Quantcast
Channel: ARAWAY MEDIA TANZANIA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 6821

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WACHANGIAJI DAMU SALAMA DUNIANI KWA PAMBANO LA MPIRA WA MIGUU KATIKA KIWANJA CHA AMANI

$
0
0
1
Waziri wa Kilimo na Mali Asili Dkt. Sira Ubwa Mamboya akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa ya Jangombe na Kimbunga ya Tazari kabla ya kupambana katika mchezo maalum wa maadhimisho ya siku wachangiaji damu salama katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar. Wa kwanza (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.
Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
2
Meneja wa Mpango wa Damu Salama Zanzibar Dkt. Mwanaheri  Ahmed Abdulrahim akizungumza na wananchi na wanamichezo katika maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama katika kiwanja cha Amani Mjini Zanzibar.
3
Wachezaji wa Timu ya Kimbunga ya Tazari ya Mkoa wa Kaskazini Unguja wakishangiria ushindi wao baada ya kuilaza timu ya Taifa ya Jangombe mabao 3-2 katika pambano maalum la siku ya wachangiaji damu salama liliofanyika Uwanja wa Amani.
4
Waziri wa Kilimo na Mali Asili Dkt. Sira Ubwa Mamboya akimkabidhi ngao mmoja wa wachangiaji  bora wa damu salama Abdalla Muhd Kassim kwa niaba ya wenzake watatu ambao wamechangia mara 40 kila mmoja.
5
Waziri wa Kilimo na Mali Asili Dkt. Sira Ubwa Mamboya akimkabidhi kombe la ushindi Nahodha wa timu ya Kimbunga Shaaban Ramadhan Kangeta baada ya kuilaza Taifa ya Jangombe Mabao 3-2 katika pambano la siku ya wachangiaji damu salama liliofanyika uwanja wa Amani.
6
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama Dkt. Sira Ubwa Mamboya  na viongozi wa Wizara ya Afya na baadhi ya wachangiaji damu salma kutoka Taasisi mbali mbali na watu binafsi katika maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu salama yaliyofanyika Uwanja wa Amani Zanzibar

Viewing all articles
Browse latest Browse all 6821

Trending Articles