WATU 18 wamepoteza maisha papo hapo kwa kuteketea na moto huku wengine 11 wakijeruhiwa vibaya kwa moto kufuatia magari mawili kugongana ambayo ni Basi Scania mali ya kampuni ya Nganga lililosajiliwa kwa namba T373 DAH na gari ;la mizigo Mistubishi Fuso T164 BKG.
Ajali hiyo imeelezwa kutokea majira ya asubuhi saa mbili katika Kijiji cha Msimba, Tarafa ya Mikumi, Wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Polisi mkoani Morogoro kupitia kwa Kamanda wake, Leonald Paulo imesema
chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Basi la Nganga kuendesha gari kwa mwendo
kasi na kulipita gari lillilo mbele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha ajali hiyo.
Kamanda Paulo aksema basi lilikuwa limepakia pikipiki katika buti na ambayo ilikuwa na mafuta hivyo baada ya kugongana palitokea mlipuko na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza basin a lori hilo.
Mbali na abiria waliokufa ni madereva wa magari yote mawili walioteketea kabisa na moto huo na abiria walioshindwa kujiokoa na majeruhi takribani 11 walikimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizzito Mikumi.