Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Zanzibar, Haji Ambar Khamis.
MAKAMU Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Zanzibar, Haji Ambar Khamis, leo amedondoka kutokana na matatizo ya moyo na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Baada ya kufikishwa hospitalini hapo, Mhe. Ambar alipimwa na kukutwa presha yake ipo juu ambapo alipelekwa katika chumba namba 7 kwa mapumziko.
Baadaye alipelekwa katika kipimo cha moyo ambapo amekutwa ana tatizo hivyo kushauriwa aanze matibabu mara moja. Mhe. Ambar baadaye aliruhusiwa. SOURCE: GPL