Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Simba kabla ya mpambano wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya Mtibwa Sugar katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar mchezo uliofanyika juzi Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Wananchi na Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia kwa makini mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa juzi katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo simba iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa matuta 4-3, [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Simba Hassan Izhaka baada ya kuifunga Mtibwa kwa matuta 4-3 mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi uliofanyika juzi ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan Studium,[Picha na Ikulu.]
Wachezaji wa Timu ya Simba wakisherehekea ushindi wao baada ya kuwafunga kwa matuta timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi 4-3 katika uwanja wa Amaan studium Mjini Unguja juzi katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Mashabiki wa Timu ya Simba Wengundu wa Msimbazi walipokuwa katika jukwaa la Saa katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja wakishangilia timu yao ilipocheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika fainali ya kombe la Mapinduzi,Timu hiyo ya Simba ilishinda kwa matuta 4-3ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk (kushoto) wakiangalia mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa jana katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo Simba iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa matuta 4-3 , [Picha na Ikulu.]