Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 6864

BONANZA LA MICHEZO DAR LIVE LAFANA

Image may be NSFW.
Clik here to view.

Mhe. Angela Kizigha na Mhe. Faustine Ndugulile wakifanya mazoezi na klabu mwenyeji wa bonanza hilo, Magenge 20.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Mgeni Rasmi ambaye ni Mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki, Mh Angella Kizigha akiongea na wanajogging wa bonanza hilo.…
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Mhe. Angela Kizigha na Mhe. Faustine Ndugulile wakifanya mazoezi na klabu mwenyeji wa bonanza hilo, Magenge 20.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Angella Kizigha akiongea na wanajogging wa bonanza hilo.
Mhe. Angela Kizigha akipokea zawadi kutoka klabu mwenyeji ya Magenge 20.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Mhe. Faustine Ndugulile ambaye ni Mbunge wa Kigamboni akipozi na Mgeni rasmi, Angela Kizigha baada ya kupewa zawadi ya kikoi.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Timu ya Magenge 20 na Classic kabla ya mtanange wao kuanza.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Baadhi ya washiriki wa bonanza hilo wakiwa ndani ya Dar Live.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Wanabonanza wakiwa stejini ndani ya Dar Live.
BONANZA la michezo la kila mwezi linalofanyika katika Uwanja vya Burudani wa Dar Live Mbagala Zakhem limefanyika leo ambapo maelfu ya wanamichezo walijitokeza kushiriki bonanza hilo la aina yake.
Wenyeji wa bonanza hilo walikuwa ni klabu ya Magenge 20 ya Mbagala Kiburugwa jijini Dar, wakizikaribisha timu zote zilizokuwa zimepewa mwaliko wa kushiriki bonanza hilo.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo alikuwa ni Mheshimiwa Angela Kizigha, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki aliyekuwa ameambatana na mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na wanamichezo mbalimbali.
Licha mvua kubwa kunyesha lakini haikuweza kukata kiu ya wanamichezo waliokuwa wamejitokea kwani waliendelea kuserebuka ndani ya mvua bila kujali.
Hata hivyo burudani ya kufa mtu inatarajiwa kuangushwa jioni hii na bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Farasi’ chini ya Ally Choky ‘Mzee wa Ambulance’.
Vilabu  zaidi ya 180 vya mbio za pole ‘Jogging’ vimeshiriki ambapo michezo mbalimbali bado inaendelea kufanyika.
Washindi wanatarajiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali za michezo katika bonanza hilo la kufuru, aidha Tamasha hilo limedhaminiwa na PSPF, Mpango wa Damu Salama, Global TV Online, Kampuni ya A-One watengenezaji wa maji ya Maisha, Global Publishers Ltd, Dar Live pamoja na Benki ya Akiba Commercial (ACB).
(HABARI / PICHA: Jelard Lucas / GPL)

Viewing all articles
Browse latest Browse all 6864

Trending Articles