora,rasilimali watu,fedha utoaji taarifa na tafiti tendaji katika halmashauri za wilaya na taifa kwa ujumla.
Lengo la mradi huo ni kuimarisha mifumo ya ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora,rasilimali watu,fedha utoaji taarifa na tafiti tendaji katika halmashauri za wilaya na taifa kwa ujumla.
Mkutano wa uzinduzi huo utakaofanyika kwa siku mbili Machi 09,2016 hadi Machi 10,2016 umehudhuriwa na Kiongozi wa timu ya mradi,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga,wakuu wa wilaya,meya wa manispaa ya Shinyanga,wenyeviti wa halmashauri za wilaya,wataalam kutoka kutoka ofisi ya Waziri mkuu na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi,mashirika na taasisi za umma na binafsi-Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde yupo eneo la tukio ametusogezea picha 30 ,Tazama hapa chini
Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe ambaye pia ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma Public Sector Systems Strenghening(PS3) utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitano na utafanya kazi na serikali kuu pamoja na halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
Wakuu wa wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini,wa kwanza kushoto ni Vita Kawawa kutoka wilaya ya Kahama,akifuatiwa na Josephine Matiro kutoka wilaya ya Shinyanga na Hawa Ng’umbi kutoka wilaya ya Kishapu
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizindua mradi wa PS3 ambapo alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 13 nchini ambayo itanufaika na mradi huo ambapo alidai umeanza kwa wakati muafaka kwani sasa serikali iliyopo madarakani inataka mabadiliko katika kuhakikisha kuwa serikali inahudumia wananchi ipasavyo
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto) akifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.Rufunga alisema mradi huo utakuwa na tija kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga aliwataka watendaji wa serikali katika ngazi ya mkoa na mamlaka za serikali za mitaa kutoa ushirikiano katika kutekeleza mradi wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma kutokana na kwamba wao ndiyo wana mawasiliano ya moja kwa moja na wananchi wa kawaida.
Tunamsikiliza mgeni rasmi……
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID)
Meneja wa Mradi wa PS3 Dkt Emmanuel Malangalila akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo ambapo alisema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano umeandaliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na kutekelezwa na mashirika saba likiwemo shirika la Abt Associates Inc ambalo ndiyo mtekelezaji mkuu.
↧
↧
RAIS DK. MAGUFULI AIAGIZA BENKI KUU KUSIMAMISHA MALIPO ILI YAHAKIKIWE
↧
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ATEMBELEA GEREZA BIHARAMULO PAMOJA NA ENEO LINAKOJENGWA GEREZA LA WILAYA YA CHATO MKOANI GEITA
Kamishna Jenerali wa Magereza – CGP John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza Kamishna Msaidizi wa Magereza, Jaili Mwamugunda alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera ambapo leo Machi 10, 2016 ametembelea eneo kunakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato lililopo Mkoani Geita pamoja na Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wengine) ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akifurahia jambo pamoja na Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Ndomba walipokutana katika Kivuko cha Busisi kabla ya kuendelea na safari kuekelea Mkoani Kagera(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, Goleha Masunzu.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaban Ntarambe(kushoto) akiwa na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya wakielekea eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato mara baada ya Kamishna Jenerali wa Magereza kuwasili Wilayani Chato kabla ya kuelekea Mkoani Kagera
Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Omar Mtiga(wa pili kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kulia) nyumba mbili za Askari wa Jeshi la Magereza ambazo tayari zimekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wa pili kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Chato wakiaangalia moja ya Bweni la kulala Wafungwa/Mahabusu ambalo tayari limekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Kukamilika kwa Gereza hilo kutasaidia kutatua tatizo la Msongamano wa Wafungwa na Mahabusu katika Magereza ya Biharamulo na Gereza Muleba.
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akisaini katika kitabu cha Wageni alipotembelea Gereza la Wilaya ya Biharamulo katika ziara yake ya kikazi leo Machi 10, 2016.
Mkuu wa Gereza la Biharamulo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Gidion Kakulu akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza maeneo mbalimbali ya Gereza hilo katika ziara yake ya Kikazi leo Machi 10, 2016. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo ambao wameambatana na Kamishna Jenerali wa Magereza katika ziara yake ya kikazi.
↧
RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongeza na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea jambo na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana kutoka nje Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango baada ya kufanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016 Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa kaongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akiwasili makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza leo Machi 10, 2016
↧