
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka, baada ya kuwasili Kijiji cha Kyamkwikwi, wilayani Muleba mkoani Kagera leo, kabla ya kupanda boti kwenda Kisiwa cha Bumbile wilayani Muleba, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera, juzi, Juni 7, 2015.
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akimsalimia Mbunge wa Mleba Kusini, Prof. Tibaijuka, baada ya yeye na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwasili Kijiji cha Kyamkwikwi, wilayani Muleba.
Kinana akisalimia wananchi, baada ya kuwasili Kijiji cha Kyamkwikwi.
Kinana akikagua ujenzi wa gati katika ziwa Victoria, katika eneo la Kyamkwikwi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiielekeza boti eneo la kutia nanga ili Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wasafiri nayo kwenda Kisiwa cha Bumbile.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda boti kutoka kijiji cha Kywamkwikwi kwenda Kisiwa cha Bumbile, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera.
Kinana na Nape (kulia) wakiwa na Prof. Anna Tibaijuka wakati safari ilipoanza kwenda Kisiwa cha Bumbile.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwa mtumbwi katika kijiji cha Katunguru, baada ya kutembelea visiwa zaidi ya vinne, katika wilaya ya Muleba.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimsikiliza kwa makini, Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka, alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofayika kijiji cha Katunguru, wilayani Muleba.
Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika Kijiji cha Katunguru.
Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika jana, kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera.
Prof. Anna Tibaijuka akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera.












Picha na Bashir Nkoromo.