Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue (kulia) akisalimiana na Waziri wa Fedha wa zamani na Mbunge wa Kilosa Mhe. Mustafa Mkulo alipowasili kwenye viwanja vya bunge jana.
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu (kulia) akizungumza jambo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai jana mjini Dodoma kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni waliofika kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika jana katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Mhe. Anna Abdallah akimfariji mume wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa mbunge wa Ukonga aliyefariki usiku wa kuamkia Juni 2 nyumbani kwake mjini Dodoma.
Waheshimiwa Wabunge na baadhi ya watu mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya bunge jana mjini Dodoma kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga.
Mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga ukiwasili kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akitoa salam za bunge kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Mchungaji Mshana Samweli wa KKKT Jimbo la Dodoma akitoa neno kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakiwa kwenye hali ya majonzi mara baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bibi Chiku Galawa wakiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa
Wabunge Mhe. Anna Abdalla (kushoto) na Mhe. Ester Bulaya wakiaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu kwenye viwanja vya bunge jana mjini Dodoma wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Martha Mlata akiimba kwa hisia wimbo wa maombolezo kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika jana katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakitoa pole kwa wanafamilia wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge jana mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA FATMA SALUM – MAELEZO