Jaji Venance Bahati ( kulia) na Jaji Constancia Gabusa (kushoto) wakijadiliana jinsi ya kuanza zoezi la kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni mara baada ya timu hiyo kuwasili katika wilaya ya Handeni kwa ajili ya zoezi hilo. Zoezi hili linahusisha makampuni yanayojishughulisha na shughuli za madini, gesi na mafuta ambapo mshindi katika utoaji wa huduma bora kwa jamii na uwezeshaji atakabidhiwa tuzo yake mapema Novemba, mwaka huu.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Handeni Bw. Dawson Temu akielezea jinsi makampuni ya utafutaji madini yanavyochangia katika huduma za jamii katika wilaya ya Handeni mbele ya timu ya majaji (hawapo pichani) ofisini kwake.
Jaji Constancia Gabusa (kushoto) na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Handeni Bw. Jared Obado (kulia) wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Afisa Utawala wa Wilaya ya Handeni Upendo Magashi (hayupo pichani)
Jaji Venance Bahati (kushoto) akikagua moja ya ofisi za waalimu katika shule ya msingi ya Nyasa zilizojengwa na kampuni ya utafutaji wa madini ya Canaco katika zoezi la kutathmini miradi iliyofadhiliwa na kampuni hiyo
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Nyasa ( wa pili kutoka kulia) ambaye jina lake halikupatikana mara moja akielezea mchango wa makampuni ya utafutaji wa madini katika huduma za jamii ndani ya kijiji hicho.
Mkuu wa Mradi wa Kampuni ya Utafutaji wa Madini ya Canaco Bw. John Holana (kulia) akielezea mchango wa kampuni hiyo katika uendelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kijiji cha Nyasa ikiwa ni pamoja na maji, shule na mkakati wa kujenga kituo cha afya. Kushoto ni mmoja wa majaji Bi. Constancia Gabusa.
Mkuu wa Mradi wa Kampuni ya Utafutaji wa Madini ya Canaco Bw. John Holana akitoa maelezo mbele ya majaji pamoja na wajumbe wengine wa kijiji cha Nyasa mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo.
Mjiolojia Mkuu kutoka Kampuni ya Utafutaji wa Madini ya Douglas Lake Minerals Bw. Godfrey Bitesigirwe akielezea changamoto wanazokumbana nazo katika utoaji wa huduma bora kwa jamii inayoizunguka kampuni hiyo mbele ya majaji waliotembelea kampuni hiyo (hawapo pichani) kwa ajili ya kuendelea na zoezi la kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Jaji Constancia Gabusa akitoa ushauri kwa kampuni ya Utafutaji wa Madini ya Douglas Lake Minerals jinsi ya kukabiliana na changamoto katika utoaji wa huduma bora kwa jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika mipango ya miradi ya maendeleo
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi ya Nyasa Bw. Ali Mhada akielezea mchango wa kampuni ya utafutaji wa madini ya Canaco katika kutoa ufadhili kwa wanafunzi waliofanya vizuri kama mkakati mmojawapo wa kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuwa wataalamu wa baadaye na kufanya kazi katika kampuni hiyo.