Naibu Waziri wa fedha na Uchumi Mh. Mwigulu Nchemba akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya miamala ya kifedha ya Airtel Money na Benki ya NMB katika hoteli ya  Selena jijini Dar es Salaam jana.
 Kaimu mtendaji  mkuu wa Benki ya NMB Tom Borghols akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya miamala ya kifedha ya Airtel Money na Benki ya NMB katika hoteli ya  Selena jijini Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi mtendaji wa  Airtel  Sunil Colaso akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya miamala ya kifedha ya Airtel Money na Benki ya NMB katika hoteli ya  Selena jijini Dar es Salaam jana.Â
Naibu waziri wa fedha   na Uchumi Mh. Mwigulu Nchemba (katikati) akizunzindua  huduma ya Airtel money  na Benki ya NMB wanaoshuhudia uzinduzi huo kulia ni  Kaimu mtendaji  mkuu wa Benki ya NMB Tom Borghols,  kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa  Airtel Sunil Colaso.(Picha zote na Emmanuel Massaka.
Na Avila Kakingo Globu ya Jamii.
Wateja wa benki ya NMB  wamerahisishiwa  kazi kutokana na  benki hiyo kuungana na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania  kwenye upande wa miamala ya fedha kwa urahisi na usalama zaidi.
Akizungumza Naibu Waziri wa fedha   na Uchumi Mh. Mwigulu Nchemba katika hoteli ya   Serena jijini Dar es Salaam jana , amesisitiza kuwa huduma za Fedha kupitia simu za mkononi ni mhimu katika kuliletea maendeleo Taifa. Mwigulu amesema kuwa ukuaji wa uchumi nchini umewasukuma watanzania kutumia simu zao za mkononi kupata taarifa kuhusu akaunti zao za benki popote pale walipo na wakati wowote.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu ya Airtel,Sunil Colaso, alisema kuwa umoja huu ni ishara ya mageuzi katika matumizi ya Teknolojia katika kuboresha masisha ya watanzania kupitia simu za mkononi.
Kwa njia hii wateja wa Airtel na benki ya NMB kwa pamoja wanaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money kwenda kwenye akaunti zao za NMB. Alisema  Colaso.
 Pia katika uzinduzi huo utasaidia wateja wa Airtel kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Benki na za NMB.