Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 6822

WANANCHI WOTE WENYE SIFA JIJINI DAR KUANDIKISHWA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA – TUME YA UCHAGUZI.

$
0
0
00
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaa , Raymond Mushi akifungua mafunzo
ya wasimamizi wa uandikishaji wa Wananchi katika Daftari la Kudumu la
wapiga kura kupitia mfumo wa BVR litakalofanyika Julai 16 hadi 25
mwaka huu.
0000
Wasimamizi wa uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga
kura katika jiji la Dar es salaam wakiwa katika mafunzo hayo.
………………………………………………….
Serikali imesema kuwa zoezi la uandikishaji wa wananchi katika Daftari
la Kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa BVR katika jiji la Dar
es salaam litafanyika kama ilivyopangwa kuanzia Julai 16 hadi 25 mwezi
huu kwa mafanikio makubwa kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanywa
na Tume ya uchaguzi kwa kushirikiana na Manispaa za mkoa huo.
Akizungumza wakati ufunguzi wa Mafunzo ya siku 2 ya wasimamizi wa
uchaguzi wa mkoa huo leo jijijini Dar es salaam, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw.Raymond Mushi amesema
lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wasimamizi wa Manispaa hizo
ili zoezi la uandikishaji wa wananchi katika daftari
 la kudumu la wapiga kura katika jiji la Dar es salaam lifanyike kwa
kiwango cha hali ya juu na kuzuia makosa yaliyojitokeza katika maeneo
mengine nchini.
Amewataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa viwango na weledi wa hali ya
juu ili kuzuia malalamiko kutoka kwa wananchi kwa kuhakikisha kuwa
kila raia mwenye sifa anaandikishwa katika daftari hilo.
Amesema kuwa wananchi wote watakaofika kwenye vituo kujiandikisha
wahakikishe kuwa wana taarifa muhimu kuhusu uraia wao pia wahakikishe
kuwa wanafuata taratibu zilizowekwa na Tume ili waweze kuandikishwa.
"Natoa wito kwa wananchi wote waliokidhi viwango vya kupiga kura
na wale watakaofikisha umri wa kupiga kura ifikapo 25 Oktoba 2015
wajitokeze kwa wingi maana wote wataandikishwa"Amesisitiza.
Aidha, amewataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa weledi, kutoa
ufafanuzi na elimu kwa wananchi pale inapobidi wakati wa ukusanyaji wa
taarifa zao na kuepuka kutumia lugha ya
 kuudhi ili kazi hiyo iwe rahisi na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza
kwa wingi katika kujiandikrsha na kuepuka vitendo vya vurugu na siasa
zinazoweza kuleta machafuko katika vituo vya uandikishaji,
Ametoa wito kwa baadhi ya wanasiasa watakaofika kujiandikisha kwenye
daftari la kudumu kuepuka kuingilia zoezi hilo kwa kuwa wao sio
watumishi wa Tume ya uchaguzi.
"Kuna maeneo nchini baadhi ya wanasiasa wamekuwa chanzo cha
kusababisha vurugu kwenye vituo vya uandikishaji, wao kama raia wanalo
jukumu la kufika kujiandikisha na kuangalia watu wanaojiandikisha kama
sehemu ya haki na wajibu wao kufuatilia ufanisi wa zoezi hilo na sio
kuingilia kazi za wataalam wa Tume"
Kwa upande wake Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Tume ya Uchaguzi Bw.
Joseph Mally, Afisa Amesema kuwa Mafunzo hayo ya siku 2 yaliyohusisha
wasimaizi 36 wa uchaguzi ngazi ya jimbo kwa manispaa zote tatu Ilala,
Kinondoni na Temeke ambao nao watatoa mafunzo hayo
 kwa wasimamizi wa Kata 36, ujazaji wa Fomu na matumizi ya mashine za BVR.
Amesema wao kama Tume ya Uchaguzi watahakikisha kuwa wanatembelea
vituo vyote vya uandikishaji ili kukabiliana na changamoto mbalimbali
zitakazojitokeza.
Aidha kwa kuzingatia wingi wa idadi ya watu katika jiji la Dar es
salaam kutakuwa na mashine 3500 zitakazofanya kazi katika vituo 1000
huku kukiwa na wataalam zaidi ya 600 waliopatiwa mafunzo kwa lengo la
kukamilisha kazi hiyo na kukabiliana na changamoto zilizojitokeza
katika maeneo mengine.
"Kwa upande wa Tume tunaendelea kujipanga ili kuhakikisha kuwa
changamoto zilizotokea katika maeneo mengine hazitokei, tunatoa wito
kwa wananchi watakaofika kwenye vituo kuandikishwa wawe wamekidhi
vigezo vilivyowekwa kulingana na vielelezo vya uraia, na umri"
Amesema.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo kutoka Manispaa za Temeke,
Ilala na Kinondoni wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati
 wa mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo ya siku 2 yanawajengea
uwezo wa kuelewa namna ya kuandikisha wapiga kura, ujazaji wa fomu
,uelewa wa sifa za mtu anayestahili kuandikishwa na matumizi ya
mashine za BVR.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 6822

Trending Articles