Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko jipya mjini Biharamulo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi akiwa katika ziara ya kikazi ya mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza.
Jana alimaliza ziaya yake mkoani Kagera na kesho anaanza mkoa wa Geita, Ziara hiyo ina lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015 inayotekelezwa na serikali na kuhimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi CCM akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano huo ambao umefanyika kwenye uwanja wa Soko jipya mjini Biharamulo.
Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika katika mkutano huo.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko Jipya mjini Biharamulo.![5 (2)]()

Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko Jipya mjini Biharamulo.
Huu niyo mradi wa maji wa kata ya Nyakahura ambao unadaiwa kujengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni moja lakini mpaka sasa hautoi maji na umejengwa chini ya kiwango.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongella mara baada ya kukagua mradi wa maji wa kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitafakari jambo wakati wa mkutano huo huku akiwa ameshika taarifa ya mradi wa maji wa Nyakahura uliojengwa kwa kiwango cha chini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wazee wa kijiji cha Nyakahura wakati alipowasili katika kijiji cha Nyakahura kwa ajili ya kukagua mradi wa maji
Mwananchi wa kata ya Nyakahura Majaliwa Issa akizungumza kwa uchungu mbele ya Kinana kuhusu uchakachuaji wa mradi huo ambao mpaka sasa wananchi wa kata hiyo wamegoma kuupokea kutoka kwa mkandarasi.
Wananchi wa kata ya Nyakahura wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kinana anayeonekana kwa mbali jukwaani wakati akiwahutubia na kujibu maswali yao.
Mitambo ya Tanesco Biharamulo ambayo inafua umeme unaotumika katika wilaya za Chato mkoani Geita na Biharamulo mkoa wa Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa meneja wa Tanesco Biharamulo Bw. Ernest Milyango wakati alipotembelea na kukagua mitambo hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo zaidi Kutoka kwa Meneja wa Tanesco Biharamulo Bw.Ernest Milyango kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongella.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata neno la mwisho kutoka kwa Meneja wa Tanesco Biharamulo Bw. Ernest Milyango.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkunga wa hospitali ya wilaya ya Biharamulo Bi. Lucy Silayo wakati alipotembelea na kukagua hudumza za hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Biharamulo Dr.Donasian Kamala.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa madirisha ya shule ya Ar-Rahman mjini Biharamulo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na walimu na viongozi mbalimbali wa shule hiyo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko Jipya
Baadhi ya akina mama wakifuatilia kwa makini wakati Kinana akiendelea kuhutubia
Viongozi mbalimbali wakiwa wamekaa meza kuu.