Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Tanga akiwa amebeba Mwenge kuazimisha Mbio za Mwenge wilaya Muheza.
Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa Wa Tanga akishiriki kikamirifu kwenye ngoma siku ya kupokea mwenge wilayani Muheza.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Tanga Akikagua Mradi wa Ufyatuaji Tofali za zakufungamana za gharama nafuu kikundi cha Mali Hai Wilayani Muheza ambacho kilitembelewa na Mwenge wa Uhuru.
Meneja wa Shirika La Nyumba mkoa wa Tanga akiwa na maofisa wa ardhi wa Halmashauli ya wilaya ya muheza kabla ya kupokea mwenge wilaya ya Muheza.
Vijana wa kikundi cha Mali Hai wakichuja udongo kujiweka tayari kwaajili ya mapokezi ya mbio za mwenge.
Askari wa Mbio za Mwenge akiuweka mwenge mahala pake huku kiongozi wa Mbio za Mwenge (Juma khatibu Chum) na Mkuu wa Wilaya ya Muheza (Mh.Esteria Kilasi) wakishuhudia tukio hilo.
Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tanga.(Isaya Mshamba) akisalimiana na mkuu wa wilaya ya muheza na Kiongozi wa Mbio za Mwenge baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili kwenye eneo la tukio.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Akimpongeza Meneja Wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Tanga (kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa) kwa Mchango Mkubwa unaotolewa na Shirika kwa jamii na hasa kuwasaidia Vijana kujiajiri na kuwainua kiuchumi kwa kuwapatia Mashine za ufyatuaji wa matofali ya kufungamana ya gharama nafuu.
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Tanga akitoa maelekezo kwa vitendo kwa maafisa wa Mbio za Mwenge jinsi ya ufyatuaji wa matofali.
Meneja akielezea ubora wa Tofali.
Meneja wa Mkoa akitoa maelekezo jinsi ya Kujengea Tofali za kufungamana.
Meneja wa mkoa,Mkuu wa Wilaya ya Muheza na kiongozi wa mbio za mwenge wakishiriki zoezi la upandaji miti.
K
utoka kushoto ni Meneja wa mkoa wa Shirika la Nyumba la Taifa (Isaya Mshamba),Kiongozi wa mbio za Mwenge (Juma Khatibu Chum),Afisa Utumishi Halmashauli ya wilaya ya Muheza na Mkuu wa Wilaya ya Muheza (Esteria Kilasi) wakiwa kwenye picha ya pamoja.