Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 6822

KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET YAZINDUA SAFARI ZAKE KATI YA (DAR – HARARE-DAR) USIKU HUU MJINI HARARE

$
0
0
01
Waziri wa Usafirishaji wa Zimbabwe Dr. Orbet Mpofu wa tatu kutoka kulia na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Balozi Adadi Rajabu wa tatu kutoka kushoto wakiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya Zimbabwe na wakuu wa kampuni ya Fastjet wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za kampuni hiyo kati ya Tanzania na Zimbabwe unaofanyika usiku huu kwenye uwanja wa ndege wa Harare Fullshangwe Inakuletea matukio haya moja kwa moja kutoka Zimbabwe Harare usiku huu. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-HARARE – ZIMBABWE.
1
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya Fastjet wakipeperusha bendera ya Zimbabwe mara baada ya ndege hiyo kutua kwenye uwanja wa ndege wa Harare kwa mara ya kwanza nchini Zimbabwe.
2
Balozi mdogo wa Zimbabwe nchini Tanzania Balozi Walter Sande akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Balozi Adadi Rajabu mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Harare usiku huu.
3
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Geofrey Meena kulia na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano bodi ya utalii Geofrey Tengeneza katikati wakisalimiana na wenyeji wao mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Harare wakiwa ni miongoni mwa abiria waliosafiri na ndege ya Fastjet wakati wa uzinduzi wa safari zake katika ya Tanzania na Zimbabwe.
5
Viongozi wa serikali ya Zimbabwe na Tanzania pamoja na wakuu wa kampuni ya Fastjet wakipiga picha ya pamoja mbele ya ndege ya Fastjet mara baada ya ndege hiyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Harare.
6
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo usiku huu
7
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo inayoendeea usiku huu.
8
Mwanamuziki Tariro Chaniwa wa nchini Zimbabwe akiimba nyimbo za taifa za Zimbabwe na Tanzania wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo ya uzinduzi wa safari za kampuni ya ndege ya Fastjet.
9
Ndege ya Fastjet ikiwa imeegeshwa katika uwanja wa ndege wa wa kimataifa wa Harare nchini Zimbabwe.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 6822

Trending Articles