Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 6805

VITABU VYA AIRTEL VYAIBUA ARI YA WANAFUNZI GUNGU SEKONDARI KIGOMA

$
0
0
……………………………………………………………….
 Meneja huduma za Jamii wa Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel
Tanzania Bi Hawa Bayumi amesema nguvu kazi ya wananchi wenye ujuzi na
elimu inahitajika nchini, hivyo wanafunzi wa shule za sekondari wana
wajibu wa kuitumia elimu kama ngazi ya kuliwezesha taifa kuwa na
maendeleo
Bayumi aliyasema hayo wakati Akikabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi
kwa Afisa Elimu vifaa na Takwimu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Bwana
Yalagwila Gwimo kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Gungu Mkoani
Kigoma, Bayumi amesema serikali haiwezi kufanya kila kitu,wanafunzi
wanatakiwa kutumia fursa hii kupanua uelewa wao kupitia vitabu
vinavyotolewa na kampuni yake
 “Sisi kama Airtel tumetekeleza jukumu letu la kutoa vitabu kwa shule
za Sekondari na tunatarajia wanafunzi mtasema kufeli sasa basi baada
ya kuwekewa mazingira mazuri ya kupata vitabu vya kiada na
ziada”…Alisema Bayumi
 Amesema taifa bado halijafikia kiwango cha kujivunia cha kuwa na
wasomi wengi wa fani ya Sayansi, hivyo Airtel inasisitiza wanafunzi
wafanye jitihada katika masomo hayo
 “Tunapotengeneza mazingira mazuri kwa mwanafunzi pia tunatengeneza
mazingira mazuri kwa waalimu kwa kutoa vitabu vya kufundishia ambavyo
vinakubalika na wizara ya elimu”Alisema Bayumi.
 Kwa upande wake Mwalimu Mkuu  wa Shule ya Sekondari Gungu Bwana
Alberto Dobeye mbali na kuishukuru kampuni ya Airtel chini ya mpango
wa “Shule Yetu” kwa kutoa vitabu hivyo ameiomba serikali kuharakisha
ujenzi wa maabara shuleni hapo
 “Tunawashuru sana Airtel kwa vitabu hivi..lakini mkubuke kupata
vitabu ni jambo moja na maabara ni jambo jingine,serikali ijitahidi
kujenga maabara hapa shuleni ili wanafunzi wasome na kufanya majaribio
ya Vitendo” Alisema Mwalimu Dobeye
 Kwa upande wake Afisa Elimu vifaa na Takwimu wa Manispa ya Kigoma
Ujiji Bwana Yalagwila Gwimo amesema vizuri wanafunzi wakajikita kusoma
vitabu kwa lengo la kupanua ulewa wao na hivyo kuwa katika nafasi
nzuri ya kuongeza ufaulu
 Nao Wanafunzi Kassim Abdallah, na Rosemary Christopher kwa  kwa niaba
ya wenzao wameipongeza kampuni ya simu ya Airtel kwa msaada huo na
kwamba vitabu hivyo vitachochea Ari za wanafunzi kuongeza bidii katika
masomo ili kufikia lengo la ufaulu kwa kupata alama za juu.
 Msaada huo wa Vitabu vilivyotolewa ni mwendelezo wa shughuli za
huduma kwa jamii zinazotelewa na Airtel kupitia mradi maalumu wa Shule
yetu unaoziwezesha shule mbalimbali kutapa vitabu vya kiada na kiada,
mpaka sasa shule zaidi ya 1000 zimeshafaidika na mpango huo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 6805

Trending Articles